Ajinyonga baada ya mume wake kumnyima nauli ya kwenda Singida

carbohydates

Senior Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
124
Reaction score
210
Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Jasmini Hamisi, mkazi wa Mtaa wa Murieti, Kata ya Murieti jijini Arusha, amefariki dunia baada ya kudaiwa kunywa kimiminika kinachohisiwa kuwa sumu na baadaye kukutwa akiwa amejinyonga ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe.

Tukio hilo limetokea Oktoba 18, 2026, siku moja baada ya taarifa kueleza kuwa Jasmini alimwomba mumewe, Hamisi Maulidi, nauli ya kwenda mkoani Singida kuwasalimia wazazi wake, lakini akaambiwa asubiri hadi hali ya kifedha itakapokuwa nzuri.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa kuhusu tukio hilo, Hamisi aliondoka nyumbani asubuhi kwenda kazini, Aliporejea na kugonga mlango bila kupata majibu, alimwita jirani kumsaidia. Jirani huyo alipozunguka nyuma ya nyumba na kuchungulia kupitia dirishani, alimwona Jasmini akiwa amejinyonga kwa kutumia mtandio aliokuwa ameufunga kwenye chuma cha kutundikia pazia.

Mtoto mdogo aliingizwa ndani kupitia dirishani ili kufungua mlango. Walipoingia, walimkuta Jasmini akiwa bado anapumua kwa shida na kufanya jitihada za kumpeleka hospitalini, hata hivyo, alifariki dunia. Majirani walieleza kuwa walikata mtandio huo kwa haraka wakijaribu kumuokoa.

Aidha, inadaiwa kuwa ndani ya nyumba hiyo kulionekana kikombe chenye kimiminika kisichojulikana, huku soda ikiwa pembeni. Hata hivyo, haijathibitishwa iwapo kimiminika hicho kilikuwa sumu.

Mpaka sasa, chanzo rasmi cha kifo cha Jasmini hakijafahamika, na hakuna uthibitisho kuwa ombi la nauli ya kwenda Singida lilikuwa na uhusiano na tukio hilo. Maelezo haya tunahitaji kuthibitisha na mamlaka husika kabla ya kuhitimisha mazingira ya kifo chake.

Chanzo: Mwendokasi Tv

Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Jasmini Hamisi, mkazi wa Mtaa wa Murieti, Kata ya Murieti ji.jpg
 
R.I.P Jasmin🌹
 
Kuna binti wa kiislamu jirani hapa…kutwa kulia lia…jamani tusomeshe watoto wapate vibarua wajitegemee…pesa ya mwanaume ni utumwa

Kwan hawezi kufanya Kaz ya mama ntilie .

Ukifanya kazi ya chini ndipo utapata kazi nyingine.

Mbona mabinti wengi Drs vii lakin wanafanya Kaz ambazo wanakidhi mahitaji Yao.
 
Back
Top Bottom