Anne Kilango adaiwa kudanganya; Ni Kuhusu kiwanda cha Tangawizi Same, hakuna kiwanda ni kiini macho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anne Kilango adaiwa kudanganya; Ni Kuhusu kiwanda cha Tangawizi Same, hakuna kiwanda ni kiini macho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 20, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  JUMATATU, AGOSTI 20, 2012 07:43 NA MWANDISHIN WETU, DAR ES SALAAM

  *Ni kuhusu Kiwanda cha Tangawizi Same
  *Yadaiwa hakuna kiwanda ni kiini macho


  MBUNGE wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango, anadaiwa kuudanganya umma kuhusiana na kuwapo kiwanda cha Tangawizi cha Mamba Ginger Growers Rural Co operative Society, katika Kata ya Mamba wilayani humo.

  Inadaiwa kuwa, maelezo anayotoa kwa umma kuhusiana na kiwanda hicho si ya kweli, kwa vile hakuna kiwanda cha tangawizi bali ni kiini macho.

  Akizungumza na MTANZANIA kwa niaba ya wakulima wenzake, mmoja wa wakulima wa tangawizi kutoka Same, Helieli Msolo, alisema kusema kweli Same hakuna kiwanda cha tangawizi ni usanii mtupu.

  "Unajua ndugu mwandishi hawa wanasiasa wetu, wanapenda kutumia vitu kwa maslahi yao. Huyu mama anasema Same kuna kiwanda ni kiwanda gani hicho?

  "Mimi ni mkulima wa tangawizi lakini hivi sasa najuta kwa sababu hakuna tena biashara, kwa kuwa wafanyabiashara wametukimbia na kinachoendelea sasa ni usanii," alisema Msolo.

  Alisema kitu kinachoelezwa kuwa kiwanda ni sehemu ambayo haina hadhi hata kuwa na banda la ufugaji.

  "Hakuna kiwanda kwa ajili ya kumnufaisha Mpare na hadi sasa wameamua kuachana na kilimo cha tangawizi na kuhamia kwenye kilimo kingine.

  "Yaani mtu anasema kuna kiwanda wakati kitu hakina hata hadhi ya kuitwa karakana. Wito wangu kwa wanasiasa, hebu yanapokuja maslahi ya wananchi, waache masuala ya siasa pembeni kwa kuwa matokeo yake sasa tumekosa lile soko tulilokuwa tunapata zamani, ambalo tulikuwa tunapata wateja kutoka nchi mbalimbali," alisema Msolo.

  Alisema mwezi uliopita Rais Jakaya Kikwete, alikuwa aende kufungua kiwanda hicho, lakini kutokana na taarifa za kuwapo usanii huo hakutokea.

  "Ilikuwa Rais aje lakini nafikiri kuna watu walimshtua kwamba hakuna kiwanda ni usanii kwa hiyo hakuja. Baada ya kumwalika Rais ulifanyika usanii wa kusaga tangawizi kiasi na kuifungasha ili aje aone kwamba kuna kiwanda, lakini hakuna kitu kama hicho.

  "Umma utambue kuwa hakuna Mpare anayenufaika na hicho kinachoitwa kiwanda na hakipo," alisema Msolo.

  Alisema Anne Kilango amekuwa akitangaza na kufanya harambee, lakini hakuna fedha zilizopelekwa kwa ajili ya kuendeleza hicho anachokiita kiwanda.

  "Mwandishi tena ikiwezekana mfanye mpango mfike huku, ili muone kinachoendelea na si kudanganya umma. Ilifanyika harambee na fedha nyingi zilikusanywa, lakini hakuna kitu kilichofanyika," alisema Msolo.

  Mkakati wa kiwanda hicho unaelezwa kufanywa na wananchi ambao lengo lao lilikuwa kuwa na sehemu moja ya kuweka zao lao waweze kuuza kwa pamoja, lakini baadaye mama Kilango alichukuwa kama wazo la kuanzisha kiwanda.

  Mkakati huo ulikwenda pamoja na Rais Jakaya Kikwete kuwa mgeni rasmi katika harambee iliyofanyika Dar es Salaam, ambako Sh milioni 300 zilipatikana ikiwa ni ahadi pamoja na fedha taslimu.

  Inadaiwa kwa makadirio ya uanzishwaji wa kiwanda hicho unakaribia Sh bilioni 1.5, lakini hadi sasa fedha zilizokusanywa katika harambee hiyo hazijafanya shughuli yeyote.

