Transfer Updates
Wakuu, naona mambo yapo kwenye hatua ya muhimu sana kwa sasa kwenye usajili.
Hadi sasa Real Madrid wanagoma kumtoa Karim Benzema mpaka watakapopata mchezaji mbadala wake.
Borrusia Dortmund nao wanagoma kumtoa Pierre- Emerick Aubameyang kwa sababu hiohio kwamba itakuwa ngumu kumpata mshambuliaji mwingine mahiri.
Hata hivyo kwa sisi wapenzi wa Arsenal tayari tumemgundua mchezaji ambae jana mzee Lord Harris alisita kumtaja kwamba yumo kwenye orodha ya Arsene Wenger kwamba ni mbadala wa Karim Benzema ikiwa dili litashindwa kukamilika.
Sasa ukiangalia opitons zote za Arsenal kwenye dirisha la usajili wa washambuliaji, ukiondoa sehemu ya kiungo ambayo Mathieu Flamini ameondoka hivyo kuhitajika kiungo mwingine, kuna washambuliaji wafuatao ambapo mmoja wao ndie atakesajiliwa na Arsenal kabla ya dirisha kufungwa rasmi hapo tarehe 31 August 2015.
1. Karim Benzema
Huyu ndie chaguo la kwanza la Arsene Wenger na Arsenal wameweka mezani paundi milioni 31 ambazo raisi wa timu hiyo Florentino Perez bado anakuna kichwa kumwachia Benzema.
Benzema ni mshambuliaji alikamilika (complete striker) na ni mmaliziaji mzuri. na miaka 27 na ni raia wa France. Thamani yake kwa upande wa Real Madrid ni paundi milioni 35.
2. Robert Lewandowsky

Huyu ni mbadala wa Benzema ikiwa dili la Benzema litashindwa ambae ndie jina lake limekuwa likifichwa lakini limegundulika. Lewandowsky ana umri wa miaka 27 na ni raia wa Poland, kwa sasa ni mshambuliaji wa Bayern Munich ya Germany na pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Poland. Mchezaji huyu anagharimu kiasi cha paundi milioni 37.
3. Pierre -Emerick Aubameyang
Huyu Arsenal wameweka mezani paundi milioni 30 na Dortmund wamekataa. Aubameyang ana umri wa miaka 26 na ni pia mshambuliaji wa timu ya taifa ya Gabon. Aubameyang ana mbio na takwimu zinaonesha anakimbia kwa kasi ya mita 30 kwa kutumia sekunde 3.7 Aubameyanga ana uwezo wa kucheza nafasi ya ushambuliaji wa kati au pembeni.
4.Fernando Llorente
Huyu Arsenal wameuliza kwa Juventus ikiwa yupo available na Juve wanaweza kumwachia aende Arsenal hasa baada ya kumsajili Mario Mandzukic kutoka Athletico Madrid. Hata hivyo bado Arsenal hawajarudi kuweka "offer" mezani. Llorente anagharimu kama paundi milioni 9 hivi.
Hivyo basi tunasubiri kuona Arsene Wenger akikamilisha usajili wa wachezaji wawili muhimu kwenye nafasi za kiungo na ushambuliaji msimu huu.