Ni kawaida kwenye mechi ngumu kupoteza ikiwa mazingira na uchezaji hayakukamilika.
Timu yetu leo imecheza kipindi cha pili tu. Kipindi cha kwanza sikuona Diaby na Coquelin wakimiliki mipira pale katikati na kuwaachia Osca,Mata na Ramirez wakitawala mchezo.
Hongera kwa Chelsea lakini Arsenal kwa sasa tumepoteza mechi tatu za ugenini na mbili nyumbani.
Jumatano tunacheza mechi yetu ya kiporo na West Ham na itakuwa ni Emirates.