Kama niliyowahi kueleza huko nyuma kwamba usajili wa Podolski ulikuwa "iminent" mchezaji huyo amekubali kutia saini mkataba na timu ya Arsenal FC ya Uingereza.
Baada ya kukamilisha usajili wa Lucas Podolski, Arsene Wenger sasa anashughulikia suala la usajili wa Jan Vertonghen ambae ni beki wa Ajax Amsterdam na timu ya taifa ya Belgium na ikiwa mambo yatakwenda vizuri usajili muhimu utakamilika kwa kumsajili mchezaji wa kiungo wa Rennes ya France Yann M' Villa.
Vertonghen amebakiza muda mfupi kwenye mkataba na Ajax na ikiwa mipango yote itakwenda uzuri basi mchezaji huyo atajiunga na beki mwenzie wa Belgium thomas Vernaelen.
Arsenal wanategemea kumsajili mchezaji huyu kwa kiasi cha paundi milioni 7 tu.
Usajili wa Podolski umegharimu kiasi cha paundi milioni 11 na mchezaji huyo atajiungana wenzake baada tu ya kumalizika kwa michezo ya Euro 2012.
Lucas Podolski akiwa na jezi ya Arsenal.
Usajili wa Arsenal mwaka huu umekuja kwa kuhofia kuchelewa kupata wachezaji ambao ni muhimu kwa baadhi ya sehemu za uchezaji wa timu hiyo hasa kwenye ulinzi, kiungo na ushambuliaji na Arsene Wenger ameona ni bora kufanya biashara mapema asubuhi.
Yann M' Villa anatarajia kugharimu kiasi cha paundi milioni si chini ya 18 na hata timu za Man Utd na Tottenham nao wanaangalia maendeleo yoyote yanayotokea.
Yann M' Villa
Hopefully kama mambo yatakwenda kama yanavyopangwa basi Arsenal itakuwa ni timu pekee ambayo ina rasilimali ya wachezaji wengi wa viungo akina Alex Song, Jack Wilshere, Mikel Arteta, Aaron Ramsey, Tomas Rosicky na Alex Oxlade-Chamberlain.
kama AW anataka kushinda hii game inabidi afanye mabadiliko mapema kipindi cha pili kwa kumtoa muisrael au gervinho na kumuweka Ox ili dogo aongeze mashambuli mbele
kama AW anataka kushinda hii game inabidi afanye mabadiliko mapema kipindi cha pili kwa kumtoa muisrael au gervinho na kumuweka Ox ili dogo aongeze mashambuli mbele
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.