Walichoiga Apple toka Android mwaka 2023

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Android ni moja wapo wa Os wenye nguvu sana ulimwenguni kutokana jinsi walivyoweza kufanya simu ionekane nyepesi kutumika na Kila moja wetu.

Turudi kwenye uzi wetu unajua apple wameiga baadhi ya feature Toka Android
Ebu Fanya kwanza usisahau kutu follow si unajua Teknolojia ni Yetu sote Kisha like .

Ni mwaka mwingine Tena apple wameachia series mpya ya iOS 17 kwenye vifaa mbalimbali simu , kompyuta pamoja na ipad.

Leo nakuletea baadhi ya feature ambazo zipo kwenye iOS 17 zimeigwa Toka Android.

1) live voicemail
Ni feature ambayo Google walikua watu wa mwanzo kuachia kwenye simu za Google pixels inaitwa live voicemail kipengele cha ujumbe wa sauti unaotokea kwenye simu yako wakati mtu amekupigia simu ujapokea.

Utaweza kuona ujumbe wa maneno unaotokea kwenye simu yako ambao utakau recorded ivyo utaweza kusoma na kuamua kama utampigia au lah.

2) Name-drop
Ni feature ambayo inakusaidia kuweza ku share taarifa za namba yako ya simu na mtu mwingine bila kubadilishana simu kwa njia ya kugusanisha tu simu mbili.

Hii feature ilikuwepo kwenye android version 10 ila kitu kibaya zaidi ni kuwa kwenye android version 14 imeondolewa
ilikuwa inaitwa android beam.

Google wamekuja feature mpya inaitwa Google nearby ambayo utaweza kuhamisha file,picha, videos docs nk.

3) apple maps
Watumiaji wa ios ilikua haiwezekani kabisa kupakua Google maps na kutumia offline jambo ambalo Google waliweka hii feature kwenye simu za android miaka 10 iliyopita hatimaye apple wameweka feature ya kuweza kupakua Google maps na kutumia offline kwenye Mazingira ambayo akuna mtandao.

4) Gboard predictive Text first
Kubadilishi maneno inawezekana ni kitu ulikua unapenda au lah lakini ilikuwepo kwenye simu za android kitambo kupitia Gboard kuweza kukusaidia kupunguza kuandika ujumbe mrefu mrefu kupitia simu yako.

kwaiyo apple pia wamekuja feature ya ku predictive ujumbe kwenye keyboard kupunguza kuandika ujumbe mrefu mrefu Kila mara kwenye iOS 17.

5) keep private tabs
Hii ni feature nyingine apple wameiga Toka Android Toka kwenye iOS 17 ni iOS mpya. Google waliweza kuweka hi feature mda kuweza kuzuia baadhi ya folder kwenye browser kushindwa kufunguliwa mpaka kupitia lock either fingerprint au password hatimaye iOS 17 utaikuta.

Hakika Teknolojia ni Yetu sote au unasemaje tuachie maoni yako ?

images.jpg
download.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom