Anne Kilango adaiwa kudanganya; Ni Kuhusu kiwanda cha Tangawizi Same, hakuna kiwanda ni kiini macho

Z
same
 
Wakuu,

nawahakikishieni huyu mwandishi hajafanya kazi ama ameifanya kisiasa. Jamani kiwanda kipo kata ya Mamba
nimefika huko mwezi wa Tano kilikua mwishoni kuanza kazi, majengo yamekamilika, machine zilikua zimefungwa
n.k kulikua na tatizo la drier.

hofu yangu ni namna mwandishi ameandika hii habari. ANASEMA HAKUNA KIWANDA. Nasema sio kweli

lakini umiliki wa kiwanda sijui ni nani lakini halmashauri ya wilaya ina mkono wake through DADP program, wabia
wachache niliombiwa ni hao umoja wa wakulima wa tangawizi (ethics haziniruhusu ningeweka picha).

Hofu yangu sio huyo mama kasema nn ama wananchi wamefaidikaje na kiwanda hicho bali mwandishi kusema hakipo.

Je ameenda Mamba akakikosa?

Je ameuliza kwenye halmashauri ya wilaya (DED, ama afisa biashara, Kilimo & Ushirika) walau kuandika story kamili?

Je, kinachogombewa na mtoa habari ni faida za kiwanda? ama kuwepo kwa kiwanda (structure and machine)?

Je tatizo ni kiasi cha hela zilizotumika?

Naomba kuwakilisha - Kiwanda kipo (kina thamani gani sijui, kinamilikia na nani sijui, kimewafaidishaje wana same sijui) hata mlemavu wa macha anaweza kukiona.
 
mwanzoni alijifanya ni mwiba wa mafisadi akaitwa kakatiwachake sasa ni mfuasi muaminifu wa mafisadi!!

Mkuu huyu mama hata mie kuna kipindi alinigusa kwa jinsi alivyokuwa akibwabwaja na kuonekana ni kweli mtetezi wa wanyonge. Lakini kama hili lina ukweli, basi serikali ya magamba inazidi kujidhihirisha ilvyokaa madarakani kwa kulaghai wananchi. inatia huzuni sana, lakini inatia hasira kwa huyu mama. sasa akirudi jimboni anawatazama vipi wananchi, au ndo zile walizozoea kuwafanya watanzania hamnazo???
 
Waandishi waingie Same chap watuletee full details za hicho "kiwanda" na picha!
 
Waandishi waingie Same chap watuletee full details za hicho "kiwanda" na picha!

kiwanda kipo .msichanganywe hii vita ya magamba baina ya simba na kilango uwt .msisahau mahusiano ya gazeti mtanzania .rostamu na mama simba .cdm aituhusu .
 
Wakuu,

nawahakikishieni huyu mwandishi hajafanya kazi ama ameifanya kisiasa. Jamani kiwanda kipo kata ya Mamba
nimefika huko mwezi wa Tano kilikua mwishoni kuanza kazi, majengo yamekamilika, machine zilikua zimefungwa
n.k kulikua na tatizo la drier.

hofu yangu ni namna mwandishi ameandika hii habari. ANASEMA HAKUNA KIWANDA. Nasema sio kweli

lakini umiliki wa kiwanda sijui ni nani lakini halmashauri ya wilaya ina mkono wake through DADP program, wabia
wachache niliombiwa ni hao umoja wa wakulima wa tangawizi (ethics haziniruhusu ningeweka picha).

Hofu yangu sio huyo mama kasema nn ama wananchi wamefaidikaje na kiwanda hicho bali mwandishi kusema hakipo.

Je ameenda Mamba akakikosa?

Je ameuliza kwenye halmashauri ya wilaya (DED, ama afisa biashara, Kilimo & Ushirika) walau kuandika story kamili?

Je, kinachogombewa na mtoa habari ni faida za kiwanda? ama kuwepo kwa kiwanda (structure and machine)?

Je tatizo ni kiasi cha hela zilizotumika?

Naomba kuwakilisha - Kiwanda kipo (kina thamani gani sijui, kinamilikia na nani sijui, kimewafaidishaje wana same sijui) hata mlemavu wa macha anaweza kukiona.

What we need is the project and not properties..... majengo yanasaidia nini kama hakuna uzalishaji (production) ambayo ndiyo inaleta ajira na soko la zao husika .... hii project huyu mama amehubiri nayo na kudanganya muda mrefu sasa... sijui kwanini unatetea usanii huu ... au wewe ni PR wa huyu mama wa kipare

Hebu tuambie .... kama kiwanda kipo kimeshanunua zao la tangawizi kwa wakulima na kuzalisha chochote

Think twice ... mwandishi yupo makini zaidi yako
 
kuelekea uchaguzi wa UWT..........................!?!?!kazi kwelikweli,naona mnyama at work!
 
Sasa naanza kupata na mashaka. Nikiwa Arusha nimepewa zawadi ya tangawizi inayozalishwa na kiwanda kinachobishaniwa hapa. Na wala hakuna alama kuwa ni kiwanda banda, hapa packing imefanywa kwa kisayansi na seal!! Ninahofia sio mleta habari tu, bali chanzo cha habari.
 
