Wakuu mpo?
Ama kwa hakika kuna patashika na mchana wa leo Arsenal wameongeza dau kwa Alexis Sanchez na limefikia milioni 32 paundi.
Barcelona wamekubali dili hilo pamoja na mpango mzima wa malipo.
Counter attack hiyo imefanywa na Arsenal baada ya timu za Man City, Man Utd na Chelsea pamoja na Liverpool kuanza kuweka madau yao kwa mchezaji huyo.
Lakini Sanchez na wawakilishi wake wameona sense na kukubali hiyo offer ambayo ni kubwa kabisa kutokea kwa Arsenal kusajili mshambulaji baada ya ile milioni 42 waliyotoa kwa kiungo Mesut Ozil.
Wenger bado yupo Brazil mpaka Jumapili ijayo ndipo arudi London na Ivan Gazidis na Dick Law pamoja na wataalam wengine wa negotiations wapo Brazil na London kumalizia mambo.
Kama mambo yatakwenda ilivyopangwa, tarehe 10 mwezi huu Arsenal watatangaza aina mpya ya uzi wa Puma ambao umebeba deal la paundi milioni 150 ambazo ni pesa nyingi sana kuweza kutolewa kwa timu ya PL kama ya Arsenal. Pia wachezaji wa timu hio watapiga picha ya pamoja kuonyesha kikosi kamili na huenda wachezaji wapya wakawemo.
Dau hili la ufadhili linazidi paundi milioni 30 ambazo NIKE walikubaliana na Manchester Utd miaka kadhaa ilopita.
Hebu tuangalie recodi ya Sanchez akiwa Barca.
Meneja Arsene Wenger amewekea umuhimu usajili wa Alexis Sanchez.