Sio kuwabeza, ila ukweli lazima usemwe! Weak link leo ni mabeki wa kati Na Flamini wamechangia goli tatu za kizembe, na hasa Per! Sio kubeza, ni kusema ukweli! Point 36 tunazo na tuko juu ila sababu mojawapo ni kwamba timu kubwa kama chelsea na mancity hazifanyi vizuri mpaka sasa, kwao si kawaida ndo maana kwa siso tuko juu!
Tuendelee kuomba wasifanye vizuri ili tuchukue ndoo, ila msimu ujao bahati haitakuka upande wetu maana chelsea watarudi!
Nina hofu pia na Tottenham, wanakimbiza mwizi kimya kimya na hatujaenda kwao!
Ila Bournemouth sio wa kuwabeza si uliona Chelsea walifungwa kwao?
Soton 0-4 Arsenal
Mmm nina walakini na kuutazama mpira au kipigo kimekuchanganya mbaya
vipi kuhusu Nacho? ambae so far ni best left back pale EPL, Bellerin? unazungumziaje Peter Cech
Unasema nin kuhusu Kos? Santi? Coqeulin
Isiwe kikitokea kipigo tu mnadharau timu yenu yoote so far point 36 wamepata hawa hawa wachezaji..unaowatukana na kuwabeza
walioshusha wachezaji wa bei mbaya kama Manure wako wapi?an city ana Defeats 5 so far kwenye EPL
kubali tu ligi ni ngumu hii ni imekuwa haitabiriki kbs
Seriously WATU NA MANENO YAO
Eti Arsenal wana tatizo la kufika kileleni Wamuone
DR Mwaka
Nimekula, wameniudhi sana! Unajua unaweza fungwa ila bado ukaikubali timu sababu ya kuonyesha kupigana mpaka jasho la mwisho, ila sio leo!
Nimepewa za uso NNE hapa uso umeumika sioni vizuri.
Kwa Arsenal hii ni lazima kuwaombea njaa maadui hasa Mancity, kwa miguu yetu pekee sisi The Gunners ni ngumu sana, hamna fighting spirit. LAZIMA TUSEME UKWELI, unafiki sio mzuri!
Nawe naona europa nayo inataka kukukimbia!