Tatizo ni Ozila ambae anaogopa kuumia kabla ya World Cup. Amekuwa mzito kusababisha magoli inagawa alikuwa afunge goli la tatu na mpira ukagonga besela.
Pia rafu aliocheza Flamini haikuwa ya lazima bali ni kuzidisha matatizo tu kwa Arsenal maana Flamini atakosa mechi tatu, Rosicky anaumwa pua, na Walcott nae ndio hayupo kabisa, Ramsey jana akawa bado ahawezi kukimbia kutokana na msuli kuuma.
Arsenal itakuwa ok tu suala ni kuifunga Crystal Palace nyumbani siku ya Jumapili na kusubiri jumatatu Man City na Chelsea maana wao pia wanaweza kutuamulia ni nani ataenda kuwa bingwa.
Arsenal itatangaza usajili wa wachezaji wawili au pengine watatu ifikapo Ijumaa jioni.
Mmoja wao anaweza kuwa Draxler au hata Morata ingawa kuna majina mengine yameibuka jana baada ya kuwapoteza Flamini na Ramsey.
Stay tuned.