Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mkuu Wacha 1 na Kashengo mambo niaje?

Mzee anataka afanye usafi wakati wa summer na halafu asajili wachezaji wa maana kama watatu au wanne, akiwemo mkoba, kiungo na mshambuliaji.

Ni mkakati tu na ameweka mezani na bodi imeafiki.
 
aise kesho lazima arsenal ipigwe na ipigwe tu ndo furaha yetu

Na utafuraia sana mwaka huu na uendelee hivyo hivyo.

Kesho Arsenal watacheza wakiwa wametulia hata Chelsea wakija na hila za kila aina.

Tunamshukuru sana Fabregas, kazi aloifanya si ndogo.

Lol
 
Na utafuraia sana mwaka huu na uendelee hivyo hivyo.

Kesho Arsenal watacheza wakiwa wametulia hata Chelsea wakija na hila za kila aina.

Tunamshukuru sana Fabregas, kazi aloifanya si ndogo.

Lol
arsenal siku zote niwabovu kwa chelsea nakuhakikishia mtaliwa wabichi wabichi
 
Wakuu habari za mida.

Naona mambo yanakwenda sawia kabisa kutokana na matokeo ya leo.

Leicester wamerudi kileleni kweye msimamo wa ligi na West Ham wametufanyia kazi ndogo ya kuwarudisha nyuma Man City.

Hvyo basi Arsenal kesho haitakubali kupoteza nafasi ya pekee ya kurudi juu ya msimamo wa ligi hii.

Leo asubuhi vijana walijituma kufanya mazoezi laini na baadae wakenda kupata lunch.

Baadhi ni picha za vijana wakiwa na meneja wao Arsene Wenger kwenye uwanja wao wa mazoezi uliopo Colney jijini London.


Wenger akiongoza vijana.


Alexis Sanchez akiwa full fit.


Theo Walcott na Rambo wakiwa wamepata nafasi ya kubadilishana hili na lile/


Wakati mwingine Ozila huwa anakuwa very "funny".


Master and apprentice


Uhakika wa mlinda mlango Petr Cech.


Ox na Gabby

Ramsey akiwa anajaribu nguvu za kijana mpya Mo Elneny.


The Boss


Our marksman


Our attacker


Joel Campbell na Gabriel Paulista.


The mastermind akiangalia kila hatua.

Baadae ntashuka na timu inayotarajiwa kuingia dimbani.
 



Team news,

Arsenal kesho inacheza na Chelsea uwanja wa Emirates ikiwa ni mechi ya tatu msimu huu.

Mechi ya kwanza ilikuwa ni ile ya Community Shield ambapo Arsenal ilishinda kwa goli 1-0.

Mechi ya pili Chelsea walishinda kwao kwa goli 2-0. Katika mechio hii Gabriel alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya vituko vya Diego Costa na baadae Santi Cazorla nae katolewa kwa kadi ya pili ya njano.

Hivyo basi Arsenal kesho inatarajiwa kuonyesha kwamba imezonga mbele kimpira na wapo tayari kukabiliana na timu yoyote ile.

Ikumbukwe kwamba Arsena ina mechi karibu sita za ugenini dhidi ya Man Utd, Everton, Tottenham, West Ham na kukaribia mwisho wa ligi dhidi ya Man City.

Habari nzuri ni kwamba majeruhi wamerudi na Mesut Ozil na Alexis Sanchez watacheza kesho.

Mesut bila shaka ataanza mechi hiyo na Sanchez huenda akaanzia bench maana haitakuwa vema kuanza moja kwa moja kutokana na kuogopa kutonesha musuli.

Fransic Coquelin na Thomas Rosicky wamepona na wameanza mazoezi magumu, Danny Welbeck anaanza mazoezi wiki ijayo na Jack Wilshere anatarajiwa kuanza kucheza tena mwishoni mwa mwezi February.

Kiungo mpya Mohamed Elneny huenda nae akaanzia bench.

Hivyo basi timu inayotarajiwa kuingia uwanjani kupambana na the blues ni kama ifuatavyo:

Kipa Petr Cech, beki kulia Bellerin, kushoto nacho Monreal.

Mabeki wa kati ni Mertesacker na Boss.

Mlinzi wa kati ni Mathieu Flamini au Mohamed Elneny.

Kiungo wa kati ni Aaron Ramsey na mbele yake Mesut Ozil.

Washambuliaji wa pembeni kulia ni Joel Campbell na kushoto ni Theo Walcott.

Mshambuliaji ni Olivier Giroud.

Haya basi tukutane kesho jioni kabisa tayari kushuhudia miamba ikiumana.
 
EXCLUSIVE: Habari za usajili Arsenal waweka dau jipya mezani kwa Leicester la Ben Chilwell.

Arsenal usiku huu wameweka mezani kwa Leicester dau la kiasi kama cha paundi milioni 5 hivi kwa mchezaji Ben Chilwell ambae ni beki wa kushoto wa timu hiyo inayoshika usukani wa ligi hii kwa masaa 24 ana umri wa miaka 19.


Ben Chilwell mbele mwenye mpira alikuwa akitafutwa sana na Arsene Wenger.

Hii ni mara ya pili Arsenal wanajaribu tena baada ya Leicester kukataa paundi milioni 3 ambazo Arsenal walipendekeza.

Wenger anapendelea deal lifanyike wakati huu badala ya kungoja wakati wa summer ambapo timu za Liverpool na Man City nazo zinamzengea kijana huyu ambae pia ni mchezaji wa timu ya Uingereza ya vijana wenye umri chini ya miaka 21.

Arsenal wanataka kumsajili mchezaji huyu kwa sababu huenda wakampoteza Kieran Gibbs ambae anataka kuhama kutokana na kukosa nafasi ambayo imechukuliwa na Nacho Monreal ambae amecheza vizuri sana msimu huu.

Pia Leicester nao wanataka kumsajili beki wa Norwich Martin Olsson jambo linalomfanya Chilwell iwe rahisi kusajiliwa na Arsenal.

Arsenal walituma tena maskauti wake kwenda kumuangalia kijana huyu siku ya Jumatano Leicester ilipocheza na Tottenham kwenye mechi ya kombe la FA na kuzidi kupendezwa nae hasa mtindo wake wa kuweza kufanya mashambulizi na kurudi nyuma haraka.
 
Wakuu, habari za mida naona mida ndio yazidi kujongea.



Team news:

Zinakuja....

Ila mwamuzi wa mchezo huu anaitwa Mark Clattenburg ambae anaishi Newcastle.

Kwa mara ingine tena Mike Dean kawekwa pembeni.
 
Leo Tunaanza Hivi Wadau 4-2-3-1
1.Czech
2.Bellerin
3.Nacho
4.Koscienly
5.Metersacker
6.Ramsey
7.Flamini
8.Ozil
9.Giroud
10.Campel
11.Sanchez
 
Leo Tunaanza Hivi Wadau 4-2-3-1
1.Czech
2.Bellerin
3.Nacho
4.Koscienly
5.Metersacker
6.Ramsey
7.Flamini
8.Ozil
9.Giroud
10.Campel
11.Sanchez

Sema unatabiri timu mkuu, ila sio mbaya inaweza kuwa ni sawa.

Tusubiri official team news, ni kama baada ya saa moja hivi.
 
Timu zinaingia uwanjani

Arsenal:
Cech, Bellerin, Mertesacker (c), Koscielny, Monreal, Flamini, Ramsey, Campbell, Ozil, Walcott, Giroud

Akiba: Ospina, Gibbs, Chambers, Gabriel, Elneny, Oxlade-Chamberlain, Alexis

Chelsea:
Courtois; Ivanovic, Zouma, Terry, Azpilicueta; Mikel, Matic; Willian, Fabregas, Oscar; Costa

Bench: Begovic, Cahill, Baba Rahman, Loftus-Cheek, Traore, Hazard, Remy
 
Arsenal kama kawaida wamevalia jezi nyekundu na chini ni kaputura nyeupe na soksi nyeupe pia.

Chelsea wao wana jezi na kaputura na soksi za rangi ya blue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…