Arfi kuondoka CCM

Arfi kuondoka CCM

Mtu mzima ovulazione!Kimberly dile mvi ni jure kabisa
 
Hapo sasa itambidi aangalie chama kisicho na mgombea hapo kwenye hilo jimbo,na siasa ilivyo ya ajabu tusishangae aka win
 
Mbona kuatapatapa hivyo. Utulivu hana.
Wasaka tonge utawajua tu kwa matendo wanataka wao ndio wawe washindi kila uchaguzi hawaamini kama wapo wengine ,wakishindwa hukimbilia kwingine,tatizo sio vyama,vyama havipigi kura ,kura inapigwa na wale waliokuchagua hao ndio wakiona umekuwa zigo wanakutosa ,matokeo wasaka tonge hubadili vyama kama vile wanavyobadili vyupi.
 
Mzee ALFI tulia Mkuu CCM ina mpango Wa kukupa UKURUGENZI Wa Halmashauri ya MILELE?
 
Mzee arfi you signed for your destruction.... Zingine porojo tu!!
 
Hiv huyu mzee kwani hana wajukuu wa kucheza nao dakika hizi za uzeeni!
 
Walewale wa Tamaa ya Madaraka kwani na wewe siulikuwa una washinda watu?
 
Makete Kwetu sita mapembelo ya bhene?

Mzee Arfi kaangushwa kura za maoni ktk Jimbo jipya la NSIMBO siyo Mpanda Kati
 
Last edited by a moderator:
lile jimbo ni la CHADEMA hata akigombea Kikwete na mtu yeyote wa CHADEMA lazima CDM itashinda tu
 
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Ndg.Said Amour Arfi ambaye alijiunga na Chama cha mapinduzi (CCM) hivi karibuni amesema anafikiria kujiondoa CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani (hakukitaja jina), kwa kuwa hakuna demokrasia ya kweli ndani ya CCM.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii kwa njia ya simu, Arfi amesema alijiondoa CCM mwaka 2000 na kujiunga na TLP kwa sababu CCM haikua na demokrasia, hivyo alitegemea miaka 15 aliyokaa nje ya CCM ingeweza kuibadilisha lakini hadi sasa hali ni ileile.

Arfi alitupwa nje kwenye kura za maoni ndani ya CCM kupitia jimbo la Mpanda Kati ambalo ameliongoza kwa miaka 10. Hata hivyo anafikiria kutetea kiti chake hicho cha ubunge kupitia chama kingine nje ya CCM. Watafiti wa masuala ya siasa wanasema huenda akajiunga na ACT wazalendo.

Arfi alikuwa mwanachama wa CCM hadi mwaka 2000 alipoondoka na kujiunga na TLP. Mwaka 2005 alijiondoa TLP na kujiunga CHADEMA ambapo alipata fursa ya kugombea Ubunge na kushinda kwa vipindi viwili mfululizo.

Mwaka huu alijiondoa CHADEMA na kurudi CCM, lakini ameangushwa kwenye kura za maoni na hivyo anafikiria kuondoka CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani ambacho hakukitaja.

Duh! Huyu mzee kiboko. Kweli alitegemea kambi aliyoinyea aikute safi inamsubiri?
 
Mchumia tumbo tu huna hana mbongo ya kuchanganua mambo.

Nilipoona Mchumia nikadhani Rungu kumbe Mchumia Tumbo :smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big:. Heri tu awe Mchumia Rungu tu, hataweza kukosa mbongo ya kuchanganua mambo teteteteh!
 
Back
Top Bottom