Arfi kuondoka CCM

Arfi kuondoka CCM

Mkuu hii ni lugha gani? Kidogo ifanane na kipare.

Baba ni yale mambo ya kibodi android,mie nabofya kiswahili kumbe sijahakiki, yaani hiyo nami ndio nashangaa hivi niliandika madudu-This is what I intended to say :Mtu mzima ovyo kumbe zile mvi ni Bure kabisa'
 
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Ndg.Said Amour Arfi ambaye alijiunga na Chama cha mapinduzi (CCM) hivi karibuni amesema anafikiria kujiondoa CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani (hakukitaja jina), kwa kuwa hakuna demokrasia ya kweli ndani ya CCM.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii kwa njia ya simu, Arfi amesema alijiondoa CCM mwaka 2000 na kujiunga na TLP kwa sababu CCM haikua na demokrasia, hivyo alitegemea miaka 15 aliyokaa nje ya CCM ingeweza kuibadilisha lakini hadi sasa hali ni ileile.

Arfi alitupwa nje kwenye kura za maoni ndani ya CCM kupitia jimbo la Mpanda Kati ambalo ameliongoza kwa miaka 10. Hata hivyo anafikiria kutetea kiti chake hicho cha ubunge kupitia chama kingine nje ya CCM. Watafiti wa masuala ya siasa wanasema huenda akajiunga na ACT wazalendo.

Arfi alikuwa mwanachama wa CCM hadi mwaka 2000 alipoondoka na kujiunga na TLP. Mwaka 2005 alijiondoa TLP na kujiunga CHADEMA ambapo alipata fursa ya kugombea Ubunge na kushinda kwa vipindi viwili mfululizo.

Mwaka huu alijiondoa CHADEMA na kurudi CCM, lakini ameangushwa kwenye kura za maoni na hivyo anafikiria kuondoka CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani ambacho hakukitaja.

Sasa Huo ni Umalaya wa Kisiasa...yeye kujiungaa ccm Leo anataka ashinde na uteuzi .....na Umri wake Huo apumzike tu !!!!!!
 
Back
Top Bottom