APPT-Maendeleo, CHAUMA Wamuunga Mkono Lowassa/UKAWA

APPT-Maendeleo, CHAUMA Wamuunga Mkono Lowassa/UKAWA

kiukweli kama wapinzani wangekuwa na dhamira njema ya kuiondoa ccm madarakani. walipaswa kuunga mkono mgombea wa ukawa. ili mpambano wa kweli uwe ni kati ya ccm na wapinzani. mpambano ungekuwa mkali sana...
 
Mkuu tafadhali! hawa jamaa kumuunga mkono ama kumvhagua Lowassa wana maana ya kwamba kama CCM ingempitisha Lowassa basi wao wasingekuwa na pingamizi maana ndiye wanayetegemea kuleta mageuzi, sasa tujiulize ni mageuzi gani hayo? Na hawa CHAUMA wameonyesha wazi kwamba sio wamewaunga mkono UKAWA bali Lowassa na hivyo wangemuunga mkono hata kama angechaguliwa na CCM. Ndivyo kisiasa inavyotafsirika.

Kama UKAWA walikuwa na dawa dhidi ya Lowassa na walijiandaa vema dhidi ya Lowassa na mgombea wao ikiwa Lowassa atapitishwa na CCM, basi hizo ndizo sababu zingewafanya wasimchukue Lowassa kwani uchaguzi wa rais unatokana na sifa za mgombea sio Chama kwa ujumla. Mrema alifanya vizuri kwa sababu wananchi walimtazama yeye na sio NCCR na hata Dr. Slaa 2010 kama Chadema ingemsimamisha Mbowe bila shaka matokeo yangekuwa tofauti kabisa na ndio maana CDM wakampitisha Dr.Slaa.

Kwa hiyo unajaribu a Chadema kwa vipi kwani wananchi hawakuiona Chadema wakati wa Dr.Slaa ama Mbowe na kwa nini hawakuichagua ikiwa itikadi na sera zake ni zile zile!. Mkuu hatupo katika majaribisho, na wala hatuna wakati huo kwa sasa isipokuwa tumefungiwa kanya boya tukiamini kuna mbuzi katika gunia.

Hii Chadema itaongoza vipi? kwa hizo ahadi za Lowassa! mtu hatangazi hata sera za Chadema isipokuwa it's all about him, leo anatuhakikishia kwamba Mkataba wa Richmond ulikuwa safi kabisa na kusema ilikuwa kosa kufuatilia kesi hiyo ilitugharimu millioni mia moja na sijui ngapi, wakati leo inatugharimu zaidi ya hicho karibu kila mwezi na umeme bado hautoshelezi!

Huyu kweli ni mtu wa kumpa nafasi kubwa azungumze uongo kwa niaba yenu kwamba haoni kama kulikuwa na makosa yalipofanyika ilihali watu wote tunaamini yalikuwa makosa!. Huyu huyu leo anadai ati alitaka kuuvunja mkataba na kwa ushahidi gani? tumuamini tu leo hii. Richmond - shirika la kitapeli la uchapishaji Houston, owner wake mhindi tumekua naye Gerezani na address ya Rostam iwe mkataba safi kabisa ulosifika ha Obama na Mama Clinton sijui baada ya kuuziwa Symbion! Lini rais wa Marekani akaingilia biashara za mashirika hata kutamka maneno kama hayo!. Huu ni uongo ulopitikliza!

Sisi tunaoishi nchi hizi tunajua fika rais wa nchi hawezi kabisa kusema maneno hayo ktk mikataba ya mashirika isimhusu na kama unakumbuka Waziri mkuu wa Canada Harper alipokuja Dar aliombwa kutusaidia juu ya Mkataba wetu na Barricks! Na akasema yeye hana mamlaka hayo maadam tumeshafunga mkataba tukajadili na wawekezaji! Leo Lowassa anaudanganya Umma kwamba Obama alisifia mitambo ya Richmond na maneno haya anayasema kwa tiketi ya Chadema (UKAWA) mnakubali tu!..

Mnasikitisha sana ndugu zangu, sijui haya mageuzi yenu yanalenga kugeuzwa kwa chapati ili iive pande zote mbili..

