Paulista apatiwa "work permit"
Gabriel Paulista akiwa kazini.
Mchezaji huyu amepatiwa kibali hicho leo hii mchana baada ya wawakilishi wa AFC kuweka mezani mbele ya maofisa wa idara ya uhamiaji na wale wa FA, maelezo yao mazuri juu ya kwanini wanamhitaji mchezaji huyu ambae anachezea sehemu ya ulinzi wa kati au ""mkoba.
Pia leo hiihii jioni mchezaji huyu alitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na AFC huenda wakatangaza rasmi usajilki wa mchezaji huyu kesho mchana.
Gaby anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa katika dirisha la usajili la mwezi huu wa January baada ya Krystian Bielik ambae nae amekuwa mchezai rasmi wa AFC.
Mjue Gabriel:
1. Alizaliwa Sao Paolo nchini Brazil lakini kimpira alipitia katika shule ya vipaji maalum iitwayo Esporte Clube Vitoria iliyopo Salvador.
2. Alianza kucheza mpira kihakika dhidi ya Flamengo nchini Brazil.
3. Kwa utaalam ni beki wa kati lakini anaweza kucheza nafasi ya ulinzi wa pembeni kulia na kushoto.
4. Alichaguliwa kuwa ni mkoba na beki mshahara wa uhakika mwaka 2013 kwenye mashindano yaitwayo Campeonato Baiano ambapo timu yake ya Vitoria ilishinda.
5. Mwaka huohuo Villareal walimgundua na kumsajili kwa mkataba wa miaka mitano. Ameisadia timu hiyo kucheza mechi 15 hadi alipoanza mazungumzo na Arsenal mwaka huu na ilikuwa haitapoteza mchezo hata mmoja.
Karibu AFC Gaby.
COYG!!!