Arfi kuondoka CCM

Arfi kuondoka CCM

Dah CCM hawana fadhila ya makubaliano mliyompa katika Bunge la Katiba, Aibu kwake ulishatumiwa huna thamani tena.
 
Hafai hata kidogo, yeye shida yake ni madaraka na uongozi. Kwake anajitafutia chakula tu hapo!

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Ndg.Said Amour Arfi ambaye alijiunga na Chama cha mapinduzi (CCM) hivi karibuni amesema anafikiria kujiondoa CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani (hakukitaja jina), kwa kuwa hakuna demokrasia ya kweli ndani ya CCM.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii kwa njia ya simu, Arfi amesema alijiondoa CCM mwaka 2000 na kujiunga na TLP kwa sababu CCM haikua na demokrasia, hivyo alitegemea miaka 15 aliyokaa nje ya CCM ingeweza kuibadilisha lakini hadi sasa hali ni ileile.

Arfi alitupwa nje kwenye kura za maoni ndani ya CCM kupitia jimbo la Mpanda Kati ambalo ameliongoza kwa miaka 10. Hata hivyo anafikiria kutetea kiti chake hicho cha ubunge kupitia chama kingine nje ya CCM. Watafiti wa masuala ya siasa wanasema huenda akajiunga na ACT wazalendo.

Arfi alikuwa mwanachama wa CCM hadi mwaka 2000 alipoondoka na kujiunga na TLP. Mwaka 2005 alijiondoa TLP na kujiunga CHADEMA ambapo alipata fursa ya kugombea Ubunge na kushinda kwa vipindi viwili mfululizo.

Mwaka huu alijiondoa CHADEMA na kurudi CCM, lakini ameangushwa kwenye kura za maoni na hivyo anafikiria kuondoka CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani ambacho hakukitaja.
 
Bora angeenda ACT walikokimbilia watoto wake, sijui kwa nn hawakumshari mzee
 
Shonza na Mwampamba wanatamani kuondoka CCM ila wanaona aibu.
 
Hii inaonesha kukosa msimamo wa kisiasa. Hatari kwa watanzania kutoka kwa viongozi wa aina hii. Tuwakatae popote watakapokua.
 
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Ndg.Said Amour Arfi ambaye alijiunga na Chama cha mapinduzi (CCM) hivi karibuni amesema anafikiria kujiondoa CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani (hakukitaja jina), kwa kuwa hakuna demokrasia ya kweli ndani ya CCM.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii kwa njia ya simu, Arfi amesema alijiondoa CCM mwaka 2000 na kujiunga na TLP kwa sababu CCM haikua na demokrasia, hivyo alitegemea miaka 15 aliyokaa nje ya CCM ingeweza kuibadilisha lakini hadi sasa hali ni ileile.

Arfi alitupwa nje kwenye kura za maoni ndani ya CCM kupitia jimbo la Mpanda Kati ambalo ameliongoza kwa miaka 10. Hata hivyo anafikiria kutetea kiti chake hicho cha ubunge kupitia chama kingine nje ya CCM. Watafiti wa masuala ya siasa wanasema huenda akajiunga na ACT wazalendo.

Arfi alikuwa mwanachama wa CCM hadi mwaka 2000 alipoondoka na kujiunga na TLP. Mwaka 2005 alijiondoa TLP na kujiunga CHADEMA ambapo alipata fursa ya kugombea Ubunge na kushinda kwa vipindi viwili mfululizo.

Mwaka huu alijiondoa CHADEMA na kurudi CCM, lakini ameangushwa kwenye kura za maoni na hivyo anafikiria kuondoka CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani ambacho hakukitaja.

atahangaika sana, dhambi ya usaliti inamtafuna!
 
Heri ya mchawi kuliko mnafiki, anavuna alichopanda sasa
 
Mnunulieni kyondomu za kike malaya huyu anapigwa mande kila kona.
 
Back
Top Bottom