  Juhudi za kumpata Anne Kilango Malecela kuzungumzia suala hilo kwa siku mbili mfululizo, hazikuzaa matunda kwa vile simu yake ilikuwa haipatikani na hata ujumbe uliotumwa kwake haukuweza kujibiwa

   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  kama ni kweli hakipo basi ni tatizo
   
 3. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Tanzania ni zaidi uijuavyo!!
   
 4. a

  afwe JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Tutajua mengi, tusubiri tuone
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,892
  Trophy Points: 280
  huyu mama mnafiiki kitambo sana
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  CCM Nyumba ya MAFISADI... KILA KITU WIZI... Lakini wakisikia chochote toka CHADEMA wanapata ULAJI wanaunda tume ya WATU

  30 Kuichunguza CHADEMA pesa zimetoka NJE; Sasa hao watu 30 wataenda ULAYA kutafuta hao Wafadhili wa CHADEMA, watatumia

  Maelfu ya $$ Si wangezitumia kuwalipa Ma-Doctor na Waalimu... Hapana bajeti hiyo hakuna...
   
 7. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Ni kuhusu Kiwanda cha Tangawizi Same
  Yadaiwa hakuna kiwanda ni kiini macho

  MBUNGE wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango, anadaiwa kuudanganya umma kuhusiana na kuwapo kiwanda cha Tangawizi cha Mamba Ginger Growers Rural Co operative Society, katika Kata ya Mamba wilayani humo.

  Inadaiwa kuwa, maelezo anayotoa kwa umma kuhusiana na kiwanda hicho si ya kweli, kwa vile hakuna kiwanda cha tangawizi bali ni kiini macho.


  Akizungumza na MTANZANIA kwa niaba ya wakulima wenzake, mmoja wa wakulima wa tangawizi kutoka Same, Helieli Msolo, alisema kusema kweli Same hakuna kiwanda cha tangawizi ni usanii mtupu.

  “Unajua ndugu mwandishi hawa wanasiasa wetu, wanapenda kutumia vitu kwa maslahi yao. Huyu mama anasema Same kuna kiwanda ni kiwanda gani hicho?

  “Mimi ni mkulima wa tangawizi lakini hivi sasa najuta kwa sababu hakuna tena biashara, kwa kuwa wafanyabiashara wametukimbia na kinachoendelea sasa ni usanii,” alisema Msolo.

  Alisema kitu kinachoelezwa kuwa kiwanda ni sehemu ambayo haina hadhi hata kuwa na banda la ufugaji.
  “Hakuna kiwanda kwa ajili ya kumnufaisha Mpare na hadi sasa wameamua kuachana na kilimo cha tangawizi na kuhamia kwenye kilimo kingine.

  “Yaani mtu anasema kuna kiwanda wakati kitu hakina hata hadhi ya kuitwa karakana. Wito wangu kwa wanasiasa, hebu yanapokuja maslahi ya wananchi, waache masuala ya siasa pembeni kwa kuwa matokeo yake sasa tumekosa lile soko tulilokuwa tunapata zamani, ambalo tulikuwa tunapata wateja kutoka nchi mbalimbali,” alisema Msolo.

  Alisema mwezi uliopita Rais Jakaya Kikwete, alikuwa aende kufungua kiwanda hicho, lakini kutokana na taarifa za kuwapo usanii huo hakutokea.

  “Ilikuwa Rais aje lakini nafikiri kuna watu walimshtua kwamba hakuna kiwanda ni usanii kwa hiyo hakuja. Baada ya kumwalika Rais ulifanyika usanii wa kusaga tangawizi kiasi na kuifungasha ili aje aone kwamba kuna kiwanda, lakini hakuna kitu kama hicho.

  “Umma utambue kuwa hakuna Mpare anayenufaika na hicho kinachoitwa kiwanda na hakipo,” alisema Msolo.
  Alisema Anne Kilango amekuwa akitangaza na kufanya harambee, lakini hakuna fedha zilizopelekwa kwa ajili ya kuendeleza hicho anachokiita kiwanda.

