Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,492
- 7,961
Naona Serikali imeanza kupita mitaani kuwasikiliza wanaoisema vibaya, Jamal Mikome mkazi wa Chanika amefikishwa mahakama ya Kisutu kwa madai ya kuitukana Serikali wakati akitoa povu kuhusu Deni la Taifa na kuinyima kura Serikali mwaka 2025.
Kwani wasipite pia kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mkataba wa bandari kama wanayo 'manpower' ya kutusikiliza mitaani?
========
Mkazi wa Chanika, Jamal Mikome (48) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka moja la kutumia lugha ya matusi kuitukana Serikali iliyopoko madaraka.
Mikome, ambaye ni mfanyabiashara, alifikishwa mahakamani hapo, leo Jumatatu Juni 19, 2023 na kusomewa shtaka lake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Neema Moshi akishirikiana na Erick Kamala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio.
Wakili Mosha amedai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya jinai namba 104/2023.
Akisomewa shtaka hilo, Wakili Moshi amedai mshitakiwa alitenda kosa hilo Aprili 28, 2023 eneo la Chanika, Wilaya ya Ilala.
Inadaiwa siku hiyo ya tukio na eneo hilo, alitumia lugha ya matusi kwa kuitukana Serikali iliyoko madaraka.
Mwananchi