Mnanikumbusha ile hadithi ya mchina alikuwa haelewani na mama mkwe wake, akaenda kwa mganga akiomba dawa ya kumwua. Mganga akamwambia nitakupa dawa inayoua taratibu kwa sababu kama akifa ghafla utashtukiwa. Mganga akampa majani yaliyosagwa vizuri akamwambia nenda mpikie chakula kizuuuuuri umwekee na hii daya kidogo. So kila siku ufanye hivyo na wewe umwonyeshe upendo yaani uwe naye karibu na umpe kila akitakaco. Akikutukana wewe cheka ni sehemu ya dawa so hata akijakufa watu hawatakushtukia wewe sana sana watakuonea huruma.
Bi dada akaanza kazi ya "kuua" akawa anajipikilisha vinono, anamcare yaani kuliko hata anavyomcare mumewe au mamake mzazi. Baada ya mwezi wakawa marafiki wa kufa yaani wakawa wanapiga story kupita maelezo. Ikabidi bi dada arudi kwa mganga amwambie anaomba dawa ya kupunguza makali ya sumu alokuwa anampa mama mkwe kwa kuwa kwa sasa hataki tena kumpoteza amekuwa rafiki yake mkubwa. Mganga akamwambia wala ile haikuwa sumu ni vitamins tu na kilichobadilisha tabia yake ni atitude yako na upendo na kujali unakompatia so endelea tu kuishi kwa furaha na rafiki yako.
So sometimes na sie wanawake tunapaswa kuangalia attitudes zetu towards wamama hawa. Ingawa nakiri wapo wale ambao hawapendeki yaani hata ufanye nini umlambe miguu kila asubuhi kama ishara ya kumshukuru kwa kukuzalia chema wapi.......atakubetulia mdomo. Mie huwa naangalia sana movie za kinigeria hasa zile za Patience Ozokwor "Mama Gee". akiamua kucheza kama mama mkwe mwenye roho mbaya huwa ananimaliza kabisa. But najifunza mengi
kaka Mbu umeniuliza chanzo cha mvutano, ni vijimambo vingi sana katika kutaka kuingilia mambo yangu ya ndani, na iliponitibua zaidi ni wakati nilipokofofishana na mr kwa kutaka niache kazi, baada ya kukosana amani ndani kwa karibia miezi 6 nikaja ambiwa chanzo ni mama yake kumshikia bango mr kwamba natakiwa niwe mama wa nyumbani, hilo tuliliongea na mr na tukasuluhisha kila kitu, baada ya hapo sasa mama akaanza kwamba cmtii mume wangu coz akitoa maamuzi ndani siyafatilii, hapo tulishaongea na mr kila kitu kuhusu mama, na akanipa support kubwa sana baada ya ule utata uliotokea, bac kwasasa support yake ndio inanipa moyo.
Kama ni upendo wa mama kweli, mbona wamama hawasumbui ndoa za binti zao kama wanavyoingilia za wakiume? Vipi wababa, hawana upendo? Mbona wababa hawasumbui ndoa za watoto wao wa kike wala wa kiume?
1. Usiyaweke moyoni, Upo wakati atajua makosa yake, usiyahesabu makosa yake, mpende kwa uvumilivu, bila kucount makosa, bila kujipndelea mwenyewe. Ifike wakati ujisikie fuiraha kqwa kuchangia kum[ponya mkweo.leo umeniamulia kunivunja mbavu....MJ1 kuna mambo unaweza kuyavumilia mengine hayavumliki kabisa, anataka akiwepo nyumbani nibadilike kimavazi, ooh mbona umebanwa hivyo huko ofcn kuna usalama, mara mama kwann unapenda kuvaa nguo za kuonyesha ulivyo kwann acvae kitenge, kitenge kuendea ofcn jamani MJ1, akiwepo kila jmc inabidi nijiendee ofcn kuepuka kero, jmc yenyewe hiyo navaa ka jeans nitaulizwa mama huko ofcn ukivaa hivyo mbona kama unawatenda vibaya wafanyakazi wenzio? yaani MJ1 hapana...lakini yeye huyo huyo kwa kulalamika kwamba mtoto wake wa kike anateswa na mama mkwe hajambo, yaani akianza kulalamika hapo hadi machozi, mie kirohoni nasema sawa kabisa!.
Mbu Darling hii yote inafanyika kwa ajili ya upendo mkuu walio nao hawa wawili juu yako. Mama anakupenda sana na mke anakuzimia kupita kiasi ila tu ni wivu unaowasumbua...
Wajua mama siku zote mwanae wa kiume hamwoni kama amekuwa na wala haamini kama kuna mwanake mwingine (zaidi yake) anayeweza kukutunza na kukupenda kama yeye so kila anachokifanya mke mama anaona anakosea. Ndio maana utakuta wamama wengine wanafikia hata hatua ya kulazimisha kipikwe aina flani cha chakula kwa kuwa mwanaye anakipenda yaani huwa wako emotional sana kiasi cha kujisahau.
Iama ni mke asokuwa na busara atatumia nguvu nyingi sana kukuwini wewe from your mom na kumwonyesha mamako kuwa yeye ni MWANAMKE wa shoka wakati mke mwenye busara huwa anajitahidi kumvuta mkwe upande wake kwa kumfanya rafiki yake so that aweze kupata la hapa na pale juu yako.
Nafikir tatizo kubwa huwa ni conflict of interest
myluv, ingekuwa kesi za mkwe hakutengewa chakula au kanyimwa mchuzi mbona hizo kesi wanaume wengi huzifumbia macho?
Hii kesi 'kwa mkichwa' bana,... Bibie povu linamtoka mdomoni!
Anyway,...hata kwa biblia imeandikwa kwenye methali 14:1 mke wa aina hiyo.
Na mashaka na huo ustahmilivu wa mume, ...pengine wengine huwaliza machozi mamazao wazazi 'walivyodhibitiwa' wake zao.
Kumtusi mama mzazi ili upendeke kwa mke si ndio laana zenyewe?
Kwa kuongezea..kama ni kunukuu maandiko Biblia hiyo hiyo kwenye kitabu cha mwanzo..utaona Mungu akiamrisha mwanaume na mwanamke kuwaacha baba na mama zao na kwenda kuanzisha maisha yao.
Mungu hakusema wakae na wazazi...alijua migogogro hii ya kunyang'anyana attention itatokea na kuvuruga amani.
Watu wanapooana ni busara zaidi kuwa na maisha yao bila kuwa na rejea kwa wazazi. Utaona katika jamii zote - waafrika, wahindi wazungu - kuna misemo mingi sana inayoashiria hali hii ya kutokuelewana baina ya mke na mama mkwe and vice versa.Hebu angalieni hii kwa mfano michache:
- Be kind to your mother-in-law, but pay for her board at some good hotel.- Josh Billing - hapa inaonyesha kabisa anavyojitahidi awe mbali na mama mkwe.
- I see by my mother-in-law's eyes when the devil takes hold of her.
- Well-married is when you have no mother-in-law and no sister-in-law.
--Spanish Proverb
Na hili la kutokuwapenda au kuelewana na wakwe siyo wanawake tu hata wanaume hutokea kutokuelewana na wakwe zao.