Anna Tibaijuka Viwanja vyake watamnyang'anya?

Anna Tibaijuka Viwanja vyake watamnyang'anya?

watu wa kanda ya ziwa hawaguswi nasikia

Hawaguswi aise. Sasa hv kuna opereshenu kama kaskazini.
Waswahilli wansea hakuna marefu yasio na ncha. Magufuli nae atastafu tu sio mbali sana na yeye atasoma namba.
 
Mafisadi Mkuu wanajuana kwa viremba. Kumbuka issue ya akina Lugumi na Escrow. Huyu mama kuhusika kwake kupokea rushwa ya 1.6 billioni pesa za Escrow hakustahili hata kuendelea kuwemo Bungeni.
Alafu eti tunaambiwa kapatikana mtu asiependa rushwa!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huu sasa upotishaji, muweke na ushahidi, huyo mama hana eneo lolote huko kigamboni, kama angekuwa nalo, nijuavyo toka ameacha uwaziri wangesha mnyanganya kitambo sana. Acheni propaganda mufilisi.wekeni ushahidi mezan, mtu mmoja kumiliki viwanja 1000??mnaona jambo jepesi eeh. ..!Watz hataree
Mkuu kwa bongo kuwa na hivyo viwanja ni kawaida kabisa!kama mtu aliweza kubeba yale marumbesa ya Escrow itakuwa viwanja?au wewe mgeni bongo?
 
Hata lile ghorofa karibu na round about ya muleba-karagwe-bukoba linasemekana ni lake..jumba haliishi lile miaka nenda rudi,sasa kajumulo pale ndo sijui nianzie wapi
 
Zama hizi ni kanda maarumu hawaguswi ni kuteuliwa tu! Wataguswa wale waTeule wa JK na wale wa kaskazini n kanda ya mashariki wale wa upande wa pili wa dini hawatakiwi kabisa!! Kila zama na wakati wake
Sijui kwa nini mnakuwa Na siasa za ubaguzi namna hii, siku mikoa ya kusini itakapotambua siasa zenu za kibaguzi ndio utakuwa mwisho wa Tanzania moja yenye Amani.
 
Ukifika kigamboni eneo la kisotha kuna eneo kuna viwanja zaidi ya 1000
wenyeji hapo wanasema ni viwanja vya Anna Tibaijuka

na ukifika huko Mapinga Bagamoyo nako kuna story kama hizo

swali nalojiuliza je na huyu nae kama ni kweli watamnyang'anya?

au hii operesheni sio kila mtu?
Mama Anna ni mbunge wangu nimewahi kumuomba msaada wakati fulani wa ada ya semister baada ya kukosa mkopo wa chuo, alinijibu " kwa sasa nasomesha watoto wa Primary tu ndo uwezo nilio nao" nilipo mtaarifu kuwa basi nimuuzie shamba langu la urithi maana mmi ni Yatima alijibu "liko wapi hilo shamba nitakutafutie mteja" kumbe mteja alikuwa yeye! kwa thread hiyo hapo juu naungana na mtoa mada kuwa huyu mama anamiliki manyarubanja huko Muleba aliyoyapata kwa njia za kuwarubuni walala hoi.
 
Uyo mwana CCM mwenzetu
 
We kwel mwana propaganda kama ulivyo jiita. By the way alikujibu vyema kabsa, make watanzania kwakupenda kitonga hatujambo, sasa unashamba kubwa bado unataka upewe ada, si ulime ujisomeshe, Acha kupenda miterezo!!!!
 
Hata nzee nkapa nae huko mapinga Ana mzigo wa ekari sijui watamnyanganya au Ni kwa ajili ya wapinzani tu!?
 
We kwel mwana propaganda kama ulivyo jiita. By the way alikujibu vyema kabsa, make watanzania kwakupenda kitonga hatujambo, sasa unashamba kubwa bado unataka upewe ada, si ulime ujisomeshe, Acha kupenda miterezo!!!!
ni zao lipi tz linalo stawi kwa wiki mbili ambalo lingenisaidia kulipa ada ya semister ya kwanza.
 
hii habari sio ya kweli,bali Ni uchonganishi kati ya Prof na JPM,pamoja na watanzania,kipindi mama anasimamia mladi wa kigamboni kama waziri,baada ya kujiudhuru wanaamini Ni viwanja vya mama kumbe Ni vya serikali
 
Ukifika kigamboni eneo la kisotha kuna eneo kuna viwanja zaidi ya 1000
wenyeji hapo wanasema ni viwanja vya Anna Tibaijuka
na ukifika huko Mapinga Bagamoyo nako kuna story kama hizo
swali nalojiuliza je na huyu nae kama ni kweli watamnyang'anya?
au hii operesheni sio kila mtu?
Ana shamba kubwa hekari 3000 Muleba ukishakunja barabara ya kuelekea Chato, shamba limezinduliwa na Kikwete. Ajabu halijaendelezwa zaidi ya kuzungushiwa fensi na kujenga vijumba vya wafanyakazi. Huu uroho na umimi utamuua huyu mama.

Hawaangushani? Au wanabebana/ wananyanyuana?

RAIS Dk. John Magufuli, amemteua aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kumwakilisha katika mkutano wa makazi wa Habitat III unaofanyika katika mji wa Quito, Ecuador.

“Hivi sasa niko Geneva, Uswisi kwa matayarisho nikielekea Quito Ecuador mkutano wa makazi duniani wa HABITAT III kumwakilisha Rais wetu nikiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,namshukuru Rais kwa heshima hii kubwa, Sitamuangusha.

Link Rais Magufuli amteua Prof. Tibaijuka kumwakilisha ktk mkutano wa Habitat III

Link2. Prof. Tibaijuka amwakilisha JPM mkutano UN
 
Back
Top Bottom