Mkuu mimi naamini kabisa kua Monaco mtakwenda kuifunga sn tu km mlivoifunga ManU jana.
Huyu kocha wenu mzee Wenger pamoja na mapungufu yake, wakati mwingine akiamua kufanya kz yake ata dunia husimama kwa muda na kustaajabu.
Nakumbuka hapo nyuma, Ac Milan ilitoka hapo kwenu ikiwa imewafunga km sikosei hivo ikabidi Arsenal na yeye vovote vile akashinde kule Milano Italy. Na kweli na kabla ya kwenda huko Mzee Wenger alisema anataka kuushangaza ulimwengu na kweli Milan ilipigwa Mbili bila ndani ya Sanciro.
B, Munich walikuja hapo kwenu wakaifunga Arsenal kutokana na kadi nyekundu iliyotelewa kwa makusudi ya mwamuzi na kuifanya Arsenal kua pungufu na kufungwa na Munich.....na Mzee Wenger aliilalamikia sn hii kadi na maana ni km mwamuzi alifanya makusudi. Lkn mchezo wenu wa pili kule Ujerumani mliweza kumfunga Munich ingawa hamkuweza kusonga mbele.
Sasa nikiangalia hayo yote na nikiangalia mmeshinda away games mbili kubwa kwa Man City na Manu jana na nikiangalia Historia yenu ya kushinda pale mnapokua ktk hali ngumu bila kujali mko ugenini au lah, Basi ninaona mna kila sababu na uwezo wote wa kuifunga Monaco....ila mnaweza mkashinda lkn mkashindwa kuitoa Monaco na km mtapambana sn basi mataitoa Monaco.
Binafsi ningependa sn kuwaona bado mnashiriki UCL maana rafiki yangu utafiti ntakua siomuoni ktk vibanda umiza kuangalia mpira km mtatolewa mapema.
Hiyo ya ac Milan ilikuwa tumetoka 0-0 then kwao ndo tukashinda 2 bila!!na pia ipo record ya inter Milan kushinda kwetu 3-0 na tukaenda shinda 5-1 sansiro!!Yote yanawezekana hapo ni kujituma na kuwa makini zaidi mchezoni
Kiongozi ulichosema kina ukweli asilimia kubwa. Wenger amestaajabisha wengi, hasa timu inapokuwa katika wakati mgumu.
Tulifanya hivyo kwa AC Milan lakini tulitolewa kwa magoli ya ugenini, tukafanya hivyo hivyo kwa Bayern Munchen na kutolewa katika hali kama hiyo.
Ngoja tuone kwa Monaco hali itakuwaje. Tatizo wale jamaa hawafungiki kirahisi. Hilo ndio linanipa wasiwasi.
Nisalimie sister!
hahahaaaaaa Mpwa.........
Mani Huo ndiyo mpira.......kushinda ama kufungwa ama droo....sasa na lazma katika hayo moja litokee.....MAN U imetokea tumefungwa na timu ndogo kama arsenal ni mchezo tu.....ila next time mambo yatakuwa mazuri.......
Timu ndogo ngoja Jiwe akusikie.....
hahaaaaaa jana nilivyosikia haya matokeo nikakukumbuka
nikakumbuka na lile chimbo tuliloangalizia kipindi kile sijui kulikuwaje jana
kwa kweli nilifuatilia haswaaaaa......
hongereni sana rafiki.
will do that rafiki......Ahsante sana rafiki, salam kwa wote. Pole kwa ubusy wa kazi pamoja na hayo ulitafuta nafasi ya kuangalia. Uwe unaangalia mechi zetu nyingi maana kila ukiangalia tunashinda ππ.
Siku na kazi njema rafiki.
will do that rafiki......
Uwe na siku njema pia
Tunashukuru sana maana wachezaji wa MANU na wapenzi wa timu yao walisema hovyo sana kabla ya mechi kwa kujua kwamba mchezo ule wa jana wangeibuka kidedea sasa wamepakatwa tena nyumbani kwao, kimyaaaaaa.
Loh!!! Haya maneno ya mwisho ni magumu sana kwa Heaven on Earth maana naye ni MANU...........uwe unaweka tasfida kidogo jamani Lol.
Hmmmm! Mtakuwa mlimrubuni ππ Heaven on Earth ajiunge na timu yenu, siku zote hupenda sana kuiangalia Arsenal inapocheza ukilinganisha na MANU na hufurahia sana jinsi tunavyocheza mpira wa kuvutia ππ
Hajarubuniwa ni mpenzi wa Manu tu, ila sikuhizi ametukimbia haji kambini kumbe weye ndo wamvutia huku eh?
LoL! Ngoja aje aseme kama yeye ni mpenzi wa MANU au Arsenal. Usianze kumuandikia PMs ili aamue upendacho wewe ππ. Wewe mwenyewe inadaiwa unaihusudu sana ila ukosefu wa makombe kwa miaka kadhaa ukakufanya uhamie timu nyingine kama yule nanihii ππ