Mkuu umenena na tusichoke kabisa kuwapa ukweli
Angalia kuna article ya 2011 na ya 2014 inayoonyesha Mbowe alishaanza mazungumzo na Lowassa tangu kipindi kile.
"Usaliti " wa Zitto ulikuwa kumkataa. Hii inadhihirisha kuwa Mbowe kweli aliuza chama. Nasema wacha tuweke mabadiliko ktk backburner na tusubiri Zitto na wana mageuzi wengine wadhati wajipange lakini si kukabidhi nchi kwa genge la mafisadi ambalo lilitesa CCM (na bado kwa kiasi). CCM it's a matter of time lakini hawa jamaa wana njaa na tamaa za kijinga hapana! Watatuuza mpk vizazi vyetu.
Wapi Dr Slaa?
 
Mkuu Mabaradhuli ni hawa mnaowapokea mkidhani wanaume kumbe mashoga tu..Mtandao ni zaidi ya fikra zenu na mnachoshangilia mimi sikioni kabisa kwa sababu Lowassa hawezi kuwa Chadema ikiwa Chadema ndio wamemfuata! hakuna mtu alowahi kujiunga na CDM kwa kuombwa yeye ajiunge na kuahidiwa nafasi kama ile.. CDM needed Edo sio kinyume. Lowassa ni Mbwa mwitu alovaa ngozi ya kondoo akiwa ndani ya zizi la kondoo ama niseme hivi Lowassa ni sawa na Chatu, mbwa humfuata wenyewe na wakabanwa mbavu na kumezwa, wewe na mimi hatutaijua sababu!.

Miaka 20+ sio swala la CCM kimaadili, hakuna mahala popote yameandikwa hayo waloyafanya kwa miaka hiyo isipokuwa wamegawanyika katika uchumia tumbo kutokana na mvutano wa kama katika kapu nla mvuvi. Kwa miaka zaidi ya 30 walikuwa wote hawa maskini kama sisi wakizeeka na umaskini wao. Toka Mwinyi hadi JK agenda ni swala la watu hao kutokana na Umaskini, kila mmoja wao kachuma kwa wakati wake na hata walipotoka tamaa za utajiri zaidi zikawashika wakaanza kuumizana wenyewe. Hii ni vita baina ya Fisi na Simba, wewe nyumbu unafurahia nini na kusema bora ya Fisi kuliko Simba?
Wewe Mkandara uko upande upi sasa?

Kuunga mkono mabadiliko au tuendelee kuipa CCM miaka kumi mingine?

Nakusoma sana, lakini hautoi alternative zaidi ya kuwapinga tu UKAWA na mkakati wao huu waliokuja nao!

Please tell us. Unajua nyie ni wachambuzi wetu wazuri wa mambo ya kisiasa za Tanzania na binafsi huwa nafuatilia sana mijadala yenu na akina Nguruvi3, Mchambuzi, Mag3, Waberoya and others kule jukwaa la Great Thinkers na hujifunza mengi sana.

Lakini huku mbona kama una piga soga tu badala ya kukosoa na kutoa altenative as a way forward

Pls sometimes muhamishie mijadala ya kina ya hoja ya kule GT huku JS ili vijana wajifunze kitu.
 
Jana kupitia kipindi cha Mtiti wa Uchaguzi cha ITV walikuwa na mgombea wa Uraisi kupitia CHAUMA anaitwa Hashimu Rungwe aliweka bayana jinsi UKAWA walivyomtosa kwenye kinyang'anyiro cha Uspika wa Bunge la Katiba dhidi ya Mh.sitta. Anasema yeye alichukua fomu na wakajitokeza Prof. Lipumba, Mbowe na James Mbatia kumuunga mkono na kumdhamini lakini mwisho wa Siku wa kurudisha fomu akaambiwa UKAWA wamekubaliana na mgombea wa CCM kwamba atasimamia masilahi yao na atawalinda kwa hiyo wakamuambia ajitoe yaye akagoma na wajumbe wa Bunge maalumu la katiba kwa vyama visivyo na wabunge wakachukua fomu nyingine na kuijaza na hatimaye akafanikiwa kugombea na kuambulia KURA 80 wakati wajumbe wa CDM na CUF wanazidi idadi hiyo.