  “Mwandishi tena ikiwezekana mfanye mpango mfike huku, ili muone kinachoendelea na si kudanganya umma. Ilifanyika harambee na fedha nyingi zilikusanywa, lakini hakuna kitu kilichofanyika,” alisema Msolo
  .
  Mkakati wa kiwanda hicho unaelezwa kufanywa na wananchi ambao lengo lao lilikuwa kuwa na sehemu moja ya kuweka zao lao waweze kuuza kwa pamoja, lakini baadaye mama Kilango alichukuwa kama wazo la kuanzisha kiwanda.

  Mkakati huo ulikwenda pamoja na Rais Jakaya Kikwete kuwa mgeni rasmi katika harambee iliyofanyika Dar es Salaam, ambako Sh milioni 300 zilipatikana ikiwa ni ahadi pamoja na fedha taslimu.

  Inadaiwa kwa makadirio ya uanzishwaji wa kiwanda hicho unakaribia Sh bilioni 1.5, lakini hadi sasa fedha zilizokusanywa katika harambee hiyo hazijafanya shughuli yeyote
  .
  Juhudi za kumpata Anne Kilango Malecela kuzungumzia suala hilo kwa siku mbili mfululizo, hazikuzaa matunda kwa vile simu yake ilikuwa haipatikani na hata ujumbe uliotumwa kwake haukuweza kujibu
   
 8. M

  Mzee Kabwanga Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hilo ndiyo tatizo la mbunge mkishamchagua anahamia Dsm.sasa Ana Kilango anaishi Dodoma atafanyaja kazi za maendeleo Same.
   
 9. m

  malaka JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli kwwli. Magamba yanazidi kuumbuka tu. Mnara wa babel ilikuwa kula mtu lugha yake mwishowe kitu hewan. Na hii sasa ni vilevile kila mtu anasema lake kupisha ukombozi. Mungu tujaalie watz.
   
 10. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  mwanzoni alijifanya ni mwiba wa mafisadi akaitwa kakatiwachake sasa ni mfuasi muaminifu wa mafisadi!!
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  I see......
   
 12. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  OSOKONI

  Kama wewe ndio mwandishi wa habari hii be very carefully. kiwanda kipo mimi
  mwenyewe nimekiona naweza hata kukupa baadhi ya parameter zake.
  Mimi nilienda kwa lengo la kufanya utafiti wangu kwenye mboga mboga na nimekiona
  na walikua kwenye final stage ya kulaunch.

  Kama ni mwandishi wa habari basi anzia wilayani ama ofisi za kilimo (ndio wasimamizi wa mradi)
  vinginevyo naona kama hii habari unataka kuianika kwenye gazeti kabla hujafanya hivyo jiridhishe.

  suala la kuwanufaisha wapare/wakulima ni kitu tofauti mimi siwezi lisemea ninachoweza kusema kiwanda
  kipo. processing capacity yake ni 4000 metric tones, Same ginger production yake ni around 12,000 metric tones
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  uongo kama huu wa viongozi ndio unaomtesa membe na jopo lake huko mzuzu sasa hivi ninavyoonandika hapa
   
 14. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  You dont know what you are talking about, Iam sorry I cant give you details but what I know only few depreciating buildings are existing there but no plant is there!
   
 15. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  kumbe ulikuta kipo bado kinajengwa? mm nikafikiri kuwa umekuta kina produce? nenda sasa kaangalie hiyo 4000 metric tones kama inazalishwa? na kwa nn rais hakwenda kukifungua tena??
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa stori hii nadhani Mtanzania wameingizwa mkenge.
   
 17. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli Nape ana habari na anasemaje? Mwisho wa mafisadi upo just around the corner!! Haya na nyie watani zangu kinachowafanya msiendelee na utaratibu wa kuwa na ile cooperative society ni nini? Achaneni na hawa matapeli dumisheni ile nguvu na sifa yenu maarufu ya ukokomavu na kujitegemea mjikomboe. Poleni sanaaa.
   
 18. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  kichakoro!! ha ha ha ha !!!!!!!!!!
   
 19. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Alafu ndo wanataka kumpa uwenyekiti UWT
   
 20. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Hivi hapa mnabishania nini? kama kiwanda kipo si mpige picha na ushahidi uwekwe hadharani? Ingawa mimi siyo Mpare nimewahi kusoma kwenye gazeti moja siku nyingi kidogo kuhusu kiwanda hicho. Mwandishi aliyeandika habari hizo alifika huko na picha aliweka. Sasa wewe unayesema hakipo una maana gani? Tuonyeshe basi hayo majengo yanayooza.
   
Loading...