Niambie maana ya On paper ni nini mzee
Google Pixel 8 Pro on paper wanasema inafikia peak brightness ya 2400nits, iPhone 15 Pro Max ni 2000nits
Lakini gsmarena wametest wamekuta Google Pixel 8 Pro inafikia 1600nits tu, iPhone 15 Pro Max anafikia hadi 1800 huko.
Hapo nani anadanganya on paper??
Kwenye kamera unaanzaje kusema iPhone ni video tu? Basi na mimi nasema Pixel ni picha tu kwingine majanga. Itakuwa sahihi kusema hivyo?
Hiyo video ya camera comparison niliyokuwekea umejisumbua hata kuiangalia? Kamera overall ni kuanzia main camera, ultrawide camera, telephoto lens, selfie camera na kuna mengi sana ya kutest ukiondoa hizo video na picha za kupoint na kushoot. Nimekuwekea hiyo video ili uone maana on paper Pixel 8 Pro ina camera specs nzuri kuliko iPhone ila kwenye kuzitest iPhone inaperform better kuliko Pixel 8 Pro. Again nani anadanganya on paper?
Kuhusu battery life, hizo sio results za On paper. Pixel 8 Pro ina 5050mAh on paper na iPhone 15 Pro Max ina around 4000mAh ila bado inatunza chaji parefu kushinda Pixel 8 Pro. Pixel 8 Pro ina utunzaji wa chaji mbovu ukifananisha na iPhone 15 Pro Max. Hii sio on paper mzee. Gsmarena wametest, kasome review Acha ubishi
Hapa pia, nani kadanganya on paper?
Kwenye performance Google Pixel 8 Pro imeachwa mbali na iPhone 15 Pro Max kuanzia on paper hadi in real life. Tests zimefanywa kaangalie. Gsmarena wamethibitisha, Pixel 8 Pro inazidiwa performance hadi na Qualcomm Snapdragon 8+ Gen 1 ambayo hii imetumika kwenye Xiaomi 12S Ultra. Kama Xiaomi 12S Ultra inazidi Pixel 8 Pro kwenye performance, sembuse iPhone 15 Pro Max?
Acha kusema neno "ON PAPER" kama hujui maana yake badala yake kafanye utafiti kwanza ndio uje kutetea unachokisema kwa data