ANTONY DIALLO ni ROLE MODEL kwa wamiliki wa vyombo vya habari

Nov 11, 2008
782
38
Kwa muda fulani nilikiuwa naangalia mwenendo wa wamiliki wa vyombo vya habari wanavyotumia au vyombo vinavyowatumia na pia naangalia malalamiko yanayohusu wamiliki wa vyombo vya habari.

Sikumbuki ni malalamiko gani yamelengwa kwa Mh. Antony Diallo anayesemekana kumiliki Star Tv na Radio Free Africa etc.

Nadhani huyu anaweza kuwa ROLE MODEL.....
Wadau mnasemaje kuhusu hili????
 
Last edited:
Ukweli hajageuza vyombo vyake kumtukuza lakini la kutoa uhuru maslahi ya wafanyakazi hilo ni la kitafiti zaidi
 
tena kanikuna sana alivyoichachafya bajeti ya MIUNDO MBINU, hao ndio wabunge wanaotakiwa, sio wengine wakishatolewa kwenye uwaziri basi ni usingizi kwa kwenda mbele wakati wa bunge session.....
 
wewe kandambilimbili mchokonoaji wa majungu.Unataka kusema nini hasa na unataka ulinganinshe na nani na kwanini haswa.Wewe nadahani ungekuwa na chombo cha habari ungekuwa unajitukuza kuliko unaotaka kuwalenga ila kwa vile mwenzangu uko hoi ndo maana unataka kuchokonoa wengine na kuwasifu wengine
 
Jamani kuna watu watakuja hapa na vizingiti lakini kwa vile hajagusa mtu mmoja mmoja najua watabaki kimyaa tu kama kawaida yao. Lakini jamaa kiboko amemuwamba Shukuru Kawamba hehehe safi sana mkuu lakini mbona kwenye ufisadi hupigi kelele na wewe unaogopa kunyoshewa kidole nini mkulu?
 
Teh teehh teeehh
wakati yeye akiwa waziri alithubutu kumnyooshea kidole waziri yoyote? au ni kutoelewana kwa wawili hawa? na ikumbukwe alipania tokea kkao cha kwanza cha kamati ya bunge walipopitia `FIRST DRAFT` au ndo yaleyale ya next election???? NAWAKILISHA!
 
Nadhan ulimaanisha kuwasilisha,siyo kuwakilisha,ebu tujaribu kutumia kiswahili fasaha.

Dialo si lolote si chochote kwani alipokuwa bosi wa wizara ya Maliasili na utalii aliendesha operation ya kuondoa wavuvi haramu lakini alipozama na bot akielekea ukerewe aliokolewa na wavuvi hao hao.

msimamo wake ni kwa kulipiza kisasi baada ya kutemwa katika cabinet ya JK inagawa hoja yake ni ya msingi lakini kwa nini sasa hivi.
 
Sidhani kama Diallo ni role model kwa wamiliki wa vyombo vya habari. Vyombo vyake vilitumika sana kupigia debe chama kimoja tu kwenye uchaguzi wa jimbo la Busanda.

Suala la kuendesha operation dhidi ya uvuvi haramu hilo lilikuwa moja ya majukumu ya wizara yake kwa hiyo kufanya hivyo ni sawa.

Suala la 'kulipiza kisasi baada ya kutemwa uwaziri' hiyo ni dhana tu ambayo nia yake kubwa ni kutaka wabunge, ambao ni wawakilishi wa wananchi wasihoji mambo yaliyokaa ndivyo sivyo (i.e. kuwanyamazisha wasihoji hata uozo) ili wasijeambiwa kuwa wanalipa kisasi kwa 'kutemwa uwaziri' au kwa 'kuukosa uwaziri'. That's an old and cheap argument.

kama ulivyosema mkuu, hoja ya Diallo ni ya msingi. Period.
 
Diallo ni mnyantuzu mjanja sijapata kuona!

Hoja.

Ona hii "Currently Active Users Viewing This Thread: 14 (3 members and 11 guests)"

Huo ni mfano.Fuatilia utagungua guests ni wengi kuliko members japo JF membership ni free,na ni immediate.

Sababu mojawapo ni kuwa watembeleaji wengi wanafuata hoja.Kusoma na kutafakari hoja na pengine kuchangia hoja ikibidi.

Sasa basi,jenga hoja mkuu.Hoja hoja.Kama vipi soma tuu,shukuru ukiikubali.

Mnyantuzu mjanja.So what?
 
Vile vile vyombo vyake vya habari vimekuwa vikitoa habari za uhakika na mpangilio mzuri wa vipindi.

Hongera bwana Diallo.
 
Ni hivi?

Mh. Diallo ana uwezo mkubwa sana wa kibiashara na wakisiasa, ni mtu makini mno anayejua mambo mengi sana.

Jamaa namwaminia na wakati mwingine anapiga kazi zaidi ya vijana wa kisasa, kama viongozi wote wangekuwa kama yeye tungekuwa mbali. kama vijana wangemuiga yule mheshimiwa tungekuwa mbali.

Sio mtu wa blabla...
 
Kwa muda fulani nilikiuwa naangalia mwenendo wa wamiliki wa vyombo vya habari wanavyotumia au vyombo vinavyowatumia na pia naangalia malalamiko yanayohusu wamiliki wa vyombo vya habari.

Sikumbuki ni malalamiko gani yamelengwa kwa Mh. Antony Diallo anayesemekana kumiliki Star Tv na Radio Free Africa etc.

Nadhani huyu anaweza kuwa ROLE MODEL.....
Wadau mnasemaje kuhusu hili????

YES! Nampa Big UP.
 
Uliyeanzisha thread hii ulifanya utafiti kwanza?
Kama ulifanya utafiti ni hivi. Wakati wa uchaguzi Busanda vyombo vyake vya habari vilikuwa biased vikitangaza habari za upande mmoja tu. Upande wa Sisi Maf.....
Wale wanaosikiliza radio hii walielewa.
 
Back
Top Bottom