Wakuu, baada ya pilikapilika za hapa na pale na mazungumzo ya muda mrefu mchezaji Gonzalo Higuain ameweka saini kwenye mkataba na Arsenal FC na atakuwa akilipwa paundi 130,000 kwa wili pamoja na "adds on" kama matumizi ya jina na mengine kufikia paundio 150,000 kwa wiki.
Higuain anavunja rekodi ya usajili uliofanywa kwa Andrey Arshavin mwaka 2008 ambao uligharimu kiasi cha paundi milioni 15.
Arsenal inaweza kutangaza mchezaji huyo siku ya Ijumaa au Jumatatu na anakuwa ni mchezaji wa pili kusajiliwa msimu huu baada ya Yaya Sanogo ambae anatoka Auxerre ya France.
Muda wa usajili ukiwa ndio unapamba moto bado inasemwa kwama Arsene Wenger anafikiria kumsajili Wayne Rooney wa Man Utd au Luis Nani pia wa Man Utd na pia Marouane Fellaini bado anazungumzwa.
Arsenal ina kiasi cha paundi 100 milioni za kutumia kwenye usajili wa sasa na January 2014 kama ikibidi na hiyo ni majumuisho ya milioni 70 zilizoko benki na milioni 30 ambazo zimetokana na kuondoa wachezaji wasiotakiwa kama Arshavin na Squillaci.
Maskauti wa Arsenal wamekuwa na muda mgumu katika soko la wachezaji huku kukiwa na taarifa kwamba mfumo wa kutambua vipaji unaofanywa kwenye mtandao maalum wa OPTA INDEx kuingiliwa na "hackers" ambao wamekuwa wakivumisha habari za usajili ziizo za kweli.
This is it na huu ndio usajili wa maana tuliotaka na inaonyesha jinsi miaka 8 ya bila kikombe ilivyokuwa ikiandaliwa.
Anaefuata ni Cesc Fabregas au Marouane Fellaini.
COYG.