Arfi kuondoka CCM

Makete Kwetu

JF-Expert Member
Jan 8, 2012
531
165
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Ndg.Said Amour Arfi ambaye alijiunga na Chama cha mapinduzi (CCM) hivi karibuni amesema anafikiria kujiondoa CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani (hakukitaja jina), kwa kuwa hakuna demokrasia ya kweli ndani ya CCM.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii kwa njia ya simu, Arfi amesema alijiondoa CCM mwaka 2000 na kujiunga na TLP kwa sababu CCM haikua na demokrasia, hivyo alitegemea miaka 15 aliyokaa nje ya CCM ingeweza kuibadilisha lakini hadi sasa hali ni ileile.

Arfi alitupwa nje kwenye kura za maoni ndani ya CCM kupitia jimbo la Mpanda Kati ambalo ameliongoza kwa miaka 10. Hata hivyo anafikiria kutetea kiti chake hicho cha ubunge kupitia chama kingine nje ya CCM. Watafiti wa masuala ya siasa wanasema huenda akajiunga na ACT wazalendo.

Arfi alikuwa mwanachama wa CCM hadi mwaka 2000 alipoondoka na kujiunga na TLP. Mwaka 2005 alijiondoa TLP na kujiunga CHADEMA ambapo alipata fursa ya kugombea Ubunge na kushinda kwa vipindi viwili mfululizo.

Mwaka huu alijiondoa CHADEMA na kurudi CCM, lakini ameangushwa kwenye kura za maoni na hivyo anafikiria kuondoka CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani ambacho hakukitaja.
 
Uroho wa madaraka na njaaa kali tumboni vina sumbua sana raia hawa wa Tz
 
Atajuta kuondoka CHADEMA, mpuuzi huyu. Ni heri kuondoka chama tawala na kuja upinzani kuliko kuondoka upinzani kwenda tawala....huyu mzee ubunge atausikia redioni na TV. Acha dunia imfunze, ndio ajue CCM walikuwa wanamrubuni akadhani wanampenda akasaliti CHADEMA. Na akome!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom