Pesa yoyote kama si yako huwa huwa shida ya kuitumia.
Lakini kama inatokana na mpango wa biashara yako unalipa, basi huwa unakuwa mwangalifu na matumizi.
Ndiyo maana Arsenal wakamsajili Mesut Ozil kwa £42m, Alexis Sanchez kwa £35m na Xhaka kwa £35M
Arsenal wanao uwezo wa kutumia pesa waliyo nayo (waliyoitengeneza wao) kwenye akaunti lakini -responsibly.
now you are talking senses
Miongoni mwa timu zilizowekeza sana kununua wachezaji last season ni ManCity, Chelsea na ManU. hebu nikumbushe ziliishia wapi kwenye table mwisho wa msimu?
Mkuu hivi huyu beki yupo vizuri? Sijamfuatilia vizuri kabisa.Usajili Updates: Schkodran Mustafi asajiliwa na Arsenal.
Beki wa kimataifa wa Ujerumani na timu ya Valencia ya Spain Schkodran Mustafi amekubali kusajiliwa na klabu hiyo ya London na itatangazwa hivi karibuni.
Lakini Mustafi huenda asiwahi mechi ya Jumapili kati ya Arsenal na Liverpool.
Dau halisi la usajili huo linakadiriwa kuwa kiasi cha pauni za Uingereza milioni 30 yaani 20 za usajili halisi na 10 ni kama bonus na marupurupu mengine.
Wakala wa mchezaji huyo bwana Ali Bulut yupo busy kumhangaikia mteja wake na kumalizana na wawakilishi wa usajili wa Arsenal mjini Valencia nchini Hispania.
Mjue Mustafi.
Ana umri wa miaka 24
Ni mjerumani na amechezea timu ya taifa ya Germany mara 12 na kufunga goli 1.
Nafasi ya uchezaji - ni katikati au pembeni mbele ya mkoba.
Alishiriki kwenye kombe la dunia mwaka 2014
Timu ambazo amechezea ni pamoja na Everton (2009-12), Sampdoria (2012-14) na Valencia (2014-2016)
Mwezi June mwaka huu Mustafi alishiriki fainali za kombe la mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa na kufunga goli la kwanza kwa Ujerumani ilipocheza na Ukraine mjini Lille.
Karibu Arsenal Schkodran Mustafi.
COYGs
Naendelea kufuatilia hizi data kwenye corridors za harakati za usajili wa Arsenal, na kuzimwaga hapa.
Mkuu hii pia nimeikuta skysports nikafarijika zaidi kuwa yaweza kuwa na uhakika.What do you mean?
I always talk sense m8, because I believe in modern football management which goes well with good business model you create.
Pamoja na weakness ya Wenger kwenye kutoa pesa, nafkiri huu ukichaa wa bei za wachezaji sokoni inabidi udhibitiwe.Mpira umekua ni biashara..wachezaji wa kawaida wanauzwa bei ghali balaa.What do you mean?
I always talk sense m8, because I believe in modern football management which goes well with good business model you create.
Forget about Mahrez joining Arsenal, Nadhani Mustafi na Bony watakuja ingawaje Bony is not my choice, hiyo investment siikubali, afadhali waongeze dau kumpata Lewandowski kuliko kumchukua mtu atakayeonekana flop after three matches.
Pamoja na weakness ya Wenger kwenye kutoa pesa, nafkiri huu ukichaa wa bei za wachezaji sokoni inabidi udhibitiwe.Mpira umekua ni biashara..wachezaji wa kawaida wanauzwa bei ghali balaa.
Soko limebadilka na watu wako tayari kulipa zaidi ya uhalisia.Eti Crystal Palace nao wanataka £30M kwa Bolasie!
Mkuu hivi huyu beki yupo vizuri? Sijamfuatilia vizuri kabisa.
Hapa akimdhibiti Suarez.
Hapa akimdhibiti Neymar kwenye La Liga
Alifuatiliwa sana kwenye Euro 2016 na alicheza vizuri sana.
Ameimprove sana baada ya kwenda Valencia kutoka Samprodia.
Pale La Liga ni mmoja wa mabeki wa kati wazuri sana waliovuma msimu uliopita.
Ila yeye huwa hapendi sana kupanda mbele kama Bellerin na hata alipochezea Samprodia kule Serie A alionyesha uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo na kujiandaa kuudhibiti, na kwa hilo anampita alama Per Mertesacker.
Yaani huyu ni real deal na Arsenal wamepata mmoja wa mabeki mishahara wa maana, hivyo baada ya boss ni huyu jamaa halafu Rob Holding.
Huyu sio namba 2 au 3, ni central defender,unategemea apande mbele kutafuta nini? labda wakati wa kona na free kick karibu na goli la timu pinzani
Naona dalili za OZIL kuondoka mpaka sasa wenger hajampa mkataba mpya yani mzee huyu hasara tunayo
Mkuu richard una hisi ozil hafanyi jambo la maana kuusu ilo kwa faida ya timu