Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Wakuu mpo?

Mimi nimejitahidi kukaa hapa kutokea St James Park

Arsenal Mesut Ozil nje na Walcott, Chamberlain ndani wanaanza.
 
Hii mechi arsenal inabidi ile tano mtungi ili wenger asajili kuongeza nguvu au nane kabisa kama za UTD kipindi kile
 
KADI NYEKUNDU

Mitrovic anamkany'aga Coquelin na mwamuzi MArriner hana jinsi ni kumtoa Mitrovic.

Dakika inaenda ni ya 18
red-card_3423170b.jpg

Alexander Mitrovic akionyeshwa kadi na mwamuzi Andre Marriner.
 
Dakika 30 zinaenda Arsenal bado hawajafunga goli na wancheza na watu 10
krul_3423165b.jpg


Walcott alikosa goli ls wazi mapema na kipa wa Newcastle akaokoa.
 
Mapumziko Newcastle 0 Arsenal 0Arsenal wameshindwa kufunga goli hata moja.

Newcastle wanacheza mtindo wao uleule wa watu kumi nyuma ya mpira na mtindo huo una faida kwao kuliko Arsenal.
Huenda Olivier Giroud akaingia ili awe nashughulikia mipira ya juu.
 
Dakika ya 71 Newcastle nao wanafanya mabadiliko na Vurnon Anita anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Ayoze Perez.

Zimebakia dakika 18 na za nyongeza mpira uishe.
 
Dakika ya 77 Steve Mac-Claren anafanya mabadiliko mengine Sissoko anatoka na Papis Cisse anaingia.

Newcastle wanatafuta goli la kusawazisha na Arsenal lazima wamalize huu mchezo kwa kufunga goli la ushindi kamili.
 
Dakika ya 80 Mikael Arteta anaingia kuchukua nafasi ya Alex Oxlade Chamberlain.
 
Newcastle wanafanya mabadiliko ya mwisho na Siem De Jong anaingia kuchukua nafasi ya Florian Thauvin.
 
Theo Walcott sio striker!
TANESCO pia wameniboaa balaa mpaka kura yangu wameikosa hivi hivi. Nimelipa buku kibanda umiza, nisu saa tu wameshakata umeme!! WAMENIUDHI sana.
 
Back
Top Bottom