*iPhone 15 Pro Max ina performance kubwa zaidi kupitia AnTuTu v10 benchmark, iPhone 15 Pro Max ina 1571000 score wakati hiyo Pixel 8 Pro ina 1141000 score. Inapitwa hata na 14 Pro kwenye performance
Google Pixel 8 Pro inatumia Google Tensor G3 (4nm) wakati 15 Pro Max ina Apple A17 Pro ambayo inafanya iPhone 15 Pro Max kuwa na performance kubwa kwa asilimia 38 zaidi ya Pixel 8 Pro
Benchmark zote zinaonesha Pixel imekalishwa parefu kuanzia GPU hadi CPU
*Hiyo display unayosema kuwa imeishinda iPhone ubora ni display ya Pixel ipi. Kama ni 8 Pro, basi Pixel 8 Pro imefanikiwa kushinda brightness simu zote kasoro iPhone 15 series.
*Kwenye ukaaji wa chaji huku Pixel ndio haigusi kabisa. Battery test za Google Pixel 8 Pro na iPhone 15 Pro Max zimefanywa na results zinajitosheleza. Soma hapa
GOOGLE PIXEL 8 PRO
Web browsing: 11hrs 6min
Watching videos: 15hrs 40min
Gaming: 4hrs 19min
Standby: 81hrs
General battery life: 30hrs 8min
IPHONE 15 PRO MAX
Web browsing: 17hrs 3min
Watching videos: 22hrs 31min
Gaming: 6hrs 42min
Standby: 154hrs
General battery life: 48hrs 25min
Hakuna sehemu hata moja ambayo Pixel katoboa mbele ya iPhone
*Speakers: iPhone 15 Pro Max ina Dolby Atmos, Pixel 8 Pro haina.
Na bado iPhone 15 Pro Max inawekewa uwezo wa kucheza games za Resident Evil Village, Resident Evil 4 Remake na Assassin's Creed Mirage mwaka huu (2024) kama tu unavyocheza kwenye PS bila kubadili chochote
Flagship za Apple ziko vizuri kushinda Pixel, kinachokuja kutofautisha unachohitaji ni software tu, aidha unataka Android au iOS ila kwa sehemu nyingine nyingi iPhone zipo vizuri
Halafu kwenye kamera kiujumla, Google Pixel 8 Pro inapitwa na iPhone 15 Pro Max. Angalia comparison mbalimbali mfano anza na hii [emoji116][emoji116]
View: https://youtu.be/RyVitycWTZU?si=NAa4TDVOM9XfSF5e