Kitomai
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 1,061
- 281
*
Wananchi wenye hasira wamemuua na kumchoma moto kijana mmoja aliyetuhumiwa kuiba piki piki, . Tukio hilo limetokea katika eneo la kimara Mwisho pembezoni mwa barabara iendayo Morogoro mita takribani 200 kutoka katika kituo kidogo cha Polisi cha kimara Matangini leo tarehe 21/8/2010 majira ya saa tano asubuhi. Mpaka habari hizi zinarushwa hewani jina la kijana huyo lilikuwa bado halijatambulika
Kwa mujibu wa mashuhuda, kijana huyo aliwasili katika eneo la Kimara king'ongo na kuiba piki piki kisha kuondoka nayo akiwa anaelekea maeneo ya Ubungo. Alipofika karibu na maeneo ya Resort akaishiwa mafuta ndipo alipoamua kuweka mafuta katika kituo kilichopo eneo hilo. Wakati akifanya hayo yote, walioibiwa walikua wakimfuatilia hatimaye wakamkuta ameshaweka mafuta na sasa anaondoka ndipo walipomkamata na kurudi naye kimara mwisho, kimara king'ongo.
Walipofika hapo wakajivisha majukumu ya uendesha mashitaka, uhakimu, hatimaye wakatoa adhabu ya hukumu ya kifo kwa kipigo, kwa kupondwa mawe hatimaye kumchoma moto mpaka alipopatikana na mauti. Polisi ambao walikuwa karibu na tukio hilo walizidiwa nguvu na raia hao wenye hasira kali, mpaka hapo baadaye kilipokuja kikosi maalumu cha kupambana na fujo, kikosi hicho kilifika wakati wauaji wameshatekeleza hukumu ya kifo.
Kunradhi nimembatanisha picha ambazo siyo nzuri lakini imebidi nifanye hivyo kwa sababu sina jinsi nyingine ya kukuelezea tukio hilo.
MAONI.
Piki piki ya kichina ina thamani gani mpaka kutoa uhai wa mtu wenye thamani kubwa isiyolingana hata kidogo na chombo cha usafiri? Kwa nini jamii inakosa subira kiasi hicho? Kumbuka huyo alituhumiwa tu, alikua mtuhumiwa, akupewa nafasi kukata rufaa! Inakuaje wananchi hao hao wanaendelea kuwatazama bila kuwagusa kwa kidole watuhumiwa wenye dhamana kubwa za uongozi ambao wanatuhumiwa kuiba mamilioni ya fedha? Nini maana yake hii, tuseme tumekosa upendo? Basi nimejiuliza maswali mengi sijapata majibu, wewe je mwana Jf huna maoni gani?
Attachments
-
PIC00250.JPG45.2 KB · Views: 188
-
PIC00251.JPG45.1 KB · Views: 188
-
PIC00236.JPG48.3 KB · Views: 180
-
PIC00240.JPG45.2 KB · Views: 171
-
PIC00246.JPG47.2 KB · Views: 180
-
PIC00237.JPG37.5 KB · Views: 149
-
PIC00249.JPG45.7 KB · Views: 146
-
PIC00243.JPG47.9 KB · Views: 156
-
PIC00247.JPG46 KB · Views: 193