BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Apple inalazimika kuruhusu watumiaji wa iPhone kuwa na uwezo wa kuweka app bila kutumia App Store ya Apple. Mabadiliko haya yatawezesha watumiaji wa iPhone ku-install app yoyote nje ya App Store.
๐ฒ ๐๐ฌ๐ ๐ ๐๐ฌ๐๐๐๐, ukiwa unataka kuweka app kwenye simu ya iPhone, unalazimika kwenda katika App Store. Sehemu ya App Store - ni stoo maalum ambayo inakuwa na apps zote ambazo Apple imezihakiki na kujiridhisha kuwa zinafaa kwa matumizi, pia ni sehemu ambayo Apple inaitumia ili kupata faida kwa sababu inachukua asilimia 30% ya faida inayopatikana katika malipo na manunuzi ndani ya apps zake.
Developers wa Apple wameanza kufanyia kazi mabadiliko mapya ya kuruhusu Third-party app store kuanzia katika mfumo wa iOS 17 na kuendelea.
๐ ๐๐๐๐๐๐๐ก๐๐ ๐ค ๐ข๐๐ฅ๐ฎ๐ ๐ฎ๐๐ฉ๐๐ ๐ช๐ฌ๐๐๐?
Mabadiliko haya yakianza rasmi, itakuwa ni rahisi kwa watumiaji wa iPhone kuweka apps ambazo zinapatikana nje ya App Store. Na mabadiliko haya hayatakwepo katika iPhone tu; Apple itabadili utaratibu wake wa kufungia app hata katika Macs na vifaa vingine vya Apple.
Kwa watumiaji wa Android tangu zamani wana uhuru wa ku-install app bila kutumia Google Play Store. Na hii imerahisisha watu kuweka app kama vile Netflix Premium ambayo sio ya kulipia, WhatsApp GB, apps ambazo zimefanyiwa mabadiliko na modifications nje ya app official, mfano hata Spotify kuna watumiaji wengi wanatumia Premium ambayo unaipata nje ya official app ya Spotify.
โ๏ธ ๐๐ฌ๐๐ฃ๐๐ฃ๐ ๐ผ๐ฅ๐ฅ๐ก๐ ๐๐ฃ๐๐๐๐๐๐ก๐ ๐ช๐ฉ๐๐ง๐๐ฉ๐๐๐ช ๐ฌ๐๐ ๐?
Apple imelazimika kufanya mabadiliko hayo baada ya Umoja wa Nchi za Ulaya kuweka sheria kuwa mwaka 2024 kampuni za tech ziruhusu store za app nyingine ndani ya mifumo yao. Hii ni kuruhusu ushindani na kupunguza utaratibu wa makampuni ya tech kushikilia power kubwa ya kuamua app zipi zizuiliwe kwenye simu.
๐ต ๐๐๐๐๐๐ง๐ ๐ฎ๐๐ ๐
Apple imetishia kwa kusema kuwa; mabadiliko haya yakianza ndio MWISHO WA USALAMA WA MIFUMO YAKE. Apple imesema mabadiliko haya yataathiri mfumo wa usalama katika mifumo ya simu na kompyuta.
SwahiliTek