Mauzo ya Apple nchini China yameshuka kwa asilimia 30, na yanatarajiwa kuendelea kushuka mwaka huu wa 2024

Reuben Challe

JF-Expert Member
Dec 10, 2021
2,761
5,039
Mauzo ya simu za Apple nchini China yameshuka na dalili zinaonesha yataendelea kushuka mwaka huu wa 2024, kwa mujibu wa utafiti wa Jefferies.
Mauzo ya iPhone 15 series hayakuwa mazuri tangu mwanzo, na hii imepelekea mauzo ya Apple yashuke kwa 30%
Screenshot_2024-01-08-12-37-58-699_com.gsmarena.android.jpg

Upande mwingine mauzo ya Huawei yamekuwa kwa asilimia kubwa sana na hii ni kwa sababu ya Huawei Mate 60 series ambazo zimepata mafanikio makubwa mno nchini humo
1694149013_huawei-mate-60-pro-1.jpg

Uzinduzi wa iPhone 15 series ulifanyika wiki mbili tu baada ya kuzinduliwa kwa Huawei Mate 60 series. Utafiti wa Jefferies unadai kwamba uzalendo wa Wachina wengi ndio umepelekea watu wengi wahamasike kununua hizi flagship za Huawei zenye chipset ambayo imetengenezwa nyumbani kwao hapohapo (Huawei Kirin 9000S) ambazo tayari zimeshatolewa details za kutosha na kampuni yenyewe

Jefferies inakadiria kuwa Huawei wameuza takribani simu milioni 35 ambazo inasadikika wangeuza nyingi zaidi kama kusingekuwa na shortage of supply.
Screenshot_2024-01-08-12-58-44-609_com.gsmarena.android.jpg

Kushuka huku kwa asilimia 30 za mauzo ya Apple kunatarajiwa kuendelea zaidi mwaka huu. Deals kibao za kupata iPhones kwa bei za chini nchini China zimeonekana sehemu nyingi mitandaoni wiki iliyopita. Lakini licha ya bei rahisi za simu hizi bado mauzo yao hayaja-improve
 
Hizi simu wachina wanazipotezea sema Hawa wachina simu zao ni balaa sana ndo maana apple hazina soko china
Usiseme Apple hazina soko China, unakosea mkuu

Apple ni kampuni ya pili kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi nchini China. Kwa mauzo ya simu China, Apple anazidiwa na Huawei tu tena amezidiwa kwa chini ya asilimia 1 tu

Smartphone market share ya China ipo hivi.
1. Huawei 23.4%
2. Apple 22.44%
3. Other brands 21.09%
4. Xiaomi 12.91%
5. Vivo 5.96%
6. Oppo 4.65%
Screenshot_2024-01-08-13-28-59-275_com.android.chrome.jpg
 
Na BYD quater hii imezidiwa unit 3000 tu na tesla ambapo inatabiriwa quater ijayo BYD atakuwa amempita tesla
 
Mkuu haiingii akilini kulazimishwa na serikali kununua simu usiyoipenda. We hayo mambo umetolea wapi

Well inawezekana sana, hasa kwa serikali kama ya china. Kama waliweza kupiga marufuku social medias za west na kuweka adhabu ukipatikana unatumia social media za west.

Why washindwe hili?
 
Well inawezekana sana, hasa kwa serikali kama ya china. Kama waliweza kupiga marufuku social medias za west na kuweka adhabu ukipatikana unatumia social media za west.

Why washindwe hili?
Kwa hiyo Mchina akishuka kimauzo, ni kwa sababu simu zao ni feki
Ila Apple akishuka kimauzo, serikali ya China inalazimisha watu wake wanunue simu za China. Si ndio?
 
IPhone tatizo wana limitations za kiwakii, ndo maana sie wengine tunaziacha, siku wakitoa hizo limitations zao, bas naishi nayoo.
 
IPhone tatizo wana limitations za kiwakii, ndo maana sie wengine tunaziacha, siku wakitoa hizo limitations zao, bas naishi nayoo.
kabisa halafu simu zao zina specifications zakawaida sana alafu bei zakiboya,
 
Hebu acha zako mkuu 😂😂
Kwa hiyo unataka kusema iPhone ni poor quality au, hizi ni dharau kiwango cha lami😅😅
Napotaja Quality sina maana ya ku refer lile li housing la nje

Quality nayoisema mimi ni ukubwa wa specifications na ubora wake.

Sasa unatoa mamilioni ya pesa kununua simu halafu unakuja kuwa limited kwenye customization, ndio nini sasa?

Una simu ya milioni 2 halafu ku-download clip ya dakika 2 YouTube ni mpaka uombe tag kwa android user aku downlodie ndio akutumie kwa WhatsApp

Karne hii na tech yote hii eti simu ya 50K inapakua video YouTube lakini iPhone ya milioni mbili haiwezi kupakua video YouTube mpaka uwe na premium subscription?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom