Anne Kilango alalamika kuingiliwa jimboni na DC

Anne Kilango alalamika kuingiliwa jimboni na DC

Ha ha ha ha ha kadege lecture wangu wa CL pale UDSM.
Huyo Jamaa haishi vituko...


Umelazimishwa kutumia maneno ya kiingereza?

Akitumia Kiswahili atakuandikia 'mhadhili'!
Hapo utasema nini? Mojawapo ya changamoto za elimu yetu Bongoland ni kwamba hatuweki mkazo wala mikakati ya kumudu vizuri lugha zote mbili, Kiswahili na Kiingereza. Tupo tupo tu.
 
Rekebisha title ya bango lako.Ulipoanza na maneno 'aibu' 'aibu' nilidhani huyo mama kaingiliwa nyumbani kwake na majambazi na kufanyiwa jambo baya.Kwenye siasa hakuna aibu, kuna ujasiri tu na kujiamini.
 
Ha ha ha ha ha kadege lecture wangu wa CL pale UDSM.
Huyo Jamaa haishi vituko...

wanajuana hao
"Lecture=Lecturer"msomi wa UDSM ebu mnawaangusha waliosoma chuo hicho, maana hata unashindwa kutofautisha lecture na Lecturer, ungeweza kutumia neno Mwalimu lingetosha. Wasomi wa siku hizi ni shida sana na kwanini usiandike na kuisoma post yako kabla ya kuirusha hewani.
 
Mkuu hii kitu siikubali kabisa. Unaacha kuwa Lecturer unaenda kufanya kazi ambayo haina hata "Job Description".

Job Description ya Mkuu wa Wilaya ni "mwakilishi wa Rais" wilayani. Mkuu u-DC unalipa kuliko u-Lecturer; ni lecturer gani anatumia yale ma-V8 ya wakuu wa wilaya? Kwa vyuo hayo wanayo ma-VCs na high rank professors and deans of faculties. Sasa Mwl. Kadege ka-course kenyewe ni "CL" hakawezi hata kupata donor funded project angalau wakapata kasafari unategemea asikimbilie u-DC ambako anapata marupurupu kibao hadi walinzi na watumishi wa ndani pamoja na hadhi ya kupeperusha bendera ya taifa.

Wala simshangai Kadeghe hata ningekuwa mimi ningefanya hivyo hivyo. By the way, hajapoteza, term yake ikiisha bado ataendelea na u-lecturer wake wakati ameshakuwa na mali kibao ikiwemo mashamba kila kona ya nchi vitu ambavyo asingekaa avipate.
 
Umesoma chuo kikuu umetoka mtupu kama ulivyoingia..lecture wako ndio nn???

"nn" ndio [sic] nini? Ni lugha gani hiyo? ".." katikati ya sentensi ni uandishi wa wapi? Je, alama tatu za kuuliza zikifuatana "???" maana yake ni nini? Neno "ndio" [sic] kama ulivyolitumia, maana yake ni nini? Ulisoma shule kweli wewe? Na kama ulipata kukaa darasani, nachelea kusema "ulitoka mtupu kama ulivyoingia".
 
Ha ha ha ha ha kadege lecture wangu wa CL pale UDSM.
Huyo Jamaa haishi vituko...

wanajuana hao
mkuuu namkumbuka sana mikwara ya kadeghe na vitabu vyake vya cl anaetulazimisha kununua
 
Kwa nini wanasiasa ni walalamishi? Kwani ukiwa mbunge ndiyo unamiliki jimbo?
 
Humu JF watu tubadilike na tukue jamani, yani mtu ameandika neno akasahau herufi tu, watu mnamzodoa hadi mnahoji elimu yake, Ivi tangu umeanza kusoma hukuwahi kumsikia hata mwalimu wako akichapia maneno. Mbona ni kitu cha kawaida mtu kukosea??? Mtu unaacha kuchangia kilichoandikwa, unatafuta makosa madogo ya kiuandishi wakati ulimwelewa anamaanisha kitu gani. TUACHE UJINGA HUU!!!

yani = yaani, kiswahili tu huwezi utaweza kichina wewe?
 
"Lecture=Lecturer"msomi wa UDSM ebu mnawaangusha waliosoma chuo hicho, maana hata unashindwa kutofautisha lecture na Lecturer, ungeweza kutumia neno Mwalimu lingetosha. Wasomi wa siku hizi ni shida sana na kwanini usiandike na kuisoma post yako kabla ya kuirusha hewani.
Ndiyo matatizo ya big results now. What matters today is quantity. Tunajivunia wingi wa wahitimu, si ubora wao. Juzijuzi tumesoma humu order ya hakimu mkazi mwandamizi huko Musoma, ilikuwa kituko.
 
Ndiyo matatizo ya big results now. What matters today is quantity. Tunajivunia wingi wa wahitimu, si ubora wao. Juzijuzi tumesoma humu order ya hakimu mkazi mwandamizi huko Musoma, ilikuwa kituko.

Ndg yangu ni hatari tupu.Ila inatia aibu pale anapopewa ofisi kuonyesha alichokisoma kwa vitendo.Basi hili ni Janga la kitaifa maana vyeti wanavyo lakini vichwa ni Vitupu.
 
Aedit nini wakati yeye anaamini yupo sawa?
Kadege ana shida zake, kuna siku nimemsikia maeneo ya Ubungo akiwatishia vijana kwamba yeye ni mkuu wa wilaya atawaweka ndani. Nadhani ubongo wake hauko sawa, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi aje kuwasweka ndani wananchi wa Kinondoni!

huo ndio ushamba wa viongozi wengi wa magamba .
 
Back
Top Bottom