Point hapa Je viongozi wa UKAWA wako makini kweli? mpaka wakamuamini SITTA kwamba atasimamia masilahi yao wakati wanajua fikra 6 ni CCM na alijeruhiwa kipindi cha Uspika wa Bunge kwa kwenda kinyume na CCM halafu leo arudie yaleyale. Nimemuamini Hasimu Rungwe sababu hata SUGU aliwahi kusema Sitta kawadanganya UKAWA walikubaliana naye na alimuomba SUGU ampigie debe. Hapa wamenitia shaka sana na bado hawajifunzi wanaendelea kuwakumbatia MACCM. Nchi ya watu millioni 40 Bado vyama pinzani wanaendelea kupigania watu wa ccm ambao wamechoka na hawana muelekeo wa kubadilika, wakati kuna vijana wengi san tena wenye Elimu na fikra mpya.
 
Si unaona wamemwamini Lowassa aliyeingia asubuhi mchana kuchukua fomu ya kugombea urais na jioni kuteuliwa? Hapa hakuna umakini, ni maslahi tu ndio yanatazamwa. Ila Subiri kashfa na matusi toka UKAWA Lowassa. 😷
 
Wewe Mkandara uko upande upi sasa?

Kuunga mkono mabadiliko au tuendelee kuipa CCM miaka kumi mingine?

Nakusoma sana, lakini hautoi alternative zaidi ya kuwapinga tu UKAWA na mkakati wao huu waliokuja nao!

Please tell us. Unajua nyie ni wachambuzi wetu wazuri wa mambo ya kisiasa za Tanzania na binafsi huwa nafuatilia sana mijadala yenu na akina Nguruvi3, Mchambuzi, Mag3, Waberoya and others kule jukwaa la Great Thinkers na hujifunza mengi sana.

Lakini huku mbona kama una piga soga tu badala ya kukosoa na kutoa altenative as a way forward

Pls sometimes muhamishie mijadala ya kina ya hoja ya kule GT huku JS ili vijana wajifunze kitu.
Katika hali tulofikia mimi sina Upande in fact sitapiga kura na hata kama ningekuwa na kadi ya kupiga kura ingenipa shida kuchagua mbora kati ya Simba na Fisi maana Wadanganyika ni kama Nyumbu malishoni. Kwa hiyo sitazami kilicho bora kwangu mimi bali kwa wananchi wenyewe na ndio somo langu kuu. It's not about me but fellow Tanzanians!

Miaka yote nimekuwa na Chadema kwa sababu walisimamia misingi imara yenye lengo la kuwakomboa wananchi dhidi ya sera za CHUKUA CHAKI MAPEMA laa sivyo CCM kama chama hakina tatizo na ndio maana tunajikumbusha na Mwalimu Nyerere. Hiki chma hakikuwa hivi isipokuwa kimetekwa na kundi la WATU ambao nashangaa mnashindwa kuwatazama wao na kuwachuja mkawavuta kwenu walokuwa na fikra za ukombozi wa wananchi. Tunataka na kuomba tumpate kiongozi mwenye uchungu kama wa mwalimu hata kama siasa zake zitatugharimu kiasi gani. Huyu mtu ndiye bado hajapatikana na ndio maana tukaitaka kwanza KATIBA MPYA ili kulazimisha Uadilifu, uwajibikaji, usawa na Uzalendo kupitia katiba hiyo na sii taifa lenye serikali ngapi!. First thing First!

