Misimu Ya Arsenal Kuchukua Premier League
Inakaribia .. I can Feel it Kama sio Msimu unaokuja basi msimu utakao fatia tena ... We are almost there ...Am sure arsene Wenger
Atachukua Premier League Tena Kabla Hajastaafu ...
Kitu ambacho Nina wasiwasi nacho sidhani kama ataweza kuchukua champions league ..
Naiona arsenal ikifanikiwa kwenye champions league
kuanzia miaka mitano na kuendelea, kutokea sasa .. Sidhani kama atakua bado manager ....
Jinsi Arsenal Tulivyokosa Premier league msimu
uliopita na msimu huu its like Mtu anaejifunza kufanya something hawezi akaenda exactly straight kufanya vizur lazima ataanza na vibaya then Ata master kadri ya muda unavyosogea ..
So far Arsene Wenger Ametengeneza kikosi cha
kuchallange premier league kilichobaki ni kuwaweka fit tu wachezaji .. Msimu uliopita tulikua tupo kwenye crisis za injury sana na hiyo
ikaharibu msimu wetu kwenye mzunguko wa pili
wachezaji key players waliumia kijinga tu na
ilikua tabu sana kupona, setback za majeruhi zilikua nyingi mno ...
Shad Foshye Yule Fitiness coach tuliemtoa team
ya taifa ya ujerumani somehow ametusaidia
msimu huu na am sure tukimpa muda zaidi
ataifanya team iwe strong .. Majeruhi ya msimu
huu yalitokana na wachezaji kupush sana kuiweka team kwenye level kubwa wakati miili Yao haikua tayari kumbuka wachezaji wetu wengi walikuwepo kwenye world cup mpaka kwenye
hatua za robo fainali walikua bado wapo wengi
wengi tu hawajatolewa ...
Shad Forshye yule
coach alichofanya alitusaidia hawa wachezaji wengi wao wakawa wanapona mapema kabla ya
muda wao kufika hadi kufikia January wachezaji
wengi wakawa wamerudi .. Mchezaji aliepata
setback kwenye injury yake msimu huu alikua ni
arteta tu ila wengine wote walipona kabla ya
muda wao wengine walipona kwenye muda halisi waliowekewa ....
Hadi kufikia sasa majeruhi ambae anahesabika
majeruhi kwenye senior team ni chamberlain tu
ambae hatakaa nje mda mrefu ... Me naona haya
ni maendeleo kwangu, kwakua msimu ulipita
ilikuahali mbaya sana
Ni kwanini naona arsenal itachallenge premier
league msimu ujao ni kwakua naona karibia
matatizo sugu yanaanza kutibika .....
Arsenal Defensive Midfielder Wetu Wa mwisho
Kutupigia kazi vizur alikua Gilberto Silva tangu
yeye aondoke ile nafasi tulikua tunaiziba kiuongo
uongo tu ... Kuna msimu ambao Flamini alijaribu
kuonesha uwezo wake ila hakuweza kuweka
alama yake kwakua aliondoka mwishoni mwa huo msimu ...
Watu mtasema Alex Song Alifanya vizur ila
mbona Arsenal Haikua vizur wakati yeye yupo
kwenye form .. Jibu langu hapa ni rahisi tu ..
Alex song wakati yupo arsenal hakua defensive
midfielder bora alikua ni midfielder bora, alikua
Ana take risk sana ya kusogea mbele sometime
alikua anatucost sana na sometimes Mikel arteta
alikua Ana mzibia makosa yake ndio maana hata
sikushangaa Wenger alivyoamua kumrudisha
arteta namba sita baada ya song kusepa ..
Kiujumla Alex song alikua bonge la player kwetu
pass zake zilikua na akili mno ila hakua typical
defensive midfielder tuliemuhitaji alikua Ana act
kama box 2 box sometime yaan ilifika kipindi
alikua anafanya kazi ya namba nane wake na
kumlazimu huyo namba wake ambae arteta kuja
kufanya kazi ya namba sita
Fransicis coquelin itamchukua misimu hata
mitatu au minne kufikisha assist 14 za Alex song
aliizotoa ndani ya msimu mmoja ... ila huyu
Coquelini Inamchukua mechi chache sana
kufanya tackling na interseption nyingi kuliko
song kwa msimu mzima ..
Huyu ni typical
defensive midfielder tuliokua tuna muhitaji ...
Tulihitaji someone ambae atakua Ana wafanyia
wenzake kazi na wenzake wawe wanaenjoy
matunda yake ....
Uzuri wa coquelin anaongeza mkataba kwaiyo
wakati wa peak yake ya career yake anaweza
kua arsenal akiwa kama key player tofauti na
flamini alietukimbia wakati wa ubora wake
amerudi akiwa ameshakua gari la mkaa..
Arsene Wenger kwa ndoto zake za kujaribu
kushinda champions league kabla hajastaafu
itazidi kutusaidia kuimarisha kikosi chetu kwa
haraka kwa nyakati hizi ambazo hatuna matatizo
ya kifedha natumaini atatuletea superstar
mwingine mwishoni mwa msimu ...
Nataka afanye usajili wa maana hatuhitaji big
name ili mradi big name alafu aje kuishia kukaa
benchi ili team ibalance, sisis tunahitaji someone
ambae kweli ataongeza kitu kwenye team yetu ..
Ni kama Mesut Ozil alivyokuja kuongeza kitu
kwenye team yetu .. Unajua kazi ya ozil watu
wengi hawaijui na kwakua waingereza wengi joking
wanao mponda wameshazoea kuona michezaji
Yao ikicheza kwa speed na nguvu hata kama
finals ball zao ni very poor hua hawajari sana
ilimradi wameona mchezaji huyo ame tackle kwa
nguvu au ame dribble kibae ...
Mesut ozil kitu anacho leta arsenal sio kupiga
watu vyenga kama ronaldinho kama waingereza
wengi wanavyotaka ozil afanye ... Huyu ozil
alicholeta kwentu ni kama tuseme uweke grisi
kwenye machine ili uweze kuilainisha mtambo
ndio anachofanya ozil ..
Hiyo kazi cesc fabregas alikua anatufanyia vizur
sana na alipondoka tukakosa mtu mwingine wa
kufanya hiyo kazi ..
Ni kwanini nafananisha kazi
zao ni sawa na grissi kwennye machine kwakua
ni hivi hawa jamaa mara nyingi hua wana make
sure mpira hua Una flow kwenye final third no
matter what .. Mfano goli la bellerin dhidi ya
Liverpool ile assist ya goli alitoa Ramsey, huyu
Ramsey alipokea mpira mzuri sana kutoka kwa
ozil aliekua kwenye upande mwingine kabisa wa
uwanja ..
Ozil alipiga pass akiwa kwenye half ya
arsenal upande wa kushoto akupeleka mpira
kwenye half ya Liverpool upande wa kulia Range
pass ilioenda diagonal .. Kwa huku uswahili
kwetu tunaita amehamisha uwanja yaani
unapotoa mpira kutoka kwenye tight area eneo
lilomabwa na wapinzani na kupeleka kwenye
upande mwingine empty area ambapo Kuna
mchezaji wa timu yako anasubiria ..
Hapa duniani wataalamu wa kuhamisha uwanja
ninao wajua ni ton kross, xavi, pirlo , fabregas na
Paul scholes labda na Michael carick .. Na hawa
wote ukiwaangalia ni central midfielders sio
number tens so ozil aki kwenye position tofauti
na number ten still hua anaelewa acheze vipi ..
Mwanzoni mwa msimu me pia nilikua Nina amini
ozil anapotea anapocheza wing ila that guy Ana
akili sana popote utakapo muweka still atapiga tu
one pass itakayo make the difference kipindi kile
cha mwanzo wa msimu nahisi hakua kwenye
maandalizi ya kutosha baada ya world cup na sio
kwakua alikua anacheza vibaya kwakua ni winger
...
Ukingalia idadi ya pass anazopeleka kwenye
final third na jinsi anavyo pangilia mashambulizi
yake akiwa na mpira au bila mpira utaelewa ni
kaisi gani Ana akili sana ozil
Na Star Wetu mwingine aliekuja kuongeza kitu
AlexiaSanchez anatupatia kitu ambachotulikua
tunakosa sana kwenye final third ..baada ya ozil
ku crack defensive line na kutengeneza nafasi
tulikua tunafunga perfect goals tu hatukua na
mtu ambae ni "cha ubishi" ambae atang'aninia
kutaka kuattempt kufunga hata kamanafasi
ngumu .. Kitu ambacho sanchezi amekuja
kufanya kazi yake vizur sana ..
Ukiangalia magoli mengi ya Giroud ni perfect
goals kwa central foward touch zake mbili au
moja anatupia sio mtu wa kuzama mabeki na
kulazimisha hadi afunge hapa sanchezi ndio kaja
kuleta utofauti na giroud na kumsaidia hata
giroud kupunguza pressure ya kufunga na yeye
nae anacheza mpira akiwa na confidence.. Na
hivyo Ina msaidia kumaster style yake
anayoimudu vizuri
Kama manager akituletea World class mwingine
atakae ongeza something kwenye team yetu I
think tutakua tayari kuchallange premier league
kwakua mpaka sasa tupo tayari ila tu tunatafuta
jinsi ya kubalance msimu wetu kushinda FA Cup
last season ilisaidia kidogo kushusha pressure
ilikuwepo awali ya kua team kubwa alafu hamna
taji ...
Kwa jinsi ninavyoona champions league ilivyo
kwa sasa ni tofauti na zamani hii ya sasa
inakulazimu ataleast uwe ume Shinda makombe
ya ndani ndio utwaweza kumudu kuchallange lile
dude ... Kwakua mabingwa wa lile kombe kwa
miaka 10 ya hivi karibuni wanakua
wameshachukua makombe ya kwao hasa la ligi
From there ndio wana push kwa champions
league glory ... Kwa arsenal naona bado sana
champions league ila kwa league ya ndani we
are almost there we need one more season then
tutakua mabigwa wa epl bila shida ...