Tottenham watamkosa Dele Ali ambae jana aliumia goti alipokuwa mazoezini.
Hiyo itakuwa ni moja ya advantage kwa Arsenal kwani Alli huwa anaunganisha vizuri pasi kati ya wachezaji wa kati wa Spurs.
Pia inaonekana Pochettino ameamua kutumia mtindo wa 3-4-3 ambao kwa sasa unatumiwa na Chelsea..
Hivyo anataka mabeki Vertonghen, Dier na Wimmer wawe nyuma.
Hivyo Walker na Rose watakuwa wakipanda na kushuka, huku Dembele akiwa kwenye nafasi ya namba 10.
Dier na Wanyama watakuwa wapo katikati kuvizia mipira na wakipata wanamtupia Dembele ambae ni mzuri kwa mbio na ambae anaweza kufunga au kumpatia Harry Kane kumalizia.