Mchezaji, Olivier Giroud ameonekana kuwa katika mazungumzo mazito na kocha wake Arsenal Wenger wakati wa mazoezi ya mwisho kabla ya kujiunga na Chelsea kwa dau la paundi milioni 35.
View attachment 687043
Mchezaji huyo rai wa Ufaransa akionekana vema kama sehemu ya kikosi kitakacho ingia uwanjani hapo kesho siku ya Jumanne kuvaana na Swansea City mchezo wa ligi kuu ya England.
View attachment 687045
Giroud atalazimika kuondoka Emirates endapo Arsenal itakamilisha usajili utakao weka rekodi ndani ya klabu hiyo wa kumnasa mchezaji wa Borussia Dortmund straika, Pierre-Emerick Aubameyang.
View attachment 687046
Wakati wa mazoezi hayo Giroud ameonekana kuwa mwenye furaha na amani akiwa na kocha wake Wenger huku wakifanyiana maskhara ya hapa na pale.
Arsenal wanafurahia ujio wa Aubameyang kutoka Dortmund ambapo watagharimika kutoa paundi milioni 55.4 huku wakitarajia kunyakuwa paundi milioni 35 juu ya uhamisho wa Giroud kwenda Chelsea.
Uwe na adabu!MKITAKA WEBSITE YA KUBET INAYO TOA MIKEKA NA NI WEBSITE YA NJE NINA MAANA YA WALE WAZUNGU NGULI WA KUCHAMBUA NA KU RISK MIKEKA NA INATOA ASILIMI 98% NI WEWE MWENYEWE UKITAKA ODD ZOZOTE NI UN CHANGUA TU BONYEZA HAPA>>>>>> WINTIPS100.COM
Kweli ulipotea au Aubamayeng amekuleta mkuu, aje tu huyo tulikuwa tunatia huruma sana, yaani tunashinda kwa bahati tu
Karibu Arsenal Aubameyang.
Wakuu mpooo?
Dah nilipotea sana na tumemshwishi Arsene Wenger abadili msimamo wake kuhusu ubahili na amekubali kwa shingo upande.
Ameambiwa Arsenal ni moja ya timu kubwa duniani kwa uwezo wa fedha na ni lazima mwakani icheze Champions league.
Kwa kweli huyu mzee alitukakisha sana tamaa.
Lakini kwa kasi ya matumizi ya Manchester City ambayo imevuka pauni milioni 450 mpaka sasa ambapo wamemsajili Laporte kutoka Athletico Madrid, Wenger amekubali ukweli na ameanza kutumia pesa.
Ni ukweli usojificha kwamba mchezaji mahiri awe beki, kiungo au mshambuliaji sasa hivi unatakiwa utumie kuanzia wastani wa pauni milioni 47 kwenda juu.
Aubamenyang angalau atatusaidia kwa kipindi kilichobakia lakini Arsenal ya 2018/ 19 itakuwa ni Arsenal mpya.
Aubameyang ana miaka 28 miaka mitatu chini ya Olivier Giroud hivyo yupo kwenye peak na atatusaidia sana ukiondoa kupata majeruhi ya Premier League.
Richard amerudi na wapenzi wa Arsenal tusubiri mechi na Swansea ambao wiki mbili zilizopita waliifunga Liverpool goli 1-0.
Swansea si timu ya kuidharau hata kidogo na wapo kwenye relegation zone.
Dah ulivyoandika kwa kujidai hadi rahaAkitua Abu na mfumo wetu hakika hata timu iwe nzuri vipi lazima wakae tu.Unaanzaje kumzuia lacazate na abu atakuachaje huku ozil yupo ,mhtaryian anakuangalia tu asikudhuru.Angalia nyuma kati hapa kuna viungo wenye akili kama xchaka beki mnapohangaika kuwazuia foward yeye keshamuona golikipa anamuagizia mashine toka kati ya uwanja inagonga post ya juu inarudi uwanjani ozil anamalizia .Duuuuh karibuni emirates kwa burudani safi.
Kweli ulipotea au Aubamayeng amekuleta mkuu, aje tu huyo tulikuwa tunatia huruma sana, yaani tunashinda kwa bahati tu
Inatakiwa mtu amiminiwe nyingi Leo, na kwa mwendo huo nafasi ya 3 au pili itatuhusu mpaka mwisho wa msimuChama la wana hili hapa leo mzigoni
Hazikuhusu.....Mnavyoongea kwa uhakika habari za tetesi hadi mnatia huruma
Sasa huku si kwetuu kwanini tusiongeee, na wewe kaongee kunakokuhusuMnavyoongea kwa uhakika habari za tetesi hadi mnatia huruma
we jamaa una kipaji vha utangazaji, Tido matatizo yake yakiisha akuchukue tu!Akitua Abu na mfumo wetu hakika hata timu iwe nzuri vipi lazima wakae tu.Unaanzaje kumzuia lacazate na abu atakuachaje huku ozil yupo ,mhtaryian anakuangalia tu asikudhuru.Angalia nyuma kati hapa kuna viungo wenye akili kama xchaka beki mnapohangaika kuwazuia foward yeye keshamuona golikipa anamuagizia mashine toka kati ya uwanja inagonga post ya juu inarudi uwanjani ozil anamalizia .Duuuuh karibuni emirates kwa burudani safi.
Duh so far nimepitia kila taarifa nimekatiza vichochoro vyote vya habari imefika time watuambie ukweli ANAKUJA au HAJI maana tunaambiwa kapanda ndege kwenda London mara kaonekana uwanja wa mazoezi(Arsenal)
C'mooooon you Gunners malizeni hii kadhia maana bia ya baridi imekua ya moto sasa.