Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

_85589578_hero_oezil_getty.jpg

10 men Gunners go down fighting .... ... .... Ding ... .... ... Dong
2-1
 
Game over na Arsenal wameanza vibaya kombe la mabingwa wa Ulaya.

Arsene Wenger ameidharau hii timu na kupelekea kufungwa, wapenzi wa Arsenal tuwe wakweli kwenye hili.
 
Dynamo Zagreb ndio gemu yao ya kwanza kushinda kwenye champions league ngazi ya makundi.Hawajawahi kuishinda timu yeyote ile kwenye makundi tokea waanze kushiriki kwenye ligi hiyo.
 
Game over na Arsenal wameanza vibaya kombe la mabingwa wa Ulaya.

Arsene Wenger ameidharau hii timu na kupelekea kufungwa, wapenzi wa Arsenal tuwe wakweli kwenye hili.

Ukweli mwingine usio na chembe ya unafiki nikiwa Shabiki makini na mzoefu

season hii naona mzee kaidhamiria EPL huku UCL ni kutafuta pesa...No priority after all naonaga kashakataga nayo tamaa
 
Hii ndo Europe, hatuna rekodi nzuri!
Ila kiukweli Debutchy, Arteta, Gibbs sio material ya Uefa.
 
Game over na Arsenal wameanza vibaya kombe la mabingwa wa Ulaya.

Arsene Wenger ameidharau hii timu na kupelekea kufungwa, wapenzi wa Arsenal tuwe wakweli kwenye hili.

Kufungwa ni Kufungwa. Hamna cha dharau wala nini. Wenger alijaribu kushinda lakini mpira ndio hivyo. Alifanya sub 3 ili kubadili matokeo lakini haikuwa. Kudai dharau ni denial na kujaribu kuficha ukweli kwamba mpira unadunda na una matokeo matatu kushinda,kushindwa na kutoka sare.
 
Mkuu Kashengo, kama priority ni EPL basi angeanza na timu ngumu, yaani nyuma Hector Berelin, Nacho Monreal na Mertesacker wangeanza kule nyuma.

Pale katikati Coquelin , Ramsey na Walcott wangeanza kule mbele na Arsenal wangeifunga Dinamo Zagreb au kutoa sare ya 1-1 au 0-0.

Mikael Arteta, Mathieu Debuchy, Gabriel Paulista na Giroud wpote wangeingia kipindi cha pili na wale watakaoanza Jumamosi na Chelsea wangepumzishwa.

Si umeona Coquelin na Walcott wamekuja kipindi cha pili na wamerudisha heshima ilopotezwa na Arteta na Debuchy?

Ni planning tu na si vinginevyo.

Bila hayo bado Arsene Wenger alitakiwa asajili DM na Striker mwingine na ndio ambao wangeanza kucheza leo.
 
Kufungwa ni Kufungwa. Hamna cha dharau wala nini. Wenger alijaribu kushinda lakini mpira ndio hivyo. Alifanya sub 3 ili kubadili matokeo lakini haikuwa. Kudai dharau ni denial na kujaribu kuficha ukweli kwamba mpira unadunda na una matokeo matatu kushinda,kushindwa na kutoka sare.

Ni dharau bana!

Angechezesha timu iloshinda mechi za EPL Arsenal ingeshinda leo.
 
Nakuunga mkono, tumefungwa kihalali kabisa na tungeweza fungwa hata nne. Hongera zao Dainamo Zagreb! Tujipange na Chelsea ambao watakuwa psyched up kwa mechi ijayo darajani.
 
Ni dharau bana!

Angechezesha timu iloshinda mechi za EPL Arsenal ingeshinda leo.

Sio dharau, isipokuwa hayo ndo matokeo ya kuwa na kikosi chembamba, wenger ana timu moja tu kikosi cha kwanza na hana hata backup nzuri za hiyo first eleven, leo kachezesha wacheZaji huku jicho lake likiwapo mechi na chelsea.
 
Sio timu hiyo unayoisema ndio ilibamizwa na West Ham au pia ilikuwa dharau?Tuweni wakweli mpira unadunda.

Ndio maana nikasema mechi ilizoshinda bila kuanza na Giroud na pia bila kuanza na Mathieu Debuchy ambae kwenye mechi na West Ham alikuwa uchochoro na leo pia magoli yote mawili yamepitia kwake.

Wewe utaona Arsenal jumamosi ikija na full force tunataka tusiwe mbali sana na Man City by Monday.
 
Back
Top Bottom