Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kutereza si kuanguka. Tutarudi tunapostahili muda si mrefu na kulibeba kombe. Makosa yatasahihiswa kesho. Muda wenu kucheka na kufurahia kutereza kwa tembo...

everlenk, Belo, Bavaria, Nzi, mentor and compay.

ngapi ngapi?
 
Kutereza si kuanguka. Tutarudi tunapostahili muda si mrefu na kulibeba kombe. Makosa yatasahihiswa kesho. Muda wenu kucheka na kufurahia kutereza kwa tembo...

everlenk, Belo, Bavaria, Nzi, mentor and compay.
Mna tatizo la kipa leteni hela tunao wengi tunauza Valdes,De Gea,Lindergard muwahi kabla wenzenu hawajachukua
 
Timu inaposhinda hatuna budi kuipongeza.

Hakuna kitu nilichovutiwa leo kama uchezaji wa huyu mtoto aitwae Reece Oxford.

Leo alimweka mfukoni Mesul Ozil ambae aliigharimu Arsenal paundi milioni 42


Reece Oxford akimkabili Ozil


Reece Oxford ana umri wa miaka 16
 
What if asiposajili?
Utazisikia hizi mtu ambazo zina "Matumaini" zikiimba "Wenger out, wenger oouutt!!"

Ukweli Wenger alikuwa na wachezaji wa kushinda hii mechi ya leo lakini baadhi ya wachezaji hao amewaingiza baadae wakiwa wameshanyolewa 2-0.

Upangaji wa Timu ndio umeumiza moyo wa Rubaman na Juwaine leo.

All credit to West Ham, walifika pale wakiwa na nia ya kushinda au kutoa upinzani wa kiwango cha juu.

BAK unahitajika kufika huku ili uzie hizi "kcuf" zinazotoka midomoni mwa mashabiki wenye hasira, waliokuwa wakinywa bia baridi huku wanaangalia "mabingwa" watarajiwa wakifanya mambo yao.
 
Reactions: Nzi
aisee inauma sana umebakwa, umetolewa bikra, umepigwa goli mbili, umepewa mimba na umeambukizwa ukimwi ............
 

Naomba nikumbushe jina la yule dogo alievaa jezi namba 8.
 
Reactions: Nzi
Oxford ameonyesha kiwango cha juu, tatizo ni muingereza, watampamba mpaka ataharibika kabla hajagonga 20!
 
Kweli Tumewaona mabingwa wa msimu mmeanza ligi kwa ushindi wa kishindo

Mabingwa mtatuona tukianza kutoa dozi baada ya dozi. Leo jamaa walituotea tukiwa choo cha makuti Mwananyamala kisiwani.
 
Reactions: Nzi
Naomba nikumbushe jina la yule dogo alievaa jezi namba 8.

Yule kiungo mshambuliaji (attacking midfielder) anaitwa Cheikhou Kouyate ndie aliefunga goli la kwanza.

Ni mmoja wa viungo wa timu ya taifa ya Senegal.
 
Reactions: Nzi
aisee inauma sana umebakwa, umetolewa bikra, umepigwa goli mbili, umepewa mimba na umeambukizwa ukimwi ............

bila kusahau nyumbani kwako na kwenye kitanda chako!
ila maisha yanaendelea, Arv zipo na inasemekana mtoto akiwa mkubwa atakuwa rais wa nchi.
 
Ehehehehehehehe rubaman kwema hapa ndugu yangu ehehehehehehehe

Jamani mmemtoa bure yule Mpoland wenu kwa kikongwe huyu ehehehehehehe poleni sana!Kumbukeni tarehe 24 MAJOGOO yanakuja kukuchapa hapo hapo kwako

Nasubiri nione Stoke City watakavyowafanya na nyie. Kipa wetu alikuwa nervous lakini atajirudi mechi ijayo. Mpolish alikuwa wa mtu wa SELFIE'S tusubiri tuone atakavyofanya Italy.
 
Kufungwa leo nadhani kuna mkono wa Mourinho na Roman Abromovich inawezekana wametuma Cech kutuvuruga lol.
 
Mabingwa mtatuona tukianza kutoa dozi baada ya dozi. Leo jamaa walituotea tukiwa choo cha makuti Mwananyamala kisiwani.

bado mapema mno, imeniuma kuwa tumefungwa nyumbani tu, ila ndo kwanza marathoni imeanza kisha watu wameanza na spidi ya usain bolt.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…