OSOKONI

Kama wewe ndio mwandishi wa habari hii be very carefully. kiwanda kipo mimi
mwenyewe nimekiona naweza hata kukupa baadhi ya parameter zake.
Mimi nilienda kwa lengo la kufanya utafiti wangu kwenye mboga mboga na nimekiona
na walikua kwenye final stage ya kulaunch.

Kama ni mwandishi wa habari basi anzia wilayani ama ofisi za kilimo (ndio wasimamizi wa mradi)
vinginevyo naona kama hii habari unataka kuianika kwenye gazeti kabla hujafanya hivyo jiridhishe.

suala la kuwanufaisha wapare/wakulima ni kitu tofauti mimi siwezi lisemea ninachoweza kusema kiwanda
kipo. processing capacity yake ni 4000 metric tones, Same ginger production yake ni around 12,000 metric tones

Weka details hapa kipo eneo gani plot namba ngapi, block namba ngapi na ikiwezekana weka picha. Wacha porojo hapa! Haponi mtu hapa kwa wizzi na janja janja tu.
 
Mkuu huyu mama hata mie kuna kipindi alinigusa kwa jinsi alivyokuwa akibwabwaja na kuonekana ni kweli mtetezi wa wanyonge. Lakini kama hili lina ukweli, basi serikali ya magamba inazidi kujidhihirisha ilvyokaa madarakani kwa kulaghai wananchi. inatia huzuni sana, lakini inatia hasira kwa huyu mama. sasa akirudi jimboni anawatazama vipi wananchi, au ndo zile walizozoea kuwafanya watanzania hamnazo???
Akifika jimboni akimwaga pilau, kanga kofia t-shirt na bukubuku watu wanasahau habari ya kiwanda wanampa tena kura life goes!!
 
Hivi hapa mnabishania nini? kama kiwanda kipo si mpige picha na ushahidi uwekwe hadharani? Ingawa mimi siyo Mpare nimewahi kusoma kwenye gazeti moja siku nyingi kidogo kuhusu kiwanda hicho. Mwandishi aliyeandika habari hizo alifika huko na picha aliweka. Sasa wewe unayesema hakipo una maana gani? Tuonyeshe basi hayo majengo yanayooza.

Hapa hakuna haja ya picha ukweli ni kwamba kuna majengo ya toka mwaka 2009 lakini kiwanda cha kusaga tangawizi hakipo, kama kipo kingekuwa kinafanya kazi na baada ya mwaka JK angeenda kukifungua tayari kikiwa kazini, kwani kama Kilango alivyosema hicho kiwanda ili kianze kazi lazima kimsubiri Kikwete, kwani Kikwete ndiyo Mhandisiau meneja wa kwenda kukiendesha. pale kilichopo ni siasa tu Kilango alianza kuvuruga utaratibu wa hicho kiwanda toka mwanzo.
 
Picha nilizo nazo tayari nimeziweka kwenye report niliyokuwa naifanyia kazi so siwezi kuziweka.

Sijawahi kufanya kazi za siasa na wala sitarajii. Mimi nimeweka mawazo yangu CLEAR

KUSEMA KIWANDA HAKIPO SIO SAHIHI mwandishi aseme alichokiona na huo ndio uliko ugomvi wangu
na mwandishi wa habari hii na Sio kumtetetea Magamba Kilango

Unapokua mwandishi wa habari lazima uwe neutral kwa kiasi fulani. Mimi sijui anayetuhumiwa kachangisha
kiasi gani ameiba kiasi, bali ila hofu yangu ni mwandishi kutuaminisha umma wa watanzania kwamba kiwanda hakipo.

Sema majengo yapo machine zimeingia mitini ama sema hela zilichangwa kwa ajili ya machine na vitu vingine zimeliwa

Mimi nimeona Majengo, ya kusindikia, ofisi, store nk(kama food processing layout ya TBS inavyotaka) niliona machine kutoka SIDO, machine za kuchabanga na na kusaga zenye capaicity mbali mbali zikiwa zimefungwa. Niliona drier ikiwa bado haijamaliziwa kufungwa. hayo ndio niliyoona na picha ninazo ila nimeshaziwakilisha kwa wahusika.

kama machine zimefunguliwa baada ya mimi kupita hilo sijui mwandishi ulietembele naomba utujulishe ulichokiona tofautin nilichokiona mimi two and half months ago ndio nimepita huko.

Tufike mahali waandishi tuache ushabiki tuseme yaliyo kweli kama Kilango kala hela tuseme kala hela na sio kufabricate story. Kama kweli ulienda mbona huna hata picha? wewe hii habari ya hakuna kiwanda umeitoa wapi ama huyo mtu uliyezungumza nae kwenye simu?

Niko tayari kuomba radhi kwenye jukwaa hili kama utaweza kuthibitisha hakuna majengo na hizo machine.

Nawakilisha, GIZA NI KUTOKUWEPO KWA MWANGA, NA UONGO NI KUKATAA UKWELI.
 
kilimo_kwanza_fund_raising_2011.jpg

Mamba Ginger Growers fundraised in order to start a factory for processing ginger in order to add value to this product. Ginger is fast becomming among the major agricultural products of some areas in Kilimanjaro region including Myamba area where the Mamba Ginger growers rural cooperative society Ltd is based.
 
Back
Top Bottom