Ansbert Ngurumo: Kikao cha siri ofisini kwa DCI kiliamua Mbowe na Wenzake wapelekwe mahakamani Jumanne wanyimwe dhamana

Hii nchi imewekwa rehani yaani wanakaa vikao vya siri alafu siri zinavuja kibwege tu ndio maana yule PK anamburuza bwana yuleee maana ashaujua uwezo wake.
Pole kwa wote waliokutwa na kadhia hii Mungu awafanyie wepesi inshaallah ipo siku moja tu tutasema na hili limepita pia.
hatari sana
 
Ansbert Ngurumo ni mwongo. Yaani unataka kutuaminisha kuwa Chadema's political goal end ni April 26? Serious!
 
Ni kama bado nipo gizani vile.
Ivi story ya maandamano bado ipo kwenye vichwa vya watu.
 
Kuna watu utafikiri wenyewe wana sehemu nyingine ya kukimbilia. Kumbe watakaoteseka hasa ni mama zetu, dada zetu na watoto wetu. Nilikuwa Congo mwaka juzi. Niliyoyaona kule yanatisha. Ee Mungu kikombe hiki na kiipite nchi yangu niipendayo. Mungu Ibariki Tanzania

Mkuu kama unayafahamu hayo waambia basi hawa wahusika waache kuminya demokrasia, waache kuasisi mipango ya watu wasiojulikana, ya utekaji, utesaji na uuaji. Waruhusu mchakato wa rasimu ya katiba pendekezwa ya wananchi, waruhusu mikutano ya kisiasa, na bunge live. Wakiyafanya hayo hayatatukuta ya Congo.
 
Jiulizeni kwanini Lowassa na Sumaye hawasumbuliwi? huenda mnapaswa kutupa kipande cha nyama kinachotoa harufu kwenye mabegi yenu mliyobeba.

Mambo yanayotokea sio ya kawaida kwa chama chenye wanachama na wafuasi wengi kama chwadwema na kafu. Kwa vyovyote vile hawa wazee wetu hawakupaswa kufanya hiki wanachokifanya wakati vyama na ukawa vikizidi kupukusuliwa meno yao kila siku.

Tulipaswa kuwaona angalau wakisema, kushauri na kuonya juu ya mambo mbalimbali ili amani abakie pahala pake.
 
Ni anahisi kuwa ni raisi wa Tanzania, anataka kutuletea maendeleo - Kama viongozi wa nchi zilizo endelea ambao hawakuishi milele. Hivyo usitumie kuishi milele kumkatisha tamaa raisi wetu. Je maraisi Amerika wameishi milele? ni raisi gani mzuri aliye wahi kuishi milele? Je wewe utaishi milele? Kwa hiyo unataka aiuze nchi yetu kwa sababu hataishi milele!
Maendeleo bila kuua, kupiga, kuwafunga wanaokukosoa hayawezi kuja? Viwanda vinafungwa, vinapunguza wafanyakazi, biashara zinafungwa kwa roho mbaya toka juu kuwapa maelekezo TRA kuongeza kodi ili zifungwe atimize azma yake ya watu kuishi kama mashetani.
Walioendelea wote walikuwa madikteta?
 
Mungu ninayemwamini na kumwabudu huwa Anasikiliza sala za kila mtu. Huenda sala yangu Ataisikiliza kuliko hata hiyo sala ya wachungaji kwa sababu nao ni binadamu tu kama mimi. Nitaendelea kuiombea nchi yangu bila kukoma na Mungu Ataiepusha na wingu hili zito linaloinyemelea. Sitaki nchi hii iingie katika machafuko wanawake na watoto waanze kuhangaika. Ingekuwa ni wanaume pekee aisee nisingekuwa na shida kabisa. Tungezichapa tu ili tuheshimiane. Tatizo machafuko na vita huwa havina macho mkuu na wahanga wakuu huwa ni wanawake na watoto...
Ni kwel kabsa anaweza kuisikiliza kulko hao maaskofu tena wakabaki wakishangaa jinsi ulivyojibiwa ,ili mradi usiwe mnafki,muuaji,mtekaji,mbakaji ...maana Mungu anasema maombi ya wenye dhambi ni makelele na machukizo mbele zangu ..
 
Wakiutoa waupeleke wapi?
Waraka wa Chadema kama chama cha siasa wanautolea bungeni ambako faru John na msaidizi wake wamejipanga kuhakikisha wanawabana wasifanye kazi yao.
Umesahau alivyoambiwa wewe wafukuze huko bungeni ili wakitoka huku tuwashughulikie
 
Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda (A.D. Bashite), alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.

Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito. Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Bashite) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.

1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni majasusi wa Chadema!

2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.

3.Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na uchawi.

4.Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.

5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe.

Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.
Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha
usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!

MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?

b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?

c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?

d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi.... nitawavunja miguu?”

e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?

f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?

g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?

h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?
Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.

Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)
 
napata tabu kuamini hii makala. musiba asubuhi alikuwa dodona. je kafikaje saa tisa dar ?

mbili mtukia kumwa imevumishwa sana, mange akipokomalia nakumbuka mtulia alijitokeza. sasa sielewi ukweki ni upi. ila time will tell!
 
Back
Top Bottom