Na siwezi kutoa Altenative kwa sababu napingana na hali halisi ambayo haiwezi kubadilika! Na siwezi kuwashawishi viongozi wala wananchi mahala ambapo nature imetuweka kuwa na hawa Simba na Fisi isipokuwa nachoweza tu kufanya ni kuwakumbusha na kuwaasa kutoamini kuwepo kwa Simba na Fisi baina yetu katika nyika hii ni kutokaa na mapenzi yao kwetu!.Ndio maana na explore tu Uhalisia wa issues (in reality)

Wanasiasa karibu wote ni wachumia tumbo it's a trend kila mtu anataka kuwa mwanasiasa kama fashion vile. Na sii rahisi kumtofautisha mmoja kati ya wengine haswa pale wanapoitwa waheshimiwa na wakaheshimiwa kweli! Hakuna mbunge hata mmoja leo ni maskini utasikia wanachukia umaskini baada ya kutumikia..Hawa sii wenzetu na kila mmoja wao yupo radhi kutumia mabillioni alovuna toka kodi zenu ama wafadhili kununua kura zenu kwa takrima ili apate kuchaguliwa - WHY?

Sababu ni kupata POWER na ukiwa na Power utaweza endesha miradi yako pasipo kuulizwa ama kuzuiwa na sheria yoyote. Nguvu kubwa mnayotumia kumnadi Lowassa ni katika jicho la kupika keki ipate kuiva juu na chini bila kujua kuwa maandalizi haya walaji wa keki hiyo ni hao hao wanaopika!
 
Mkandara,

..acha tuwape ukawa uchaguzi huu.

..hiyo itamsafishia zitto njia kuchukua nchi 2020.
Mimi sidhani kama Zitto ataweza kuwa rais wa Tanzania mwaka 2020 maana itachukua miaka mingi kwa ACT kujenga imani mpya za watu kutoka kuishi kwa mazoea na naweza sema kwamba pengine January Makamba is our next President! Na Usishangae kabisa kwani kanishangaza sana katika matokeo ya mwaka huu ndani ya CC. Nje ya CCM bado kabisa ushindi kupatikana hilo nakuhakikishia...

Kwani jinsi wananchi walivyogeuka ghafla kutoka watu walokuwa wakilaani Ufisadi (Uhalibifu wa mali za umma) leo wameubeba wao kwa mbereko, mabango na njuga kama viongozi wa CCM 1960s walokuwa wakilaani RUSHWA na kunadi UZALENDO mara ghafla alipoingia Mwinyi wote wakaibwaga chini na kuchuma kwa Ruksa na mabango! Hakuna rais alopendwa kama Mwinyi japo kiuchumi ilikuwa laana. Hii yenu na Edo imekuwa reflection of who we are! Sisi ni WANAFIKI (Husema uongo, tukiahidi hatutimizi na tukiaminiwa hufanya Hiyana) haya yote yamejionyesha wazi mwaka huu.

Na usije shangaa ukiambiwa majority ya wapiga kura wetu ni swingers! Hawa jana walimchukia Edo, leo ndiye kipenzi chao na sababu hawana. Hawa watu wanaweza kugeuka wakati wowote na itakuwa kazi kubwa sana kwa Zitto na ACT kuwasoma watu hawa (maskini walalahoi wanaokumbatia Mtandao ule ule waloulaani kwa miaka 20+ dhidi ya CCM klwa kuyadhoofisha maisha yao. Hii inanipa picha mpya kabisa ya kwamba sio swala la vyama vya siasa kukosea kujinadi na sera ama siasa zake bali Adui wetu mkubwa ni sisi wananchi maskini wenyewe - WANAFIKI na ukiwaendekeza mtalala wote njaa.

CCM inajenga mbinu zake kwa kutambua maskini umpe nini, umfanyie nini, umdanganye nini na hivyo ndio maana wameweza kutawala kwa miaka mingi kama alivyokuja Wakoloni. Tumemuondoa Mkoloni baada ya kututawala kwa miaka mingapi vile? na walokuja kuleta mageuzi na fikra mpya karibu wote walitoka nje ya nchi sio wananchi wakazi wenyewe wanaoishi kwa mazoea! Haya maisha ya mazoea hadi yaje kututoka itachukua pengine fikra kundi la watu kutoka nje tena - who knows!
 
Mkuu tafadhali! hawa jamaa kumuunga mkono ama kumvhagua Lowassa wana maana ya kwamba kama CCM ingempitisha Lowassa basi wao wasingekuwa na pingamizi maana ndiye wanayetegemea kuleta mageuzi, sasa tujiulize ni mageuzi gani hayo? Na hawa CHAUMA wameonyesha wazi kwamba sio wamewaunga mkono UKAWA bali Lowassa na hivyo wangemuunga mkono hata kama angechaguliwa na CCM. Ndivyo kisiasa inavyotafsirika.

