Wana Arsenal wenzangu, nimefurahi kuona special thread yetu huku, nilikua sijaiona. Lakini hebu tujikite kweye maswala ya msingi kidogo, Jana tumeskia the Legendary TH14 Thierry Henry, the best ever player to ever grace the Premier League kastaafu, niliskitika but ilibidi tu maana kila mtu anastaafu katika proffessional yake. Lakini hebua angalieni legend mwingime Patrick Vieira anavyo ifaidisha man city badala ya kuwa pale Ashburton Grove na mzee Wenger, Vivyo hivyo best ever defender Tony Adams mbona hatumtumii, je Henry atarudi Arsenal? Haya ni maswali ambayo siwezi kupata majibi yake.
Twende sasa kwenye swala la EPL. Dirisha la usajili lililopita Wenger alimuuza TV5, Akamuachia Sagna na Jenkinson kaenda kwa mkopo, badala yake ameleta defenders wawili, Debuchy na inexperienced Chambers, ni dhahiri tulikua tunahitaji defenders atleast wawili kabla ya hata kuwaruhusu hao walioondoka. Kikubwa zaidi tulihitaji Holding Midfielder, but mzee wetu hakununua, badala yake akamuacha Song aende West Ham kwa mkopo akitokea Barca, wakati Wenger ana first buy option kwa Song kama ilivyokua kwa Cesc. Kinachoniskitisha ni kuona wachezaji wetu waliokulia pale Emirates wakiwafaidisha wenzetu ambao mpaka sasa wapo juu yetu, nikimaanisha Chelsea, West Ham na Man City, kama ilivyokua Man utd mwaka juzi.
Hapa kuna mambo mawili, aidha Bodi imeshindwa kazi yake ama mzee wenger ameshindwa majukum yake. Something has to change at the Emirates kama the Legend Ian Wright alivosema juzi "Someone should be sacked for letting Fabregas join Chelsea"
Up The Gunners
#COYG