Rajab_Omar
JF-Expert Member
- May 15, 2016
- 16,481
- 27,185
Leo kulikuwa na mkutano wa mwaka wa wakurugenzi na watendaji wa arsenal London (annual general meeting)
Agenda mbalimbali zilijadiliwa ikiwamo kanuni, na pesa za uendeshaji wa klabu, uchaguzi wa mwenyekiti wa bodi ya watendaji na mustakabali wa klabu.
Sir Chips keswick amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa kamati ya utendaji.
Bodi pia iliulizia utendaji wa klabu upande wa uwanjani na wenger aliwakilisha makocha na madaktari wa wachezaji kujibu maswali
Kroenke kwa mara nyingine tena alisisitiza kuwa hayuko tayari kuiuza arsenal kwa yeyote.
Sir chips alikataa kusalimiana na na baadhi ya watu kwenye kikao baada ya kikao kuisha. Ni arsene pekee alibakia kusalimia mashabiki wakereketwa waliokuwa nje ya tukio.
Bodi ya wamiliki wa shares wengi walipinga sir chips kuendelea ndio maana hakuwasalimia
Pia wamiliki wengi walimpinga mtoto wa kroenke, josh
Gazidis aliwakilisha watendaji upande wa klabu na mahusiano ya nje. Na alisisitiza kuwa objectives za arsenal ni kushinda epl kwanza.
![]()
Dadeki!! Kama kawa Kroenke Ban Yake inaendelea Kwa Usmanov Kutokushiriki Katika Vikao Vya Bodi...
️