Kama UKAWA walikuwa na dawa dhidi ya Lowassa na walijiandaa vema dhidi ya Lowassa na mgombea wao ikiwa Lowassa atapitishwa na CCM, basi hizo ndizo sababu zingewafanya wasimchukue Lowassa kwani uchaguzi wa rais unatokana na sifa za mgombea sio Chama kwa ujumla. Mrema alifanya vizuri kwa sababu wananchi walimtazama yeye na sio NCCR na hata Dr. Slaa 2010 kama Chadema ingemsimamisha Mbowe bila shaka matokeo yangekuwa tofauti kabisa na ndio maana CDM wakampitisha Dr.Slaa.

Kwa hiyo unajaribu a Chadema kwa vipi kwani wananchi hawakuiona Chadema wakati wa Dr.Slaa ama Mbowe na kwa nini hawakuichagua ikiwa itikadi na sera zake ni zile zile!. Mkuu hatupo katika majaribisho, na wala hatuna wakati huo kwa sasa isipokuwa tumefungiwa kanya boya tukiamini kuna mbuzi katika gunia.

Hii Chadema itaongoza vipi? kwa hizo ahadi za Lowassa! mtu hatangazi hata sera za Chadema isipokuwa it's all about him, leo anatuhakikishia kwamba Mkataba wa Richmond ulikuwa safi kabisa na kusema ilikuwa kosa kufuatilia kesi hiyo ilitugharimu millioni mia moja na sijui ngapi, wakati leo inatugharimu zaidi ya hicho karibu kila mwezi na umeme bado hautoshelezi!

Huyu kweli ni mtu wa kumpa nafasi kubwa azungumze uongo kwa niaba yenu kwamba haoni kama kulikuwa na makosa yalipofanyika ilihali watu wote tunaamini yalikuwa makosa!. Huyu huyu leo anadai ati alitaka kuuvunja mkataba na kwa ushahidi gani? tumuamini tu leo hii. Richmond - shirika la kitapeli la uchapishaji Houston, owner wake mhindi tumekua naye Gerezani na address ya Rostam iwe mkataba safi kabisa ulosifika ha Obama na Mama Clinton sijui baada ya kuuziwa Symbion! Lini rais wa Marekani akaingilia biashara za mashirika hata kutamka maneno kama hayo!. Huu ni uongo ulopitikliza!

Sisi tunaoishi nchi hizi tunajua fika rais wa nchi hawezi kabisa kusema maneno hayo ktk mikataba ya mashirika isimhusu na kama unakumbuka Waziri mkuu wa Canada Harper alipokuja Dar aliombwa kutusaidia juu ya Mkataba wetu na Barricks! Na akasema yeye hana mamlaka hayo maadam tumeshafunga mkataba tukajadili na wawekezaji! Leo Lowassa anaudanganya Umma kwamba Obama alisifia mitambo ya Richmond na maneno haya anayasema kwa tiketi ya Chadema (UKAWA) mnakubali tu!..

Mnasikitisha sana ndugu zangu, sijui haya mageuzi yenu yanalenga kugeuzwa kwa chapati ili iive pande zote mbili..

