Usajili so far.
Suala la Karim Benzema.
Real Madrid wamekataa paundi milioni 32 ambazo Arsenal waliweka mezani na kudai kwamba mchezaji huyo bado ni muhimu kwa timu hiyo.
Kwa kuangalia namna Raphael Benitez alivyopanga timu hiyo hasa kwenye mechi ya kwanza ya majaribio Jumamosi ilopita, na Roma ya Italy, Cristiano Ronaldo ndie anapangwa kama central striker akiachwa mbele, hivyo kupunguza uwezekano wa Benzema kuanza mechi nyingi na kuwa anakaa bench.
Pia Benzema ni mmoja wa wachezaji wanaopendwa sana na raisi wa timu hiyo Firentino Perez hivyo kupunguza uwezekano wa kukubali mchezaji huyo aondoke bila kupata mchezaji mwingine wa calibre yake hasa kama Sergio Aguero wa Man City.
Lakini baada ya mchezaji mwenyewe kushindwa kukanusha habari za usajili wa Arsenal bado Raphael Benitez anataka apatikane mchezaji mwingine wa kuziba nafasi yake endapo Benzema atakwenda Arsenal.
Nacho Monreal.
Nacho bado ana tatizo la kuangalia mikono yake pale anapokabiliana na wachezaji wengi wa pembeni wa timu pinzani hii inaitwa kwa kiingereza handbal rule.
Handbal Rule
Hii "handbal" rule ni pale unapokuwa ukimwangalia mchezaji wa pembeni au mshambuliaji pale anapokuwa akifuatilia mpira wa kona au wa kupigwa juu kuekekea eneo la hatari la goli lako.
Hivyo unapokuwa unageuka unapaswa kuangalia mikono yako na kuhakikisha haigusi mpira.
Bado Nacho anafanya mafunzo ya handbal rule lakini Athletico Bilbao wanataka kumsajili beki huyu na Arsenal na endapo Nacho ataondoka, tayari wamepata mchezaji beki mwingine ambae anaitwa Sead Kolasniac na anachezea timu ya Schalke ya Germany.