Another ???MW Project in TZ


M

mambomengi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2009
Messages
829
Likes
24
Points
35
M

mambomengi

JF-Expert Member
Joined May 16, 2009
829 24 35
Wachina kupitia benki yao ya Exim wamesaini mkataba wa kuikopesa serikali ya Tanzania karibu dolla za kimarekani billioni moja (1bn US$) kujenga bomba la gesi lenye ukubwa wa inchi 36 kutoka kisiwa cha songosongo mpaka Jijini Dar es Salaam. Mkataba huo ulisainiwa uchina Jumanne iliopita. Waziri wa Nishati, J. Ngeleja (MB) ameeleza kuwa kukamilika kwa bomba hilo kutawezesha Tanzania kuzalisha 3,900 MW za umeme hivyo kujikwamua kutoka kwenye nishati tegemezi ya maji. Waziri Ngeleja amesema ujenzi wa bomba hilo utakamilika Desemba 2012.
 

Forum statistics

Threads 1,235,153
Members 474,353
Posts 29,213,380