Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Goners mpo ...??? Napita kuwapa hi wadau

Sent from my hisense tablet honeycomb 3.2.1 using Tapatalk
 
Van Persie departure hint: Gunners release squad numbers - but no shirt for Podolski

Arsenal have announced their squad numbers for the 2012-13 season and although Robin van Persie has retained his No.10 shirt, new signing Lukas Podolski has yet to receive a number.

1 Wojciech Szczesny, 2 Abou Diaby, 3 Bacary Sagna, 4 Per Mertesacker, 5 Thomas Vermaelen, 6 Laurent Koscielny, 7 Tomas Rosicky, 8 Mikel Arteta, 9 Ju Young Park, 10 Robin van Persie, 11 Andre Santos, 12 Olivier Giroud, 14 Theo Walcott, 15 Alex Oxlade-Chamberlain, 16 Aaron Ramsey, 17 Alex Song, 18 Sebastien Squillaci, 19 Jack Wilshere, 20 Johan Djourou, 21 Lukasz Fabianski, 22 Francis Coquelin, 23 Andrey Arshavin, 24 Vito Mannone, 25 Carl Jenkinson, 26 Emmanuel Frimpong, 27 Gervinho, 28 Kieran Gibbs, 29 Marouane Chamakh, 31 Ryo, 35 Kyle Bartley, 52 Nicklas Bendtner, TBC Lukas Podolski .
 
Game letu na mancity soon linaanza ni friendly match ... Inachezwa nest stadium katika jiji la Beijing
 
I watched yesterday's game, vijana walicheza vizuri apart from two defensive errors that City capitalized. Wenger amewatest wachezaji wengi, watu kama Aneke, Bartley, Eisfield, Eastmond na wengine. Kipindi cha pili tulicheza vizuri zaidi and it shows kwamba uwepo wa striker wawili wapya (ambao hawajasafiri na timu) utaleta maumivu kwa wapinzani.
 
Naona Jack Wilshere anafuata nyayo za Owen Hagreaves
 
Naona Jack Wilshere anafuata nyayo za Owen Hagreaves



Nope! Anafuata nyayo za RVP, siku atakapokuwa na msimu mzima mzuri atataka kwenda Man City. Once a feeder club always a feeder club.
 
Mchezaji wa kiungo wa Malaga Santi Cazorla, leo mchana amewasili jijini London akitokea nchini Hispania ambapo atafanyiwa uchunguzi wa afya na baadae kukamilisha taratibu za usajili.

Santi-Cazorla-008.jpg


Santi Cazorla

Arsenal imekubali kuilipa Malaga kiasi cha paundi 17.3 (Arsenal hawajathibitisha) milioni na kuondoa tatizo la ukinzani kati ya wamiliki wa timu hiyo kwamba wauze wachezaji ili walipe madeni au waendelee kufadhiliwa na mwekezaji wa arabuni Sheik Abdullah Bin Nasser Al-Thani.

Ikiwa mipango yote itakamilika Cazorla mwenye umri wa miaka 27 atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Arsenal baada ya Lucas Podolski kutoka FC Cologne na Olovier Giroud kutoka Montpellier.

Pia Arsenal kama watakubaliana na Jose Mourinho meneja wa Real Madrid basi watamsajili kwa muda wa msimu mzima wa 2012/13, mchezaji wa akiba kiungo wa timu hiyo Nuri Sahin ambae ana asili ya Uturuki mwenye umri wa miaka 23.

Pia Arsenal inaangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo moja kwa moja pindi atakapozoea utaratibu mzima wa uchezaji wa timu hiyo ya Kaskazini mwa jiji la London.

hi-res-136034526_crop_exact.jpg

Nuri Sahin

Ikiwa timu hizo zitakubaliana masuala ya malipo na mkataba basi Sahin anaweza kuwasili mjini London ndani ya wiki moja ili kuwahi tarehe ya mwisho kabla ya muda wa usajili kumalizika.

Arsenal imeamua kusajili wachezaji wa kiungo kutokana na wachezaji Thomas Rosicky na Jack Wilshere kutokuwa tayari kurudi kucheza pindi msimu ujao utakapoanza ambapo Arsenal inafungua dimba kwa kucheza na Sunderland.

Thomas amefanyiwa upasuaji wa mfupa wa kisigino au "Achillies Tendon" na Jack anasumbuliwa na kifundo cha mguu au "ankle" na wachezaji hao itawachukua zaidi ya miezi miwili kuwa tayari kucheza kwa ushindani. Pia Aaron Ramsey anachezea timu ya taifa ya Uingereza inayoshiriki kwenye michezo ya Olympic na hadi anarudi kwenye ligi atakuwa hayupo tayari kutokana na uchovu.

Ikiwa Arsenal itaanza ligi na mtindo wa 4-3-3 ambayo itajumuisha Mikael Arteta, Alex Song na Abu Diaby inaweza kuleta tija kwenye eneo hilo ingawa itategemea na uzima wa Diaby ambae nae ana matatizo ya kupata majeraha ya mara kwa mara.

Lakini ikiwa Wenger atatumia mtindo wake wa kawaida wa 4-2-3-1 itakuwa ni mapema mno kwa wachezaji hao kushika kasi ya mchezo na hasa Diaby ambae nae ni hivi karibuni tu amerudi kutoka kwenye mpango wa matibabu.

Ligi ya Uingereza ni moja ya ligi ngumu duniani na yenye mikikimikiki mingi na mzee Wenger anapenda kuwa anabadilisha wachezaji mara kwa mara.

Ni kwasababu hio huenda pengine Arsenal inataka Cazorla na Sahin wasajiliwe ili wasaidie kuleta muiano wa uchezaji hasa sehemu ya kiungo. Sahin ni mchezaji mwepesi na mtaalam wa kupiga mipira ya adhabu.

Karibuni Arsenal Santa Cazorla na Nuri Sahin.

In Arsenal we trust.

 
Habari njema sana hio Mkuu Richard.

Naomba kila kitu kiende salama tuwapate hawa wachezaji.

Naona Barca wanamtolea macho Song.
 
Suala la Santi Cazorla - Update

Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 27 leo amekubali kutia saini mkataba na Arsenal ambao unagaharimu paundi milioni 16 na huenda zikaongezeka na kufikia paundi milioni 20 kutegemea na ufanisi wa uchezaji wake.

Santi-Cazorla-who-is-join-008.jpg



Santi Cazorla aliwasili jijini London jana jioni na kuelekea moja kwa moja kwenye zahanati ya timu hiyo.

Unaweza kuangalia video inayoonyesha zahanati mpya ya timu iliyofunguliwa mwishoni mwa mwezi uliopita.

http://www.arsenal.com/news/news-archive/medical-centre-opens-at-training-ground

Pamoja na huduma zote zinazohitajika kwa wachezaji, zahanati hiyo inaweza pia kutoa huduma za upasuaji kwa kuwa na vifaa vipya na vya kisasa kabisa "state of the art" kupatikana kwenye moja ya timu maarufu duniani.
 
Jamani nimemtizama RAMSEY toka Olympic inaanza dogo anajua jamani sasa sijui akivaa jezi za arsenal anakuwaje?
Waliotizama game yao na S.KOREA leo watathibitisha...kama si SHAWCROSS pale britania 2009 angekuwa mbali sana huyu dogo kwa kweli
 
Back
Top Bottom