Anywa sumu baada ya kunyimwa Penzi

Anywa sumu baada ya kunyimwa Penzi

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,944
Reaction score
4,511
UPO usemi usemao kuwa mapenzi ni sumu na mapenzi yanaua ni usemi ambao ni vigumu kuuelewa ila ni rahisi sana kuutumia usemi huu kama ni funzo kwa wasiojua nini maana ya mapenzi.

Kwa wakazi wa eneo la Pawaga Road mjini Iringa usiku huu wamepata kuhusudia tikio la aina yake kutoka kwa kijana Kevin Swale (20) mkazi wa Njombe ambae amelazimika kunywa sumu kwa lengo la kujiua baada ya kunyimwa penzi na msichana mmoja mkazi wa eneo hilo aliyemtaja kwa jina la Tunu ambae pia ni mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne mwaka jana.
Tukio hili la aina yake kuelekea siku ya wapendanao duniani limetokea leo jumanne mida ya saa 4 usiku katika eneo la barabara ya Pawaga Road jirani na ofisi za shirika la Nyumba Tanzania.
Mashuhuda wa tukio hilo waliueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com uliofika eneo la tukio kuwa kijana huyo alikutwa akiwa hajitambui huku akiwa amelala katika mtaro wa maji machafu na mkononi akiwa ameshika pipi ya kijiti yenye rangi nyekundu mithiri ya siku ya wapendanao huku akiwa na sumu ya Panya na machi nyenye rangi ya kijani ambayo yalikuwemo katika chupa za maji ya kunywa ambayo kwa kawaida huuza kati ya Tsh 500 hadi 600.


kijana Kevini Swale akiwa amepoteza fahamu baada ya kunywa sumu ,huku mkononi akiwa ameshika pipi ya upendo kwa mpenzi wake ,pembeni kukiwa na ujumbe aliotaka kuuacha ,sumu ya panya na maji

Mbali ya kukutwa na sumu na maji hayo ambayo pia yanasadikika kuwa ni sumu pia kijana huyo alikuwa na kisu kilichofungwa katika karatasi nyeupe kilichoandikwa kwa wino na kalamu ya blue maandishi yanayosomeka kuwa LAZIMA UFE LEO.

Hata hivyo kando la mwili wa kijana huyo ambae alikuwa akipumua kwa mbali kulikuwa na daftari lililoandikwa kama kurasa 15 zenye jumbe mbali mbali kwa wapenzi wake ,ndugu na jamaa pamoja na Historia ya maisha yake toka alipozaliwa hadi leo alipoamua kukatisha maisha yake.



Hapa kijana Kevini akinywa dripu baada ya kufikishwa Hospitali


Miongoni mwa warembo waliotajwa katika maandishi hayo ni pamoja na Nuru Mlowe wa Ilembula ,Lucy wa Dar es Salaam ,Anna wa Moshi,Shangazi Solina wa Kilimanjaro ,James Swale wa Njombe ,Jack wa Tanga,mama Tunu wa Semtema,Elina wa Miyomboni ,MAGE wa POSTA ,FARIDA WA MBEYA na wengine wengi pamoja na ujumbe kwa mpenzi wake TUNU ambao unasomeka kuwa TUNU SIAMINI KAMA WEWE NDIO CHANZO CHA KIFO CHANGU KWANI MNENO MTAMU ULIYOKUWA UNANPA TUKIWA TANGA?na mwisho kila ujumbe aliouandika aliweka sahihi yake.
Kijana huyo katika ujumbe wake wa maandishi alisema kuwa ameamua kujiua baada ya kutoswa na pia tatizo la ugonjwa wa kansa na ugonjwa mwingine unaomsumbua ambao hakuutaja katika maandishi yake.
Hata hivyo tukio hilo lilionyesha kuwavuta watu wengi na baadhi yao kujiuliza TUPO WANGAPI? Kwani idadi ya warembo waliotajwa ilikuwa ni ndefu na si rahisi kuimaliza kwa haraka huku wakitaka vijana kuepuka kuchukua uamuzi wa kujiua kwa kitu mapenzi.

Wananchi wakimtazama kijana huyo aliyezima kwa kunywa sumu kisha kunyimwa penzi

Baadhi ya warembo waliofika kushuhudia tukio hilo walisema kuwa hata kama kijana huyo ametoswa na wapenzi wake dawa haikuwa hiyo ya kujiua alipaswa kutafuta mwingine ama wengine
Jitihada za kuokoa maisha ya kijana huyo zilizaa matanda baada ya wasamaria wema pamoja na askari wa Doria kufika eneo hilo na kumkimbiza kijana huyo katika Hospitali ya mkoa ambako alipewa maji ya Dripu mbili na kuyanywa na kabla ya kupata nafuu na kutaja jina lake na kuwa yeye ni mkazi wa Dar es Salaam aliyefika Njombe kufuata mpenzi wake aliyemaliza kidato cha nne na kuelezwa kuwa yupo Iringa na baada ya kumfuata mrembo huyo alianza kumzingua na yeye kuchukua uamuzi huo.


Hata hivyo alidai kwa upande wake alikula keki yenye sumu na sio alikunywa sumu hiyo japo alipoulizwa kuhusu ujumbe wa maandishi alioacha katika daftari hilo na mwingine kujichora mkononi alisema kuwa alifanya hivyo kama njia ya
​
kujiandaa kwa kifo.
“Ndugu zangu mimi mwenzenu ninatatizo la kupoteza fahamu kila ninapomkumbuka mpenzi wangu hivyo si mara ya kwanza kuanguka ni mara nyingi nikimuwazo Tunu huwa nazimia “
Hadi tunakwenda mitamboni mida ya saa 5 usiku kijana huyo alikuwa katika chumba cha Daktari wa Hospitali ya mkoa wa Iringa huku nje ulinzi wa polisi ukiwa umetanda kwa ajili ya kumchukulia hatua zaidi ya kutaka kujiua .

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
​
 
Msanii tu huyo wanaotaka kufa huwa hawarembi hivo
 
jamani tunu c umpe mwenzio tundi,alibip kifo cheki anavyofakamia drip hahaaa,chezea Israel mtoa roho,atakua kamuona lucifer live akiwa anjiandaa kumpokea!
 
Chezea mapenzi...Suluhu yake sio afiki ila naamini ataanza vyema safari nyingine ya mapenzi. Ila hapo akimkumbuka anazimia hii ni new to my brain. Thanks hakufa nisingejua haya.
 
Hili nalo bw.e.g.e kweli wenzie enzi zetu tulikua tunachukua picha, tunaitumia kule bafuni....unatoka mwepesii! then u call it a day
 
jamani tunu c umpe mwenzio tundi,alibip kifo cheki anavyofakamia drip hahaaa,chezea Israel mtoa roho,atakua kamuona lucifer live akiwa anjiandaa kumpokea!

:becky::becky: tatizo Tunu ni denti anataka akamua kwanza masomo
 
me wananiudhi wanaojifanya kutaka kufa, hadi uwape watu habari jamani, hebu tukue fanya mambo yako kimyakimya tutakuja ona mzoga , ya nini utusumbue tukupeleke hospitali, mnakera nyie
 
mh!usikute walishakulana sasa tunu kapata bf mwingine kamtema jamaa!

"Ndugu zangu mimi mwenzenu ninatatizo la kupoteza fahamu kila ninapomkumbuka mpenzi wangu hivyo si mara ya kwanza kuanguka ni mara nyingi nikimuwazo Tunu huwa nazimia"

umeona nukuu hiyo mama lao?
 
Back
Top Bottom