Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kumbe humu ni kwa washabiki wa Goons tu?!? 😳😂😳😂

Utakuwa mgeni weye!

..unajua tulipoanzia au unadandia tu,vyema ukasoma kwnz hizo post za juu uelewe sio unakurupuka tu.Mi hapa naizungumzia arsenal nayoishabikia huyo mwenzio ameifata arsenal huku asiyoishabikia,ndio tofauti ndogo iliyopo.
 
..timu yenu imeonekana kidogo na kaunafuu baada ya kupewa hao wabelgiji,mpk vipofu wamefunga hat trick ngoja mrudi kwa wanao jua.!!
Nakuunga mkono, "new ronaldo" kwenye EPL hamna kitu, na timu ya pub ya belgium kang"ara balaa, jana ilikuwa kwa yule striker butu!
 
Champions League Draw:

Inafanyika saaza Ulaya 11.45 jioni.

Kuna timu 32 katika makundi manne na kila timu itachaguliwa na timu zingine tatu kufanya kundi lenye timu nne.

Pot 1: Barcelona, Chelsea, Bayern München, Juventus, Benfica, Paris, Zenit, PSV Eindhoven

Pot 2: Real Madrid, Atlético, Porto, Arsenal, Manchester United, Valencia, Bayer Leverkusen, Manchester City

Pot 3: Shakhtar Donetsk, Sevilla, Lyon, Dynamo Kiev, Olympiacos, CSKA Moscow, Galatasaray, Roma

Pot 4: BATE Borisov, Borussia Mönchengladbach, Wolfsburg, Dynamo Zagreb, Maccabi Tel-Aviv, Gent, Malmö, Astana

Je ni timu zipi zinaweza kupangwa na Arsenal?

Arsenal wanaweza kupangwa kundi moja na timu za Barcelona, Bayern Munich, Juventus, Benfica, Paris-Saint Germain, Zenit St Petersburg au PSV.

Na kwa kuwa Arsenal wapo kwenye kundi la pili basi hawawezi kupangwa kundi moja na timu za Real Madrid, Atletico Madrid au FC Porto.

Timu yoyote mpya?

Ndio, kuna timu iitwayo Gent ambao ni mabingwa wa Belgium amba ni mabingwa kwa mara ya kwanza nchini humo na pia wanashiriki cl kwa mara ya kwanza.

Pia kuna timu ya Astana kutoka nchini Kazakhstan ambayo nayo ni mara ya kwanza kucheza CL. Timu yoyote itakayokwenda kucheza nchni Kazakhstan itasafiri kwa ndege Zaidi ya masaa tisa kutokea barani Ulaya.

Lini mechi zitachezwa?

Mechi za kwanza: 15/16 September

Mechi za pili: 29/30 September

Mechi za tatu: 20/21 October

Mechi za nne: 3/4 November

Mechi za tano: 24/25 November

Mechi za sita: 8/9 December

Haya basi tujiandae na hio draw baada ya masaa mawili hivi.
 
Nakuunga mkono, "new ronaldo" kwenye EPL hamna kitu, na timu ya pub ya belgium kang"ara balaa, jana ilikuwa kwa yule striker butu!

..hako katoto kao kakifikisha goli 15 msimu huu kwangu nitakahesabu kanajua,kana mbwembwe nyingii end product zero!
 
tuna point 7 za kwenye ligi au nayo ligi ni ya ubelgiji?
hao wabelgiji walifika robo fainali ya Europe league, vp livapuli na Everton wanaocheza ligi ngumu walifika wapi?

Point7 magoli2 kati yahayo moja la kujifunga safi sana.
 
Haya sasa mtanange ndio umetayarishwa na Arsenal imepangwa kwenye kundi F. Timu zingine kwenye kudi hilo ni pamoja na Olympiakos, Dinamo Zagreb na mahasimu wao Bayern Munich.
 
bayern nimeshawazoea,nawaona km hawapo vizuri sn kwenye champions league kulinganisha na ligi yao ya nyumba.Kushinda emirates is possible and even draw away at allianz arena is possible again,hizo timu nyingine tushindwe wenyewe,inshort last 16 tumeshafika.Issue kuanzia hapo kwenda mbele, Je, Wenga ataongeza striker,holding midfielder..?anyway let's wait and see.
 
Ya huyu mzee sijui vipi we pesa za usajili unapewa watu wa kusajili wapo mpaka wengine wanachukua lakini ye yupo tu kama anaganzi yani aaargh mzee sajiliii unazingua mpaka inaboa kuzungumzia CL inaonekana wazi kazi tunayo
 
..kuvuka hilo kundi sio issue tutavuka,last 16 km kawa ndio tutaanza kutafutana au Mungu asaidie tuje pata timu km monaco last season japo nao walitutoa.!!
 
..kuvuka hilo kundi sio issue tutavuka,last 16 km kawa ndio tutaanza kutafutana au Mungu asaidie tuje pata timu km monaco last season japo nao walitutoa.!!

Kaka at first place tutaangukia pua kwa forward yupi kiungo mkabaji yupi beki ZIPI we Acha tu
 
bayern nimeshawazoea,nawaona km hawapo vizuri sn kwenye champions league kulinganisha na ligi yao ya nyumba.Kushinda emirates is possible and even draw away at allianz arena is possible again,hizo timu nyingine tushindwe wenyewe,inshort last 16 tumeshafika.Issue kuanzia hapo kwenda mbele, Je, Wenga ataongeza striker,holding midfielder..?anyway let's wait and see.

Umewazoea vipi timu iliyowapeleka nje 16 bora mara 2 mfululizo.??
 
Haya sasa mtanange ndio umetayarishwa na Arsenal imepangwa kwenye kundi F. Timu zingine kwenye kudi hilo ni pamoja na Olympiakos, Dinamo Zagreb na mahasimu wao Bayern Munich.
Mteremko, sioni wa kutisha kivile. Fair draw!
 
Arsenal kama kawa ata mkukuruke vipi nafasi ya 2 mkicheza ya 3 itawahusu pia, na mwaka huu mkipita tena kama no. 2 kwenye group stages Barcelona, Real Madrid, Psg, m1 wapo atawahusu, naomba niwatakie mkono wa kwaheri mapema wazee wa 16 bora..
 
Itabidi Arsenal tuwanunue Bayern Munich sababu tunapangiwa na hawa wadudu karibia kila msimu. Utadhani UEFA wana kisirani fulani na sisi. Anyway, msimu huu itabidi tuwafanyie kubwa tuwapige ubaya kwao na kwetu, tumfukuzishe kazi Guardiola.
 
I am always confident that a last-minute situation or solution is available, because the transfer market is especially moving in the last four or five days.
Asked if he was confident of making any more new signings, he said: "At the moment, I cannot say I am very confident because we are not close to signing anybody.

"I don't know because I am always confident that a last-minute situation or solution is available, because the transfer market is especially moving in the last four or five days.

"At the moment, I cannot promise you that. We work very hard... you know I have a team around me who work day and night to find good solutions.

Hapa ndio namuonaga mzee m******e
 
Umewazoea vipi timu iliyowapeleka nje 16 bora mara 2 mfululizo.??

..narudia tena bayern wanapigika,Wenger tu apange wachezaji kwa nafasi zao,aachane na habari za winger ramsey af kina ox na walcott bench..
 
Back
Top Bottom