Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Matokeo mazuri Arsenal, good season so far.... ila huko Etihad kimewakaaaaa!
 
Nimemkubali dogo serge gnabry,anajua,ana mbavu za EPL halafu ni mbishi.
 
Nimeona kule Manyema united kupo kimya!
Jamani naombeni kujuzwa yaliyojiri Etihad stadium
 
Namsubiria sana hapo Novemba 10.

Haha mkuu Nzi huchoki tu?li-timu lenu mwaka huu libovu aisee, RVP ndo mtima wenu basiiiiii,akikabwa vizuri hamchomoki,manake hata arsenal waamshwe usingizini kwa mziki ule mtachezea kichapo sana!! Mark my word!!

Ingawa ubora wa timu kwa EPL ni kucheza na big 4 lakini I dare to say Arsenal wako vizuri msimu huu..labda wawe na mgogoro hapo badae!! Manake nimeona sehemu Carlo Anchellot anajuta sasahv kumuuza OZIL anadai eti aliomba mwenyewe aihame timu kwa kuhofilia kukaa benchi...does this sound good??
 
...hahaha..... Umenikumbusha "miaka ya 47" kulikuwa na dawa unamwagia on surfaces... Ya unga unga hivi, nzi wakitua tu wana rest in peace...

Halahala jamani, msipulize dawa mingi mkaua na mbu!


hahahaha mkuu hiyo ni kwa nzi tu !! ... Ameomba mpaka nov. 10 .. Ndio tumwage bana
 
Reactions: Mbu
Haha mkuu Nzi huchoki tu?li-timu lenu mwaka huu libovu aisee, RVP ndo mtima wenu basiiiiii,akikabwa vizuri hamchomoki,manake hata arsenal waamshwe usingizini kwa mziki ule mtachezea kichapo sana!! Mark my word!!

Bongo pundits bwana! Gemu 5 tu washaanza kusema timu libovu!! Hadi sasa ni points 15 tu ndiyo zimetafutwa; bado zipo 99 ambazo hata bingwa uwa ni nadra kuzifikia!!

Game styles ubadilika kutokana na timu zinavyocheza. Sasa kama wewe ni mfuasi wa soka huwezi kutumia matokeo ya jana kama benchmark ya matokeo ya United vs. Arsenal. United vs. Arsenal na United vs. City ni games 2 zilizo tofauti sana. Unakumbuka ule mwaka United ilivyowapiga Arsenal 8-2, kisha ikapigwa 6-1 na City? Sasa hapo utasemaje?!?

Tuombe uzima; tusiandikie mate. Novemba 10 jibu litapatikana.


Ligi ni sawa na mashindano ya marathon na si ya sprinting kama akina Usain Bolt. Hivyo hizo games 5 si kiashiria kizuri cha kujua kama timu itashinda marathon.
 
Ingawa ubora wa timu kwa EPL ni kucheza na big 4 lakini I dare to say Arsenal wako vizuri msimu huu..

Unakumbuka Arsenal hii ya mwaka 2007/08?

espnfc.com/team/squad/_/id/359/season/2007/league/eng.1/arsenal?cc=3888

Cheki hapa baada ya games 5..Arsenal at the top of EPL with 13 points.

www.statto.com/football/stats/england/premier-league/2007-2008/table/2007-09-17

But look at the end of season!

www.statto.com/football/stats/england/premier-league/2007-2008/table

Ligi ni marathon chifu.

Anyway hongereni kwa kuongoza ligi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…