Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

IMG_3409.JPG

IMG_3408.JPG

Duh Kreonke kubali yaishe basi kuna maisha nje ya Arsenal.
 
Alisher Usmanov ametoa ofa ya Paund Bilioni 1.3 kununua hisa kubwa katika klabu ya Arsenal , kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports.

Imearifiwa kwamba anayemiliki hisa nyingi katika klabu ya Arsenal kwa sasa ni Stan Kroenke bado hajajibu chochote kuhusu ofa hiyo , lakini inatarajiwa kutupiwa kapuni.

Usmanov kwa sasa anamiliki asilimia 30 tu ya hisa katika klabu hiyo ya London na ana utajiri wa thamani ya Pauni Bilioni 11.2
b1e13f9f4909f7db7e1ff267944f1a55.jpg
 
Wenger atoa Onyo kwa Chelsea.

Arsene Wenger amewapongeza Chelsea kwa kutwaa Ubingwa wa EPL lakini amewaonya kwamba msimu ujao hautokuwa rahisi hasa ikizingatiwa kwamba watakuwa na mashindano ya UEFA pia.

The Blues wametwaa taji la pili la EPL ndani ya miaka mitatu bila ya kucheza Ulaya msimu huu na wanaweza angalau kumaliza juu kileleni kwa tofauti ya pointi 12 dhidi ya Gunners ambao wenyewe bado wanapigania kumaliza nafasi nne za juu.

Wenger anaamini kwamba timu kama Real Madrid na Bayern Munich wapo imara sana Ulaya kwasababu hawalazimiki kucheza katika kiwango cha juu sana katika ligi za nyumbani kupata matokeo baada ya Gunners kuondolewa hatua ya 16 katika mikono ya Wajerumani.

Kuelekea mechi ya EPL siku ya jumanne dhidi ya Sunderland Wenger amesema," Chelsea wamefanya vizuri. Hongera zao."

"Lakini katika misimu miwili iliyopita timu ambazo zilikuwa hazichezi Ulaya zimetwaa taji la EPL"

"Utakuwa msimu tofauti kwasababu watalazimika kucheza Jumamosi - Jumatano - Jumamosi kwasababu ya mechi za UEFA."

"Nahisi nchini Hispania, Real Madrid wanaweza kushinda mechi wakicheza katika daraja la wastani kuliko Uingereza. Labda pia ni wazuri kuliko sisi."

"Bayern pia ni sawa na Madrid - Wanatawala ligi ya Ujerumani kwa urahisi sana."
30aa5ee32ce17f2950c63fccc857a675.jpg
Up his ass!
 
Bora hta tusiende champions league maana ni vipigo tu kila mwaka so haina maana hta kushiriki!!
Kabisa, kama tumecheza kwa muda wa miaka ishirini na kufika mbali mara mbili tu, hatustahili kwa kweli. Ngoja tujaribu futuhi huku wenger akiendelea kuburuzwa, arsenal tutabadilika na kuwa tena timu ya kugombea vikombe wenger alitoka.
 
Dah natamani arsenal tupate kocha kma simeone ili tusajili wachezaji wa ''kazi kazi'' ili timu ipate muamko mpya kma enzi za mijitu kma lauren,cygan,vieira,campbell,keown n.k dah ila kwa kikosi hiki cha wauza sura kma bellerin,gibbs na Oxlade sioni wapi tunachukua ligi ndani ya karne hii
 
Ni wenger aondoke tu, aje mtu wa kazi kazi, Simeone akipewa na pesa ya kupata wachezaji anaowataka, timu itarudi kwenye heshima yake! Hii timu ya sasa wa kubaki ni Cech, Sanchez na Kolsielny!
 
Una maana goli 10 zinajirudia tena mwakani 😀😀😀😀...... huu ni uchochezi mkuu
Hawa jamaa tukiwa na wenger tumewashindwa, tulikuwaga tunadai sababu tunamaliza wa pili, tukimaliza wa kwanza ktk kundi wao wanakuwa wa pili, tunakutana nao na safari yetu inaishiaga hapo.
 
Ni wenger aondoke tu, aje mtu wa kazi kazi, Simeone akipewa na pesa ya kupata wachezaji anaowataka, timu itarudi kwenye heshima yake! Hii timu ya sasa wa kubaki ni Cech, Sanchez na Kolsielny!
Bellerin ni mzuri sana, Cech kachoka mno, bado tunamuhitaji Mtakatifu Carzola japo injury hua hazimwishi. Pia naamini kua Chamberlain ni aina ya mchezaji ambae akipata cocha kwenye hamasa anaweza kuleta matokeo. Wengine wote wasepe, hawana quality ya kuwepo Arsenal.
 
Dah natamani arsenal tupate kocha kma simeone ili tusajili wachezaji wa ''kazi kazi'' ili timu ipate muamko mpya kma enzi za mijitu kma lauren,cygan,vieira,campbell,keown n.k dah ila kwa kikosi hiki cha wauza sura kma bellerin,gibbs na Oxlade sioni wapi tunachukua ligi ndani ya karne hii
Lee Dixon, winterburn,Tony Adams, keown, hii ndio beki bora ya arsenal
 
Lee Dixon, winterburn,Tony Adams, keown, hii ndio beki bora ya arsenal
Dah walikuwa hatari sana hao..... afu mbele tukapata mtu kma ian wright, alan smith au thierry henry!!!! Mbona the invicibles class of 2004 itajirudia
 
Hawa jamaa tukiwa na wenger tumewashindwa, tulikuwaga tunadai sababu tunamaliza wa pili, tukimaliza wa kwanza ktk kundi wao wanakuwa wa pili, tunakutana nao na safari yetu inaishiaga hapo.
Kumbe nyie ni Arsenal wenzangu?
Ila mkuu barafuyamoto umepata maumivu mara dufu!
Huku Simba kule Arsenal,dah!

Back
Top Bottom