Ansbert Ngurumo: Kikao cha siri ofisini kwa DCI kiliamua Mbowe na Wenzake wapelekwe mahakamani Jumanne wanyimwe dhamana

watanzania waliowengi ni watu wakusahau,sasa hivi wananyanyasika lakini ikifika kwenye kampeni sijui akili zao zinapumbazwa na nini mpaka wanasahau njia mbovu walizopitishwa,
 
Hii nchi imewekwa rehani yaani wanakaa vikao vya siri alafu siri zinavuja kibwege tu ndio maana yule PK anamburuza bwana yuleee maana ashaujua uwezo wake.
Pole kwa wote waliokutwa na kadhia hii Mungu awafanyie wepesi inshaallah ipo siku moja tu tutasema na hili limepita pia.
na litapita tu, maana hawataishi milele, ila wana hatari kubwa mbeleni, viongozi wanauwoga pia,wengine wanashindwa kukosoa wanaamua njia pekee ni kuvujisha siri tu, wengine hawapendi mambo ya serikalii basi tu wafanyeje na hali ndio imeshakuwa hivi, mpaka mtu unatamani kumuombea mabaya tu bwana mtukufu.....
 
Namba ya maajabu 26042018.

Nipo Butiama huku wazee wanapindua juu chini, lazima adate huyu jiwe


Na wazee wa Pemba wafanye Yao , wao wana jeshi sisi tuna mungu , jamani mungu Uwa anajibu mwenye haki faster
 
mimi nawaza tatizo ni katiba au, maana hata hii tulionayo inavunjwa!!! ningependa kazi kama Majaji,wakuu wa idara wawe wanagombe hizo nafasi na sio kuwekwa na mtu aliyepo madarakani, hivi unapewa nafasi na Mtu, eti kunauwezekano wakumkosoa kweli,haiwezekani, kila atakalotaka liwe hata kama ni wrong litakuwa hivyo hivyo


That is absolutely right. Hawana uhuru na kuna njia nyingi za kuwa punish.

Kwa mfano, yule Hakimu Mkazi Mkuu aliyekuwa ana rule sana kesi za dhamana za Lissu kwenye mashtaka ya kusema “dikteta uchwara” alipigwa transfer kutoka Kisutu kwenda mkoani, Bukoba huko kama sikosei, yeye na wenzake kama watatu hivi chini yake. Alikuwa ana run a very tight ship pale Kisutu, a no-nonsense adherent to the letter of the law. Wakampiga buti pale bana.
 
Kuna wale mahakimu walishtakiwa wakashinda kesi mahakamani. Jaji Mkuu akawa fire eti kwa manufaa ya umma baada ya kesi kuisha. Rais akasema nakupongeza sana Jaji Mkuu kwa kuwastaafisha kwa manufaa ya umma kwa vile, japo wameshinda, mke wa Kaisari hatakiwi kuwa na tuhuma.

Kwani hakimu kaolewa na Kaisari? Yani wanachezea haki za watu with total impunity...

Sasa jana Jaji Mkuu kapewa agizo kali: Ahakikishe serikali inashinda trillioni 4 za kesi za kodi.

Huko ndio ukisikia kuingilia uhuru wa mahakama! Kuwashinikiza mahakimu na majaji. The textbook definition of it. Sio watu wako bungeni au wamekaa kijiweni Manzese wanaongelea kesi za public figures unasema wanaingilia uhuru wa mahakama. Halafu wewe Rais unatoa order wazi wazi kabisa za kushurutisha majaji...
 
Mkuu majuzi nilienda maeneo ya Mbezi kwa Musuguli. Nikakuta vijana wametengeneza kibanda na kupaka rangi na kuchora nembo za CCM na kauli mbiu ya hapa kazi tu.
Walikuwa wanagombea kupiga picha kwenye lile banda.

Nilishangazwa sana tangu lini CCM ikapendwa huku kwa waliobomolewa tena uchaggani?

Nikapata ujasiri wa kuwauliza nyie mtaandamana kweli kwa mapenzi haya ya CCM?

Walinjibu kwa swali, Tuandamane kwa sababu gani?

Tunaandamana sababu tumeambiwa na mtu aliyeko marekani?

Watu wamebanwa kidogo tu kuhusu ufisadi na uwajibikaji wanataka tufe kwa ajili yao?

NB: Kwa jinsi nilivyoona huko Mbezi na mitaani naku hakikishia hakuna maandamano.
Hizi ni kelele za watu wachache mitandaoni. Hata tukianza kuwahesabu hapa JF hawifiki 600.

Mimi sio mwana CCM na niliwahi kuwa shabiki wa CHADEMA sasa sitaki kuwa shabiki wala mwanachama wa chama chochote bali shabiki wa Magufuli na shabiki wa mabadiliko ya kweli yanayoleta maendeleo, umoja na usawa ktk taifa.
Yan shabiki wa Magufuli usiwe Ccm tena kipinɗi hichi..!!! Utakuwa kisanɗuku wew
 
Kikao cha siri ofisini kwa DCI Alhamisi kiliamua Mbowe na wenzake wapelekwe mahakamani Jumanne 17:03:2018, wanyimwe dhamana, kupima joto. Leo Jumatatu katika kikao cha Mwanza, ukumbi wa BoT, kwa maagizo kutoka juu, azimio ni "kamata, funga, poteza, ua watu hawa" kabla ya 26:04:08

View attachment 726876
Bila shaka umeishapata mahali salama pa kuandika unavyotaka! Hongera sana!
 
Ccm imeamua kujuchimbia kaburi tanzania sio kisiwa

MACHIZI.jpg
 
Back
Top Bottom