Anna Mghwira Kuhubiri Injili ndani ya siasa

Chama kimebebwa na zitto,mama haoni haja ya kuendelea kutuma kwa matapeli wa kisiasa kwa kuwanufaisha.
 
Anna Mghwira kuhubiri injili siasa basi tena

HATIMAYE aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya ACT wazalendo Anna Mgwira mapema leo hii ameweka wazi hatma yake kisisa ambao amesema kuwa anageukia injili huku akiwa bado mwanasiasa.

Mgwira kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa amekubali ushauri alioshauriwa wa kuachana na Siasa na kugeukia injili, ila haweza kuiacha saisa moja kwa moja.

annamghwiraofficial @annamughwira
Nimeombwa niache siasa nikahubiri injili. Nakubali kazi ya injili ni wajibu mwema. Kazi ya injili ndani ya siasa ni wito maalum.

annamghwiraofficial @annamughwira
Kufuatia ombi la kuacha siasa kuhubiri injili ninafikiri nifanye Injili ndani ya siasa kwa sasa. Ninaamini mnanielewa. Asanteni

1a4f1309bd1d333c875e968467fc6d15.jpg
kibooooooo
 
Salamu zangu za kwanza zimfikie Gwajima.

Salamu zangu za pili zimfikie mama rwakatale.

Salamu zangu za tatu na za mwisho zimfikie mchungaji peter Msigwa.
Inasemekana Msigwa alichukua KITU cha maana kutoka kwa FISADI MKUU ili afunge mdomo!
 
Kuna chama huwa hakipendi ushindani, kinataka watu wa namna hii. Watafurahi sana na habari hii.
 
BG UP Mama Mgwira. Umechagua Fungu lililo Jema sana Kumtumikia Mungu.

Siasa ni Kuchafuana Chuki, uzabi zabina Majungu, umbea, kila Aina ya fitina ipo ndani ya Siasa.

Bora ufalme wa Mungu Maana Mungu ni Kweli Hamna hila Ndani yake.

Nakuombea Mungu Akutumie Kwa Utukufu Mwingi ili uwalishe Kondoo wake.
 
Alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Mkoa Singida lakin pamoja na uwezo wake Mkubwa wa kujieleza na kujenga hoja hakuwahi kufikiriwa hata kupewa udiwani wa kuteuliwa.
Nafasi yake ilikuwa ikichukuliwa na ndugu wa Mbunge
 
Alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Mkoa Singida lakin pamoja na uwezo wake Mkubwa wa kujieleza na kujenga hoja hakuwahi kufikiriwa hata kupewa udiwani wa kuteuliwa.

angekua wa Kilimanjaro fasta tu.
 
Sikujua kuwa sikueleweka kiasi hiki. Niliandika kuombwa si kutaka...niemombwa na msomaji mmoja niache siasa nikahubiri injili nikamjibu nitafanya injili katika siasa. Yaani ninataka kuchangia kuboreha siasa zetu ziwe rafiki kwa maendeleo yetu. Siasa si uhasama ni ushirikishaji wa hoja ili kupata hoja bora baada ya mjadala.
 
ok tulizani umeamua kuwa nabii dokta na mtume anna mgwira mama!
 
Back
Top Bottom