Arfi kuondoka CCM

Arfi kuondoka CCM

Kiukweli si vyema na sipendi kuwatukana wazee....... Lakini Arfi ni Mpumbavu

.....mpuuzi kabisa yule mzee!

Bado atatanga na njia mpaka apate pressure.
Haki ya Mungu hawezi tena kupata ubunge mpaka age. Mark my words kamanda.
 
Ya kweli hayo? Km ni kweli basi huyu mzee atavunja record ya kuhama vyama kabla ya October.
 
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Ndg.Said Amour Arfi ambaye alijiunga na Chama cha mapinduzi (CCM) hivi karibuni amesema anafikiria kujiondoa CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani (hakukitaja jina), kwa kuwa hakuna demokrasia ya kweli ndani ya CCM.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii kwa njia ya simu, Arfi amesema alijiondoa CCM mwaka 2000 na kujiunga na TLP kwa sababu CCM haikua na demokrasia, hivyo alitegemea miaka 15 aliyokaa nje ya CCM ingeweza kuibadilisha lakini hadi sasa hali ni ileile.

Arfi alitupwa nje kwenye kura za maoni ndani ya CCM kupitia jimbo la Mpanda Kati ambalo ameliongoza kwa miaka 10. Hata hivyo anafikiria kutetea kiti chake hicho cha ubunge kupitia chama kingine nje ya CCM. Watafiti wa masuala ya siasa wanasema huenda akajiunga na ACT wazalendo.

Arfi alikuwa mwanachama wa CCM hadi mwaka 2000 alipoondoka na kujiunga na TLP. Mwaka 2005 alijiondoa TLP na kujiunga CHADEMA ambapo alipata fursa ya kugombea Ubunge na kushinda kwa vipindi viwili mfululizo.

Mwaka huu alijiondoa CHADEMA na kurudi CCM, lakini ameangushwa kwenye kura za maoni na hivyo anafikiria kuondoka CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani ambacho hakukitaja.

Huyo mzee ndio kesha jichanganya kwa kudanganywa na maccm wakati wa bmk kwa kuwasaliti viongozi wenzake wa ukawa kwa tamaa ya posho,sasa ubunge ndio basi tens.huko act hata udiwani haupati kabisa
 
wengne wakiama ni demokrasia wengne ni waraf wamadaraka duuh
 
Hakaribishwi mtu ccm ili agombee,kawakuta wanaccm huko akafikiria atapishwa,no no no. Hayo ya Chadema unaingia leo unateuliwa kugombea urais. Kule hapana banaaa kuna wenyeji waliokijenga chama hadi kufikia hapo halafu anakuja mtu tu katoka Chadema apewe? Nooooo lazima afate taratibu za chama
 
Atajuta kuondoka CHADEMA, mpuuzi huyu. Ni heri kuondoka chama tawala na kuja upinzani kuliko kuondoka upinzani kwenda tawala....huyu mzee ubunge atausikia redioni na TV. Acha dunia imfunze, ndio ajue CCM walikuwa wanamrubuni akadhani wanampenda akasaliti CHADEMA. Na akome!!!

Huo ndio Mshahara wa wasaliti
 
shikamoo ccm. Maana kwenye bunge la katiba alijifanya kidume eti anatetea wananchi. Ametumika kama ile mipira sasa hana la kufanya. Ccm ndivyo wanavyowaua kisiasa kwa vipande vya pesa

Umenikumbusha msaliti wa kigoma
 
Back
Top Bottom