Mkaandara umesema yoote sina la kuongeza ila unawaambia watu ambao masikio yao yameshazibwa na macho hayawezi kusoma chochote utakachoandika dhidi ya Lowasa. Kardinali pengo alituonya watanzania kua Hitler hakupindua ujerumani bali watu walimchagua kwa kujaribu sura mpya yaliyowakuta hawatadiriki tena. Wapinzani wa tanzania wote ni wasanii. Katiba iliyopo ni ya chama kimoja iliyojaa viraka vya kisanii vilivyopachikwa na ccm.. miaka 20 wapinzani wanaitafuta ikulu sijui wakafanye nini badala ya kujaza wabunge
Ningewasifu UKAWA kama wangemchukua Lowasa kama manager wao wa kampeni kukjza wabunge badala ya kumnadi aende ikulu. Atatengenezaje serikali miswada gani itapita na atawezaje kubadilisha katiba na wabunge wachache? Mimi napenda sana mageuzi lakini si haya ya kuchukua walioshindwa na kukimbilia ukawa. Lowasa angejiuzuru na kutueleza ukweli wa mikataba ya Richmond tungejua ni msafi lakini daima ukikaa kimya ni dalili ya kukubali tuhuma. Unapohojiwa na police unaambiwa umekamatwa kwa tuhuma fulani una uhuru kukaa kimya kila utakachosema kitapelekwa mahakamani kama ushahidi. Hii trick no comment inaweza ikakutokea puani maana wanasema ulikaa kimya kuangalia upepo. Kwa ujumla Lowasa hatufai. Wenzangu mtakaobahatika kupiga kura chagueni wabunge waadilifu bila kujali vyama si mifano tunayo ktk sakata la escrow na katiba mpya waliokuwa upande wa serikali wapigwe chini hawatufai. Mungu ibariki Tanzania
 
Wanachama wa UKAWA ni wale wananchi wa mijini na vijijini waliopigika kwa sera za CCM zilizoshindwa kuwaboreshea maisha yao, hivyo wakajikusanya chini ya UKAWA ili kujaribu kutafuta ahueni kwa kuiondoa CCM madarakani sawa na walalahoi wa Marekani walivyomchagua Obama na democrat wakijaribu kutafuta nafuu ya maisha yao.

Rungwe na wenzako mnaogombea urais kupitia vyama ambavyo havina hata diwani mmoja nchini mnajua kuwa hamtashinda, na sisi wananchi tunawaona nyie kama watu wenye nia ya kuisadia CCM ili iendelee kutubana wananchi kwa kuzigawana kura za upinzani wakati wa uchaguzi.

Tunakufahamu kuwa wewe ni mkurugenzi wa bahari motors pale Mwananyamala, hivyo sio mlalahoi kama sisi.

Lakini rasilimali ya watu wanyonge ni umoja wao, tutahamasishana wapenda UKAWA wote ili kuzisusia biashara zako zote na za wenzako sokoni ili muwe walalahoi kama sisi, lambda mtaelewa mateso yetu na juhudi halali tunazozichukua katika kujitafutia nafuu.
 
mbona huyu alisha sema ana muunga mkono lowasa muda tuu itv
 
Akina Dovutwa? 2010 huyu alitangaza kujitoa kisha akawataka wafuasi wake kura wampe jk
 
Wanachama wa UKAWA ni wale wananchi wa mijini na vijijini waliopigika kwa sera za CCM zilizoshindwa kuwaboreshea maisha yao, hivyo wakajikusanya chini ya UKAWA ili kujaribu kutafuta ahueni kwa kuiondoa CCM madarakani sawa na walalahoi wa Marekani walivyomchagua Obama na democrat wakijaribu kutafuta nafuu ya maisha yao. Rungwe na wenzako mnaogombea urais kupitia vyama ambavyo havina hata diwani mmoja nchini mnajua kuwa hamtashinda, na sisi wananchi tunawaona nyie kama watu wenye nia ya kuisadia CCM ili iendelee kutubana wananchi kwa kuzigawana kura za upinzani wakati wa uchaguzi. Tunakufahamu kuwa wewe ni mkurugenzi wa bahari motors pale Mwananyamala, hivyo sio mlalahoi kama sisi. Lakini rasilimali ya watu wanyonge ni umoja wao, tutahamasishana wapenda UKAWA wote ili kuzisusia biashara zako zote na za wenzako sokoni ili muwe walalahoi kama sisi, lambda mtaelewa mateso yetu na juhudi halali tunazozichukua katika kujitafutia nafuu.

kwani el na mega bite hawana biashara?
Kwa nn unataka kuutumia uhuru wa mtu mwingine?
Democracy na vikwazo vya biashara ni ubakaji!
 
Uvivu na ulalamikaji ndo sifa ya wabongo, chapa kazi kihalali uone kama utalalamika hivyo, endelea kulalamika uone kama ukawa watakuletea ugali
 
Back
Top Bottom