..sawa.
..lakini this time ccm lazima wapumzishwe.
..kama ni mtandao, sijui kitu gani, wacha tujaribu na chadema nao tuone uzuri au ubaya wao.
Mkuu tafadhali! hawa jamaa kumuunga mkono ama kumvhagua Lowassa wana maana ya kwamba kama CCM ingempitisha Lowassa basi wao wasingekuwa na pingamizi maana ndiye wanayetegemea kuleta mageuzi, sasa tujiulize ni mageuzi gani hayo? Na hawa CHAUMA wameonyesha wazi kwamba sio wamewaunga mkono UKAWA bali Lowassa na hivyo wangemuunga mkono hata kama angechaguliwa na CCM. Ndivyo kisiasa inavyotafsirika.
Kama UKAWA walikuwa na dawa dhidi ya Lowassa na walijiandaa vema dhidi ya Lowassa na mgombea wao ikiwa Lowassa atapitishwa na CCM, basi hizo ndizo sababu zingewafanya wasimchukue Lowassa kwani uchaguzi wa rais unatokana na sifa za mgombea sio Chama kwa ujumla. Mrema alifanya vizuri kwa sababu wananchi walimtazama yeye na sio NCCR na hata Dr. Slaa 2010 kama Chadema ingemsimamisha Mbowe bila shaka matokeo yangekuwa tofauti kabisa na ndio maana CDM wakampitisha Dr.Slaa.
Kwa hiyo unajaribu a Chadema kwa vipi kwani wananchi hawakuiona Chadema wakati wa Dr.Slaa ama Mbowe na kwa nini hawakuichagua ikiwa itikadi na sera zake ni zile zile!. Mkuu hatupo katika majaribisho, na wala hatuna wakati huo kwa sasa isipokuwa tumefungiwa kanya boya tukiamini kuna mbuzi katika gunia.
Hii Chadema itaongoza vipi? kwa hizo ahadi za Lowassa! mtu hatangazi hata sera za Chadema isipokuwa it's all about him, leo anatuhakikishia kwamba Mkataba wa Richmond ulikuwa safi kabisa na kusema ilikuwa kosa kufuatilia kesi hiyo ilitugharimu millioni mia moja na sijui ngapi, wakati leo inatugharimu zaidi ya hicho karibu kila mwezi na umeme bado hautoshelezi!
Huyu kweli ni mtu wa kumpa nafasi kubwa azungumze uongo kwa niaba yenu kwamba haoni kama kulikuwa na makosa yalipofanyika ilihali watu wote tunaamini yalikuwa makosa!. Huyu huyu leo anadai ati alitaka kuuvunja mkataba na kwa ushahidi gani? tumuamini tu leo hii. Richmond - shirika la kitapeli la uchapishaji Houston, owner wake mhindi tumekua naye Gerezani na address ya Rostam iwe mkataba safi kabisa ulosifika ha Obama na Mama Clinton sijui baada ya kuuziwa Symbion! Lini rais wa Marekani akaingilia biashara za mashirika hata kutamka maneno kama hayo!. Huu ni uongo ulopitikliza!
Sisi tunaoishi nchi hizi tunajua fika rais wa nchi hawezi kabisa kusema maneno hayo ktk mikataba ya mashirika isimhusu na kama unakumbuka Waziri mkuu wa Canada Harper alipokuja Dar aliombwa kutusaidia juu ya Mkataba wetu na Barricks! Na akasema yeye hana mamlaka hayo maadam tumeshafunga mkataba tukajadili na wawekezaji! Leo Lowassa anaudanganya Umma kwamba Obama alisifia mitambo ya Richmond na maneno haya anayasema kwa tiketi ya Chadema (UKAWA) mnakubali tu!..
Mnasikitisha sana ndugu zangu, sijui haya mageuzi yenu yanalenga kugeuzwa kwa chapati ili iive pande zote mbili..